Niliyoyashuhudia Jeshini

Kabla hamjaanza kozi mnaitwa wazalendo. Kipindi cha uzalendo tulifundishwa sana chenja.

Moja ya chenja ilikuwa inaimbwa "yaule wema, ae yaulee wema. Mama wee mama wee utamu wa jeshi nauona eeh"

Baada ya kumaliza kozi, tukiwa safarini tunarudi makwetu, kwenye basi mmoja wetu akaianzisha hiyo chenja. Dah! Kuna feelings Fulani zinakuja hadi unahisi machozi. Unakuwa unakumbuka lifestyle yote ya jeshini, jinsi ulivyoungia na ulivyotoka.

Moja ya kitu nikichokipenda JKT, ni ile mnakutana watu karibu pande zote za Tanzania. Baadhi mnajikuta mnaelewana, mnakuwa mnaroll pamoja mda mwingi. Washkaji wengine mnakuja kukutana chuo, wengine haujui wako wapi, ukikumbuka ule ukaribu mliokuwa nao inahuzunisha sana.

Moja ya kitu nakikumbuka sana maisha ya jeshi ni upendo, Bakabaka sometimes anakuja na karanga (za.pakti), anawapa Kila mtu karanga mojamoja hadi zinaisha, wanatuambia jeshini upendo. Kwahiyo hata sisi makuruti kwamfano umefanikiwa 'kubasti' (kuongeza msosi) unawaita washkaji mnakula wote.

NB: kama Intro ingekuwa inafanyika Kila siku, kambi nzima tungetoloka
SOMETIMES BEST MEMORY MAKES YOU SAD, BECAUSE YOU KNOW THEY WON'T HAPPEN AGAIN🙏
 
SEHEMU YA 7
Nashangaa muda unaenda mbona haturuhusiwi kwenda kulala?
Yule bakabaka akastopisha kwata akasema hivi sasa ni saa 2 usiku muda bado kabisaa!
Kuruta tunaulizana muda bado kivipi akati tumetumia muda mwingi kombania.
kuruta wakisinzia wanapewa kazi ya kushindana kukimbia
Mimi sikua nasinzia nilikua najipa moyo muda simrefu tunaenda kulala ila wapiiiii.... kila muda bakabaka anasema ndo kwanza saa 2 kamili usiku.

Tunaimba chenja, mazoezi ya viungo kwenye mazoezi nilikua napenda viroba (squats) hata 100 nashuka tu nasihisi kuchoka. then bakabaka anasema hapohapo ulipo jilaze ulale! Basi watu fasta tunajilaza kwenye vumbi
Dakika 5 nyingi anasema inuka rukaruka kichura
Kuruta tulipata hasira hadi wengine wakaanza kusonya.

Hapa nilishangaa kitu! Kuruta anamsonya bakabaka halafu hafanywi kitu zaidi tu anasmile halafu anasema "kuruta fungua moyo huo"
Ila walikua wanaudhi fikiria mtu anakuambia lala ghafla ruka kichura anarudia mara nyingi zile hasira plus usingizi watoto wengine hawana adabu wanamsonya na yeye anablush tu.

Hamuwezi amini alfajiri ilifika tukishuhudia kwa macho! Sasa tunaulizana "mbona leo hatujaenda kulala?" Tutafanya nini ndo ishapita hiyoo

Tukapanga foleni mabio yakaanza, kama nilivyosema muda wa mabio niliupenda sana zile chenja ndo ugonjwa wangu nikawa nakimbia bila kutegea nafurahia kukimbia.

Tumerudi jogging uelekeo shambani, tukitoka shambani chai kuipata hadi ukimbie 2km, tukitoka chai uelekeo kwata
Sikupenda kwata nilikua nanga nimekula mabao mengi tu mpaka bakabaka akanichoka! Akaniambia labda utaweza vitu vingine kama ngoma coy, karate au kazi mchanganyiko.

Ratiba iliendelea mpaka wiki ikakata hatukurudi angani hatukulala wiki nzima!

