JF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.
Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.
Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.
Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.
Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.
Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh
By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.
This is a challenge to you JF- hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.
Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
Heshima kwako ELNINO,Sawa kuna miscellaneous lakini kupita 5m target is vigumu - kwa mafano sasa hivi mpaka upandaji nitakuwa nimetumia 2m tu - palizi nitaweza kutumia 1m nyingine - uvunaji na kuhifadhi ni 3m approx
hata ukisema nipate magunia 20 kwa heka still jumla itakuwa tatal gunia 1000 times 60,000 = 60m ( Kadirio la chini kabisa)
Mie nigependa kuwa jirani yako! tuweke two big estates unasemaje?
Kwa nini usianze wewe na sisi tukufuate? joke. Mkuu kuna mapori mengi sana ambayo sio ya kununua ila kuokota tu basi, Mimi naamini tukiwa pamoja ki-jkt jkt hivi kambi itanoga.nikaribishe niwe jirani yako huko Kabuku,
nami nataka kununua ardhi kwa kilimo cha umwagiliaji
thanks
Mkuu MalilaKwa nini usianze wewe na sisi tukufuate? joke. Mkuu kuna mapori mengi sana ambayo sio ya kununua ila kuokota tu basi, Mimi naamini tukiwa pamoja ki-jkt jkt hivi kambi itanoga.
Mkuu Malila
nilekeze how to go about aquiring hilo farm,tuwesote ki-jkt,nipedata by PM,
nataka kulima embe na parachichi
Heshima kwako ELNINO,
Mkuu wangu bei ya mbegu ni tsh 3500/= per kilo,utatakiwa kutumia kilo 10 kwa kila eka. 3500 x 10 x 50 = 1,750,000/=.kulima eka moja si chini ya tsh 20,000/= x 50 = 1,000,000/=.kupanda eka moja si chini ya tsh 5,000/= x 50 = 250,000/=,kupalilia eka moja si chini ya 10,000/= x 50 = 500,000/= kuvuna,kuhifadhi [magunia & dawa],kupukuchua na kusafirisha ni gharama inategemea na umbali wa masoko.Mkuu gharama za chini kabisa weka 8,000,000/= pembeni kwaajili ya hiyo shughuli yako.
Naona at least watanzania kadhaa wana mawazo chanya. Kumbuka kuna kukosea mwaka pia (sikukatishi tamaa mm mwenyewe ni mkulima, lkn kuna jamaa yangu tulikuwa tukichuuza wote enzi hizo, alichimbia Tsh 50M kibaigwa kwa mategemeo ya kuvuna mabilioni, mwaka huo jua likawaka hakuvuna kitu-alitamani pesa hiyo angenywea bia!!). Kilimo kinalipa sana jamani ukienda nacho vizuri hauna haja ya kutumikishwa na mtu kwa mshahara wa milioni 20 kwa mwezi
Kilimo cha kutegemea mvua ni hatari,lakini kunamaeneo yana mito namifereji kiasi kwamba huhitaji nguvu kubwa kupata maji. Nendeni nje ya maeneo yenye majina makubwa mkaone mambo mazuri huko. Halafu yapo ni wewe kujimegea.