Nimeamka asubuhi nikaenda kununua raia mwema, kumbe limefungiwa, nikasikitika sana.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Mimi ni msomaji mzuri sana wa gazeti la raia mwema. Ni aina ya gazeti ambalo kabla hujalisoma na baada ya kulisoma, lazima kutakuwa na tofauti kwenye afya ya ubongo.

Ni gazeti ambalo limejaa (healthy contents), siku zote lina habari zenye mantiki zilizoshiba. Nguvu kubwa ya hoja kwenye kila makala, na siku zote unakutana na watu wenye fikra pevu ambao unahisi kabisa kwamba walikuwa wanatafuta mahali pa kuyawekea hadharani mawazo yao na wakapapata.

Leo asubuhi kama kawaida yangu ya siku ya Jumatano, nikaenda kwa muuza magazeti wa hapa mtaani, nikatoa buku yangu mfukoni ili ninunue nakala yangu ya raia mwema, ghafla muuzaji akanikumbusha suala la gazeti hili kufungiwa kwa miezi miwili!!, nikabaki nasikitika ndani kwa ndani.

Na huu ni mwezi wa kumi kuelekea miaka 18 tangu Mwalimu Nyerere aage dunia, gazeti hili lingekuwa limejaa uchambuzi wa kina Prof Issa Shivji na wabobezi wengine wenye kumfahamu RIP Mwalimu.

Ni mpaka baada ya miezi miwili kuanzia sasa ndipo raia mwema litarudi mitaani, labda litokee na kutokea. Lakini inasikitisha kuona kwamba habari moja tu ndio inakuwa chanzo cha wasomaji wengine kukosa chakula cha ubongo kwa miezi miwili!!. This is so unfair.

Huwezi kukwepa kukosolewa, iwe na msomi mzoefu mwenye uzoefu wa kimaisha na kijamii, iwe na mtoto mdogo ambaye kagundua kuwa zipu ya suruali yako haijafungwa na nguo yako ya ndani inatazamwa na kila mtu
 
Ni gazeti ambalo limejaa (healthy contentes), siku zote lina habari zenye mantiki zilizoshiba. Nguvu kubwa ya hoja kwenye kila makala, na siku zote unakutana na watu wenye fikra pevu ambao unahisi kabisa kwamba walikuwa wanatafuta mahali pa kuyawekea hadharani mawazo yao na wakapapata.

Leo asubuhi kama kawaida yangu ya siku ya Jumatano, nikaenda kwa muuza magazeti wa hapa mtaani, nikatoa buku yangu mfukoni ili ninunue nakala yangu ya raia mwema, ghafla muuzaji akanikumbusha suala la gazeti hili kufungiwa kwa miezi miwili!!, nikabaki nasikitika ndani kwa ndani.

Na huu ni mwezi wa kumi kuelekea miaka 18 tangu Mwalimu Nyerere aage dunia, gazeti hili lingekuwa limejaa uchambuzi wa kina Prof Issa Shivji na wabobezi wengine wenye kumfahamu RIP Mwalimu.

Ni mpaka baada ya miezi miwili kuanzia sasa ndipo raia mwema litarudi mitaani, labda litokee na kutokea. Lakini inasikitisha kuona kwamba habari moja tu ndio inakuwa chanzo cha wasomaji wengine kukosa chakula cha ubongo kwa miezi miwili!!. This is so unfair.

Huwezi kukwepa kukosolewa, iwe na msomi mzoefu mwenye uzoefu wa kimaisha na kijamii, iwe na mtoto mdogo ambaye kagundua kuwa zipu ya suruali yako haijafungwa na nguo yako ya ndani inatazamwa na kila mtu
Nimewai siti..pole sana
 
Kama ulikuwa hujajua kama Raia Mwema limefungiwa JF inakufaa nini? Be the first to know, bwana.
 
Yaani we acha tu kwani kila Jumatano ninautakasa ubongo wangu kwa hilo gazeti. Miezi miwili ni mbali sana, labda nibane JF
 
Halijafungiwa ila limepigwa ban ya siku tisini,tuvumilie tu.
 
A
Mimi ni msomaji mzuri sana wa gazeti la raia mwema. Ni aina ya gazeti ambalo kabla hujalisoma na baada ya kulisoma, lazima kutakuwa na tofauti kwenye afya ya ubongo.

Ni gazeti ambalo limejaa (healthy contents), siku zote lina habari zenye mantiki zilizoshiba. Nguvu kubwa ya hoja kwenye kila makala, na siku zote unakutana na watu wenye fikra pevu ambao unahisi kabisa kwamba walikuwa wanatafuta mahali pa kuyawekea hadharani mawazo yao na wakapapata.

Leo asubuhi kama kawaida yangu ya siku ya Jumatano, nikaenda kwa muuza magazeti wa hapa mtaani, nikatoa buku yangu mfukoni ili ninunue nakala yangu ya raia mwema, ghafla muuzaji akanikumbusha suala la gazeti hili kufungiwa kwa miezi miwili!!, nikabaki nasikitika ndani kwa ndani.

Na huu ni mwezi wa kumi kuelekea miaka 18 tangu Mwalimu Nyerere aage dunia, gazeti hili lingekuwa limejaa uchambuzi wa kina Prof Issa Shivji na wabobezi wengine wenye kumfahamu RIP Mwalimu.

Ni mpaka baada ya miezi miwili kuanzia sasa ndipo raia mwema litarudi mitaani, labda litokee na kutokea. Lakini inasikitisha kuona kwamba habari moja tu ndio inakuwa chanzo cha wasomaji wengine kukosa chakula cha ubongo kwa miezi miwili!!. This is so unfair.

Huwezi kukwepa kukosolewa, iwe na msomi mzoefu mwenye uzoefu wa kimaisha na kijamii, iwe na mtoto mdogo ambaye kagundua kuwa zipu ya suruali yako haijafungwa na nguo yako ya ndani inatazamwa na kila mtu
Aya ya mwisho ndo yenye maana na ndo iliyobeba kile halisi unachomaanisha. Maelezo mengine yote ya awali ni bla blaa tupu.
 
Back
Top Bottom