Nimeamua kuwatetea Lowassa, Chenge na Rostam

Lowassa ni mchapakazi anayeweza kubadili maisha ya watanzania.
Kwa kweli tanzania inahitaji maendeleo zaidi kuliko demokrasia

Kama alivyobadili maisha ya Monduli na wamasai kwa ujumla. Hivi sasa hawafugi tena, wanalinda na kusuka nywele wanawake! Hivi ni nani mnayemfanya ***** hapa. Amekuwa kwenye utumishi wa serikali kwa zaidi ya miaka 20 na hakuna rekodi yoyote ya maendeleo ya kujivunia aliyoifanya hata jimboni kwake na sasa hali ya Monduli ni mbaya kuliko hata wakati wa Sokoine. Tafuteni sababu nyingine siyo huo upuuzi wa maendeleo kwa watu wakati tulichoshuhudia ni wizi wa kutisha uliofanywa na yeye, familia yake na washirika wake wakubwa. Baba tafuta namna nzuri ya kulipa madeni kwa fadhila ulizofanyiwa, badala ya kichefuchefu hiki!
 
Acheni unafiki,tangu nianze kutembelea JF ni threads na posts za kuwaponda hao mapacha watatu, ghafla mmeanza kwatetea?Duuh.
 
Acheni unafiki,tangu nianze kutembelea JF ni threads na posts za kuwaponda hao mapacha watatu, ghafla mmeanza kwatetea?Duuh.
hapa hakuna unafiki mkuu, hapa ni suara la sheria, tuache kuwahukumu watu kwa tuhuma tuu, serikali ya kikwete inapashwa tuwapeleke hawa watu mahakamani ndipo iwafukuze kwenye chama kama si hivyo huu niuonezi mkubwa sana!
 
hapa hakuna unafiki mkuu, hapa ni suara la sheria, tuache kuwahukumu watu kwa tuhuma tuu, serikali ya kikwete inapashwa tuwapeleke hawa watu mahakamani ndipo iwafukuze kwenye chama kama si hivyo huu niuonezi mkubwa sana!

Ha ha haaa Hawawezi ndiyo Maana kutwa wanafanya Vikao Kuwashawishi wajitoe "ILI KUKINUSURU CHAMA"
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni

tunajua RA na Lowassa & family wametoa ajira kwa wengi wakati JK & family especially riz1 hatoi ajira tunaweza elewa hasira zako ulizozivalisha vazi la kizalendo huku ukiwa uchi unatetea fisadi huyu juu ya yule

hongera kwa ajira
 
Back
Top Bottom