Baada ya wiki sasa bila kulala! vituko vilianza mtu anachuma machungwa huku kafumba macho anaota kabisa
Mimi ile mabio nikawa nakimbia huku nasinzia, chenja naitikia miguu inaenda mbele lakini nimelala ila naota nakimbia.
Unaweza usiamini lakini hali ndio hiyo.

Bakabaka wakawa wanasema hawa itabidi leo wakalale wasije kutufia bure hapa!
Kitengo cha kuvuna machungwa tulikua tunapiga story sana na bakabaka.
Wiki ilipita bila kuoga.


Usiku ukafika mimi najua kabisa leo tunaenda kulala, nikawa na furaha , sasa muda unaenda ila haturuhusiwi, njaa ikawa inaniuma nikasema subiri nitoroke niende kunywa chai jikoni halafu nirudi fasta kombania nilihisi tulidanganywa leo tena tunakesha.

Lahaula nilijuta kwanini nilitoroka........

Itaendelea.

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
Pole ndiyo ukubwa huo
 
SEHEMU YA 13
MAOKOTO

mwanzoni kuruta wote tulipewa kopo la uani na sanitizer sisi tukajua ni upendo tunapendwa sanaaa na bakabaka.
Mwisho wa mwezi ukafika kuruta njoeni kuna maokoto yenu jeshi tunawapa iwasogeze siku.

Tumekaa kombania bakabaka kashika burungutu mimi jina langu ni herufi ya mwanzo kwahiyo hela nilikua napewa wa kwanza

Nikaitwa jina nikaenda nikapewa hela halafu nisign, nikapiga jicho kwenye amount iliyoandikwa ni tofauti na niliyopewa, nikimaanisha nimepewa nusu ya hela.

Wote tukapewa tukaanza kuulizana vipi mbona tumepewa hela nusu?
Bakabaka akatuambia "Mlivyokuja mlichukua makopo yetu na sanitizer mlidhani tumewapa bure?"

Ikawa kila mwezi tunapewa maokoto nusu kisingizio ety tulivyokuja walitupa makopo na sanitizer zao!

NADHARIA YA WANAJESHI KUTEMBEA NA KURUTI

NIilivyotoka nyumbani usia ulikua kua makini huko wajeda sio watu wazuri!
Nikiri kwa nilichokiona WANAJESHI MNAWASINGIZIA!

Labda kama hiyo tabia ipo kambi zingine lakini kambi niliyokuepo mimi wanajeshi walikua wanajiheshimu sana.

Hawakua hata hivyo kusema wanatusumbua kuruta hapana.
Ila wanaoharibu sifa ni wale service man, wale ni vichomi kazi nyingi tunakua nao hivyo wanachukua nafasi hiyo kupenyeza nia yao ovu.

Ole wako service man umkatae utapata adhabu kama zote.
Mzazi usiogope mtoto kwenda kwa mujibu, faida ni nyingi kuliko hasara

"If it's bitter at the start, then it's sweeter in the end"
Hongera sana kwa kumaliza, swali kwahiyo hao wasumbufu mlikuwa mnawakubali?
 
Hahaha mkuu umenichekesha sana aisee, mdogo wangu wa kiume alipangiwa maramba Tanga, Sasa yeye ni mweupe, siku amerudi ile wiki moja wanayopewa ya kuapply chuo na mkopo aisee kawa mweusi, kakondaa, mama alipomuona akamkumbatia tu huku machozi yanamlenga, kila saa tunampa mara matunda, mara supu, hafokewi yaani tulimhandle with care, baba na mama wote wamepita jkt ile mujibu ya mwaka mmoja na kaka etu mkubwa yupo jwtz wakampa mbinu mbinu na kumtia moyo hapo akarudi Tena.Ile program ilimtransform Sana dogo kwanza alirudi ile miezi mitatu ilipoisha ana furaha, self discipline ilikua juu sana, zamani kusafisha tu chumba chake mpaka mgombane, maji anaoga ya Moto lakini alipotoka kule anaoga mara 2 kwa siku bila kuambiwa Tena maji baridi anafanya mambo yake kwa wakati, yupo active, nilimfurahia Sana nikasema Jeshi kumbe linabadilisha watu.Mpaka leo anasoma MD mwaka wa 3 yeye ni mtu wa mazoezi tu , anacheza mpira wa miguu na kukimbia hizi mbio fupi, yupo kwenye timu ya chuo.Nilisema nikipata mtoto wa kiume lazima aende JKT mwaka mmoja.

