Nimeacha kudharau wanaosoma vyuo tofauti na UDSM

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,043
2,000
Kwa kweli, nilikua nadharau sana watu ambao hawasomi au hawajasoma UDSM ila ulikua ni utoto tu, sasa imetokea nimeenda kufanya field practical pale TRA makao makuu, ebana nimekutana na vijana wanasoma kachuo flani kadogo tu kanaitwa ITA {Institute of tax administration} hata cjui kako wapi kwa hapa Dar, vijana wako vizuri sana katika masuala ya kodi, na TRA wanaonekana kuwakubali sana, kuna vijana wana diploma tu lakini mkwanja wanaovuta ni balaa.

Ninachotaka kuwashauri wadogo zangu ni hvi,usikimbilie kusoma udsm au chuo kingne chenye jina hapa bongo likozi la ajabu ili tu nawe uonekane eti unasoma udsm au chuo flan maarufu.kozi za udsm ni zle zle kama zinazotolewa na vyuo vingne hvo ushndani ni mkubwa sana katka soko la ajira,angalieni kozi ambazo zina channel za moja kwa moja katika ajira..

sasa we kimbilia bcom,bba,baf na zingne za aina hyo then uje usugue soli mtaani mpaka ufurahi.
 
Course za kienyeji enyeji hizo mpk data star na eagle wing wanazo...

Ukitaka kujua utamu wa udsm, kamata m/funzi wa CoET, CoNAS au kitivo cha sheria, then compare na m/funzi wa chuo kingine...

Nilikua field Puma Energy na w/funzi udom 3rd yr petro. Eng. M/funzi hajui kbs hata zile essentials ndogo ndogo, ukimwambia drilling rigs, blowout preventer, drilling bits, pipe tongs, drill pipe elevator, stingers, swellable packers, phase separation gas/oil mixture, oil dehydration and desalting, ata ukimwambia 2nd phase separation of oil-water emulsion anabaki anakutumbulia mijicho...

Hadhi ya UDSM ipo pale²
 
utagundua chuo hakikupi ajira au kujiajiri bali ni jitihada zako binafsi
hebu rudi mtaan uthibitshe hili gpa 2.0 kisa ud
 
Kwa kweli,nilikua nadharau sana watu ambao hawasomi au hawajasoma udsm ila ulikua ni utoto tu,sasa imetokea nimeenda kufanya field practical pale TRA makao makuu,ebana nimekutana na vijana wanasoma kachuo flani kadogo tu kanaitwa ITA{Institute of tax administration}hata cjui kako wapi kwa hapa dar,vijana wako vizuri sana ktk masuala ya kodi,na tra wanaonekana kuwakubali sana,kuna vijana wana diploma tu lakini mkwanja wanaovuta ni balaa.ninachotaka kuwashauri wadogo zangu ni hvi,usikimbilie kusoma udsm au chuo kingne chenye jina hapa bongo likozi la ajabu ili tu nawe uonekane eti unasoma udsm au chuo flan maarufu.kozi za udsm ni zle zle kama zinazotolewa na vyuo vingne hvo ushndani ni mkubwa sana katka soko la ajira,angalieni kozi ambazo zina channel za moja kwa moja ktk ajira..sasa we kimbilia bcom,bba,baf na zingne za aina hyo then uje usugue soli mtaani mpaka ufurahi.



Hongera kwakuacha utoto.
 
Tena makubwa,niko shirikani na staff tuko 57 lkn hakuna ht mmoja toka udsm. Ni watu toka saut,open university na vyuo vingine na tunafanya vzr tu.


Kwani huwez kudanganya juu ya hili?tutaamini vipi kua ni kweli hakuna wa UDSM?
 
Toa na wewe views zako na sio kudandia treni kwa mbele, sasa chuo kama St´Joseph cha wahindi utafananisha vipi UDSM? Chuo kama Josiah kibira na TEKU utafananisha vipi na MZUMBE?

huwa nawasikitikia sana watu wanaoshadadia dmi-st.joseph, ni majanga na I'm a victim.
 
wanafunzi wengi(sio wote) wa udsm wanakariri tu vitini ili wafaulu mitihani yao ndio maana hawapo competent ukilinganisha na vyuo vingine tena vinavyochipukia. Mfano nilivyokuwa field mwaka wa pili kwenda wa tatu, nilipata field tanesco makao makuu kufanya field ya accounting. Sasa ndipo nilipogundua wanafunz wengi wa udsm ni shalloow. wao kaz yao ni kujisifu tu kuwa wamesoma udsm na zarau nyiingi. Ila kwenye kaz ni f na wavivu. Mkuu wa kitengo akiwauliza maswali ya kawaida tu ya accounts hawajui hata kidogo, wakibanwa sana wanasema eti hilo swal ni la koz ya mwaka wa kwanza so hawakumbuki, yaan ni full aibu. Ila wanafunz wa tia na ardhi wapo vizur aisee had raha ingawa mimi sijasoma ivyo vyuo.
 
Back
Top Bottom