ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,128
- 49,863
Kwanza sijui kama hizi habari mnazo.
Ilianza ka Kuzuia kuingiza mahindi baada ya mavuno na Sasa muelekeo ni kukomesha kununua kabisa mahindi Nje ya Nchi hususani Tanzania.
Kulingana na Rais wa Kenya mwaka 2024 ndio itakuwa mwaka wa mwisho Kwa Kenya Kuagiza mahindi kutoka Nje ya Nchi na hapa mlengwa Mkuu ni Tanzania ambao tumekuwa tunategemea soko la Kenya.
View: https://twitter.com/TheStarKenya/status/1718631210212000222?t=ZxLz05RhTJGY9D3GhCRKOg&s=19
Kwa mantiki hii,Wizara ya Kilimo,Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Wizara ya Fedha na Wizara ya Mipango na uwekezaji kaeni chini Ili mtafute njia mbadala y kuhakikisha Kilimo Cha mahindi kinaendelea vinginevyo kitaanguka na kuja kuleta njaa baadae Kwa kukosa soko.
Ushauri wangu Kwa Serikali ni huu hapa ;
-Tuhamasishe Ufugaji wa Kisasa Ili mahindi yapate soko kwenye mifugo Kwa Kutengeneza chakula Cha mifugo kama kuku,nguruwe,Ng'ombe na Samaki.
-Tuweke deadline ya kupiga marufuku uuzaji wa mahindi ghafi Nje ya Nchi na hivyo kuhamasisha value addition na kuuza unga.Hapa kwenye unga tutunge sheria ya kufanya blending Ili uzalishwe unga Lishe Kwa viwango vitakavyoelekezwa.
-Tuanze kulima kimkakati na kutegemea soko la ndani zaidi ambapo Serikali ndio iwe mnunuzi Mkuu.Serikali ianzishe programu za chakula ch asubuhi na mchana Kwa Watoto wa Shule ambapo Wazazi tutachangia gharama kidogo ya chakula in terms of money.
-Tutafute masoko mengine Nje ya Nchi Kwa kuingia makubaliano maalumu na mashirika na Nchi Ili Wakala za Serikali ziuze chakula Cha ziada huko yaani NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko CPB.
Mwisho mwenye maoni mengine ya jinsi ya kukabiliana na Ukomwengu unaobadilika aweke hapa.
Mahindi ndio chakula Kikuu Cha Tanzania na ndio zao kuu la Biashara Kwa Zaidi ya nusu ya Mikoa ya Tanzania.
Kufanya mzaha ni Kuchezea na Uchumi wa watu na Ustawi wao.