Ahsante sana kuiona Taswira nzuri namna hiyo
 
1) Wewe service man alikujaribu kama ndio ilikuwaje?.
2) Namesake ulimtafuta tena kwenye maisha yako au bado mpaka sasa?.
3) Uliwacha jeshi?. Vipi na Anna yupo jeshi au nae karara mbele?.
4) Umetaja vitengo vi5 tu hivi jeshini hakuna kitengo cha spy,Medical na mechanic?.
5) Vyakula huja kwa msimu jeshi lina mfumo wa vyakula vya makopo?. Hivi hata siku ya vita vinaweza saidia jeshini kuwa na supply chain kwa wanajeshi kirahisi.
1. Kuna service alinitesa hadi naondoka, akinikuta nimeoga nimeng'aa ananipa adhabu ya kutoll ili nichafuke upya.

2. Nilimtafuta kwasasa sina mawasiliano yake.

3.Jeshi niliacha wote na Anna, course yetu ya miezi 3 ilipoisha tulirudi nyumbani.

4. Sisi kwa mujibu hatukua na hivo vitengo ulivyovitaja.

5.Hatukuwahi kupewa vyakula vya makopo.
 
1) Wewe service man alikujaribu kama ndio ilikuwaje?.
2) Namesake ulimtafuta tena kwenye maisha yako au bado mpaka sasa?.
3) Uliwacha jeshi?. Vipi na Anna yupo jeshi au nae karara mbele?.
4) Umetaja vitengo vi5 tu hivi jeshini hakuna kitengo cha spy,Medical na mechanic?.
5) Vyakula huja kwa msimu jeshi lina mfumo wa vyakula vya makopo?. Hivi hata siku ya vita vinaweza saidia jeshini kuwa na supply chain kwa wanajeshi kirahisi.
mujibu ni brash to yani kama mvua za rasha rasha... awawezi kukutana na vyakula vya kopo...wala biscuits zetu zile awazijui...vyakula hivyo ni vya cozi za walio sajiliwa. na kama ni ulinzi wanafundishwa wa kujilinda yeye mwenyewe sio kulinda wengine.

maana ile dhana kuwa mwanajeshi mmoja sawa na raia 100 haiwezi kuingia kwa hawa Mujibu...yani wanakuwa bado awana wanacho jua kuhusiana na Jeshi. wanafundishwa asilimia 10% ya mafunzo ya awali...

tuchukulie ni sawa na short course za Veta, mtu alie soma short course awezi kufahamu mambo kiu ndani kama alie maliza full course.

wao wana mjua mzabuni wao anae wapelekea mikate tu...!

kuku, nyama, mboga za majani na matunda vinapatikana hapo hapo maana kambi nyingi zimejikita kwenye uzalishaji wanafanya kilimo na ufugaji.​
 
mujibu ni brash to yani kama mvua za rasha rasha... awawezi kukutana na vyakula vya kopo...wala biscuits zetu zile awazijui...vyakula hivyo ni vya cozi za walio sajiliwa. na kama ni ulinzi wanafundishwa wa kujilinda yeye mwenyewe sio kulinda wengine.

maana ile dhana kuwa mwanajeshi mmoja sawa na raia 100 haiwezi kuingia kwa hawa Mujibu...yani wanakuwa bado awana wanacho jua kuhusiana na Jeshi. wanafundishwa asilimia 10% ya mafunzo ya awali...

tuchukulie ni sawa na short course za Veta, mtu alie soma short course awezi kufahamu mambo kiu ndani kama alie maliza full course.

wao wana mjua mzabuni wao anae wapelekea mikate tu...!

kuku, nyama, mboga za majani na matunda vinapatikana hapo hapo maana kambi nyingi zimejikita kwenye uzalishaji wanafanya kilimo na ufugaji.​
Course ya kujitolea nisingetoboa
 
Back
Top Bottom