Nimeamua kubadili mfumo wa maisha yangu, nimeamua kuanza na vikwazo hivi viwili

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
10,333
10,948
Wahenga walisema "jiongoze mwenyewe (kiakili) usingoje uongozwe". Wengine walienda mbali zaidi waliposema "Mkubwa hapangwi bali hujipanga". Hivyo ndivyo nilivyo amua kufanya kwa mwaka huu.

Kuna mengi naona yananichelewesha kufikia malengo yangu yakua tajiri (kwaamaana yangu) lakini hivi ni vikwazo ambavyo naona nisipoviacha vitanichelewesha ama kunifutia kabisa ndoto yangu.

Vikwazo hivyo ni BANGE & UMALAYA.

Nikianza na Bange, niseme tu kiroho safi kua nimeshavuta sana takriban miaka 15 sasa na sijaona ni kipi ninacho faidika nacho pindi nivutapo zaidi ya mazoea tu niliyo jijengea. Yaani ni kama kichangamshi tu cha akili na Mwili kiujumla. Zaidi ya hapo ni khasara tu.

Kwanza ni full pressure pindi nivutapo, yani kwamiaka yote niliyovuta nishakamatwa si chini ya mara 5 na marazote nimekua nagharamia kutoka polisi post.

Pili nimepiga hesabu pessa ninayo gharamia kwenye ulevi huu ni zaidi ya 100,000 kwa mwezi mmoja tu.

Tatu saikolojia yangu naiona tofauti na pale Mwanzo kabla kuanza kuvuta. Yani sometimes kuna vitu huwa navifanya mpaka mwenyewe nashangaa. Kununa hovyo, kuchelewa kupata usingizi ect.

Hivyo leo naamua kuachana na bange rasmi, nina imani navuta kwa ajili ya mazoea tu, hivyo mazoea hayo yapo ndani ya akili yangu na naweza kuyabadilisha mimi mwenyewe singoji mtu aje anisaidie sababu hakuna mtu anaefikiria ndani ya akili ya mwingine.

Jambo lingine ambalo nimeamua kuachana nalo ni Umalaya. Wanawake wananirudisha nyuma, hilo nimeliona kabla mtu mwingine hajaniambia. Japo hufanyaga kwa siri lkn nafasi yangu inanisuta na nisipoishinda changamoto hii Biashara zangu zitanishinda na nitawapa watu la kuongea.

Kwanza sioni sababu ya kugonga vimada wakati mm ni mume wa wake wawili tena mataifa mawili tofauti (Angola & Tanzania), nataka nini tena hapo?!

Nimegundua kuwa naishi kwa mazoea, sasa mazoea nataka niyakomeshe. Nina vikwazo vingi tu, lkn hivyo ni ambavyo nimeamua kuanza kupambana navyo.

Najua hata wewe unavyo vya kwako, naomba tusaidiane uzoefu jinsi ya kuvishinda vikwazo vyetu vinavyo sababisha tushindwe kufikia malengo yetu.

#KITO-MKATAKIMEO.
 
Yani ulikua uvuta bange ya laki moja kwa mwezi...hongera
 
Pia ni muhimu kutambua kwamba hiyo azma ya kubadilika na kusutwa rohoni/nafsini ni Mungu anakuvuta maana Neno la Mungu Biblia inasema kuwa Mungu hataki mtu yeyote apotee bali wote waifikie toba ya kweli.

Mradi umejitambua, ungama na tubu makosa yako ujipatanishe ma Muumba wako. Yeye atakupa nguvu ya kushinda vishawishi.

Pia mpokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako na utakuwa huru kweli kweli.

Tatu azimia kuishi sawa sawa na mapenzi ya Muumba maana Yeye ndiye anaejua yaliyo mema kwa ajili yako.

Kama utahitaji msaada zaidi tuzidi kuwasiliana.

Mungu anakupenda sana
 
Yani ulikua uvuta bange ya laki moja kwa mwezi...hongera
Mkuu inchi niniyopo kete moja inauzwa Cinquenta (50) sawa na 2500 TZ kwa kete moja.

