Ushuhuda wa waliowahi kutusaidia tukapotezana nao kabla hatuwalipa fadhila

donga

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
2,475
4,926
Naamin jukwaa la JamiiForums ni dubwasha kubwa zaidi ya bahari..
Huenda tukakuta humu kuna watu wazuri walitusaidia lakini tukapotezana nao bila kurudisha fadhila ni vyema tukashare story huenda wahusika wapo humu****

Ngoja nianze kushare kisa changu

*****************

PART: I

Exactly ngoja na mimi nichangie lililonikuta
Nakumbuka 2015 ndio nimemaliza Advance shule X Kanda ya kaskazini.........

Basi bwana hili na lile kipindi kile awamu ya mkwere nikachaguliwa jeshi huko kusini mwa Tanzania, kambi 842Kj ( Mlale jkt, kwa wasiojua hii ni utambulisho namba ya kikosi)

Kwakuwa mzee alikuwa kikazi akisafiri safiri...akanipa nauli, pesa ya matumizi na hela ya guest ..net akuzidisha.
Basi bwana safari ilianzia dar tulipokiwepo tunakaa
Akanipakia kwenye bus ( Kampuni ya wale macho madogo) wakati naenda kupanda aliniambia maneno haya

"Mwanangu ww ni mtoto wa kiumbe lazma uishi kiume hivyo unajua kusoma na simu unayo ufike salama"

Nikamjibu Ahsante ila moyoni nilikuwa naogopa maana km unaenda mikoa ya kusini nimeishia kufika moro tu huko mbele nilikuwa sikujui I mean, iringa,njombe, mpaka songea

Safari ilianza Alfajiri saa kumi na moja..kimbembe kwanza nilikosa siti na deadline kuriport ilikuwa tarehe 15/june/2015 ...mimi nikawa nasafiri tarehe 14/june/2015

Mzee aliwaambia muwekeni popote ajibanze ila cha msingi afike ...konda akaniweka pale mbele kwa dereva ( wazee wa mabasi wanaita kwenye kigodoro 😁😄😄)

Safari ilienda mchana kutwa mpaka usiku hatimaye tukafika Songea saa sita usiku, Hebu kwanza kuna kakitu nimesahau ngoja niwajuze( Kwakuwa nilikuwa nimekaa kwenye kigodoro nikapewa task na konda ya kusupply vitrey vya dust bin 🥺😔😔, Nitafanyaje sasa ndio nimepewa kazi ....but good thing ni kwamba kila tulipokuwa tunashuka kula msosi kwenye hotel konda na dereva wakawa wananichukua kwenda kupiga MENU free yaani kwa kifupi nilikuwa chawa wa safari siku hiyo😁😁😁😁)

Basi bwana ile kufika stand kipindi hicho palikuwa panaitwa msamara sijui kama sahizi wamebadili jina maana sijafika tena huko.

Kufika stand show inaanza umeme umekata giza totoro vitorch tu unaviona...lakini kilichonishangaza sikuile sikuona nyumba zikiwaka taa kwa wale watumia majenereta na soral pannel sikujua kwann nikaamua kuachana nalo maana hilo sio lililonipeleka...Baadhi ya abiria walishuka wengine wakalala ndani ya gari

Mm huwa napenda hadithi sana kiasili hasa za masimulizi nikakumbuka kuna msemo niliwa usoma "NDEGE ASIYERUKA HAWEZI KUJUA WAPI ULEZI UMEKOMAA"

Basi nikashuka kuzungukazunguka usiju ule angalau nipate muhindi wa kuchoma....Ghafla pembeni muendesha tax aliniita akaniuliza unataka usafiri

Nikamjibu ....Hapana mm ni mgeni naenda jeshi kituo "Y" (Nishakitaja juu kule 👆) maongezi yaliendelea baadaye akasema km hutojali twende ukalale nyumbani kwangu na ukicheki simjui kabisa

Kweli nikakubali nikaenda nae mpaka kwake nikamkuta mkewe na mtoto mdogo umri makadirio km miaka 9 hivi wa kike na mwingine wakiume km miaka 15 hivi

Wakaniandalia màji nikaenda kuoga , Lakini wakati naenda kuoga nikapata hofu nisije kuibiwa kwenye begi langu..nikatoa pesa na simu ( Maana hizi ndio visa na passport za safari🤣🤣🤣).....nikaenda navyo bafuni

Kurudi nikakuta msosi pale na baba mwenye nyumba tukakipiga ipasavyo kile kiuno cha ray C ( Ulikuwa wali maharagwe) nikaandaliwa chumba tukalala na yule mtoto wa kiume miaka 15 chumba kimoja