Sasa mm kikawaida navuta kete 3 kwa siku.
Yani Asbuh moja, mchana moja na usiku moja.

Kwa siku moja ni zaidi ya Cento ccinquenta ( 150) 7500 kwa siku moja tu.

Hebu ifanye mara mwezi pesa hiyo itakuja shilingi ngapi za kitanzania ninazo ziangamiza kwa mambo ya kipuuzi?!
 
Kuna mstari nimesoma una wake wawili.....hata kuwa na hao wote ni kujitia hasara mkuu
 
Ahsante baba mchungaji kwa Ushauri wako wa kiroho, lakini mm bado ninaona mpaka Dini ni kikwazo pia kwa wanaadam wengi kuyafikia maendeleo. (Hapa naomba nisiulizwe chochote kuhusu hili la dini)
 
Kuna mstari nimesoma una wake wawili.....hata kuwa na hao wote ni kujitia hasara mkuu
Wapo sina khasara, tena hilo nalipinga kwa nguvu zote.

Kwanza kabla ya kufanya hivyo nilizingatia vigezo vingi tu ikiwepo kuakikisha kila MKEWANGU anakua msaada kwenye ndoa yetu.

MKEWANGU wa TZ (bimdogo) yeye anabishara zake na nilimkuta hivyo.

Kwanza yeye nilimuoa baada ya kunijia wazo wenda siku ikitokea nikaachana na huyo Angolana akaja akasepa na watoto wenyewe wote hivyo nikarudi TZ bila mtoto na ujana wangu nikawa nimepoteza. (Kumbuka waangola wanaamini mtoto ni wa mama baba shaidi tu)

Kuhusu huyo Muangola mwenyewe ni mfanya kazi (Mwalimu) nilimkuta chuo na mpaka leo tushazaa mtoto mmoja na anamimba nyingine.

Hivyo katika hilo sikuoa tu kuifurahisha nafasi?! Bali vigezo na masharti vilizingatiwa.
 
Hongera sana kwa kujitambua,

Wazungu wanasema "If u don't change yourself nobody will change you"

MUNGU awe nawe mkuu na kama ulikuwa husali jaribu kujiweka karibu na Mungu zaidi ili kujijenga kiimani zaidi,

Pia jaribu kuwakwepa marafiki wasiokuwa na mienendo mizuri ili shetani asije kukurudia na ukashindwa kufanikisha Azma yako uliyo dhamiria,

Tutaomba mrejesho toka kwako baada ya muda fulani ili tuweze kujua kama ulifanikisha ili na wengine wajifundishe kupitia kwako

ALL THE BEST MKUU.
 
Hongera sana mkuu umenifanya na mimi sasa niamue kuacha yote mabaya niliyotenda,ulevi umalaya uvutaji bangi na anasa zote hakuna ambacho sikuwahi fanya mpaka nahisi shetani ananishangaa jinsi nilivyo muumini niliyepitiliza kwake hakuna cha maana nilichofanya zaidi ya kuwa na madem kila mtaa ninaokaa tena wa permanent wasiopungua watatu acha viruka njia najaza semi ulevi ndo usiseme nahisi tumboni na depot bangi zimenifanya malazi yangu yawe mara kwa mara police station najionea huruma Mungu aniongoze nami niyashinde haya.
 
Mkuu inchi niniyopo kete moja inauzwa Cinquenta (50) sawa na 2500 TZ kwa kete moja.

Sasa mm kikawaida navuta kete 3 kwa siku.
Yani Asbuh moja, mchana moja na usiku moja.

Kwa siku moja ni zaidi ya Cento ccinquenta ( 150) 7500 kwa siku moja tu.

Hebu ifanye mara mwezi pesa hiyo itakuja shilingi ngapi za kitanzania ninazo ziangamiza kwa mambo ya kipuuzi?!
Mkuu mbona jani lao lina bei hvi aisee
 
Back
Top Bottom