Asubuhi kulivokucha akanipakia kwa tax mm na watoto wake ...akawapeleka shule na mimi akanipeleka stand kisha akaniandikia namba kwenye kikaratasi nikipata changamoto yoyote nimpigie but kitu alichokuwa hakijui alijua sina simu

Kufika stand picha linaanza naendaje kambini na sipajui ukicheki na ule mteru wa story za jeshi

Basi mwana ikabidi nijiongeze kwenda migahawani kunywa chai ....nikaingia mgahawa flani nikaagiza chai na viazi utamu (Kumbuka lengo langu halikuwa chai ila nilijua kupitia migahawa lazima tu nitakutana na Mates wenzangu wanaoenda kambini...swali je nitawajuaje? Kwangu nilikuwa naangalia kigezo kimoja tu body appearance yaani upara) japo mm nilikuwa cjanyoa

Kweli mle mgahawani niliwapata km watano hivi tukajioganise tukawapata wengine km kumi tukakodi hiace tiyari kwa kwenda kambini

Kufika getini kabla hatujaingia tukapokelewa na rolling na kucrow ukaanza ukaguzi pale na siku ile pale getini ndio nilidondosha ile karatasi yenye namba za simu but sikujua km sikuile ndio niliidondosha

Nikawa offline muda kwa mazoezi na simu tulipokonywa but baada ya six week kulikuwa na utaratibu wa kwenda out mjini wenye walikuwa wakiita siku ya kupunguza uzito kuruti( yaani mikasi au kwa lugha nyingine ku-downlod na ku-upload upwiru😄😄)

Sasa si ndio natafuta ile namba mzee akanitembeze mji wa songea dah I was so dissapointed bwana ile😔😔😔🥺🥺, karatasi siioni na nilipanga nikampe fadhira kidogo nilizosave pocket money na zile posho za jkt za mwezi

NAkiri huyu ni mtu muhimu pia niliyepotezana nae Although I was too teeneger na yeye he was like, my father

Kama hii story anahisi alikuwa ni yeye please nicheki pm alinisaidia sana kwanza aliniamin na mm sikumuangusha
 
Op kikwete hyo

Nilikuepo hapo miaka 50 ya muungano...

Wazee wa Magagula lusonga..chipole mission ..

Uelekeo Kwa kusekwa.
Sikukaa sana baada ya kuapa tuu kiangaiko ilifunguka na sis nikiwa teenager

Daaa nimepamis songea
 
Siwezi kusema ule ulikua ni msaada ila ila upendo alionionyesha yule dada mpaka leo natafakari bila majibu na bahati mbaya sina matarajio ya kukutana nae tena hata ningemwambia asante!

Mwaka 2006 Veta kihonda Morogoro, tulikua tumekaa wavulana kama nane, karibu wote walikua wachokozi , wahuni, na kila aina ya usumbufu wa vijana wa kiume.

Alipita dada mwanafunzi mwenzetu mbele yetu, moja wetu akamuta , yule dada akaja, alikua anakula pipi , wakimwambia tunaomba pipi yako, alijibu mpo wengi na pipi imebaki moja itakuwaje, mmoja wetu aka mwambia amchague mmoja wetu anayempenda ampe, yule dada alifunga macho akaja upande wangu akanipa mimi!

Ilinistaajibisha sana kwa vile mimi nilikua mtu nisie na swagga yoyote, mkimya na muoga sana, hata salamu kumsalimila mtu hususan wanawake nilikua mwoga!

Wakati wakiambiana na kuombana pipi mimi sikua nao kifikra kabisa, maana ninajijua sikua na mbele wala nyuma, nilikua nimekaa nao lakini sikua nimestahili kwa mwonekano na taswira yangu, nguo zangu na viatu nilikua duni sana japo ni uniform za shule lakini zilikua zimechakaa, sikua na sababu yoyote ya kuvutiwa na mtu kwa vyovyote.

Lakini dada watatu sijui aliona nini kwangu na kunipa thamani ile tena mbele ya watu wananicheka kila siku na kunibeza, sikuwahi hata siku moja kumsalimia dada wa watu lakini sijui ninini kilichomfanya akanithamini vile!

Wenzangu wale baada ya hilo wakamcheka eti amechagua huyo boya kwa vile hawezi kukusumba kwa lolote!

Hatukuwa na muda mrefu tuka maliza masomo, sikuwahi kumuona tena tokea hio 2006 , hata sikuwahi kujua ni mwenyeji wa wapi maana shule ile ilikua inachukua wanafunzi toka mikoa mingi.

Jina lake tu na taswira ya mwonekano wake ndio nimebaki nayo mpaka leo, alikua mweupe ambeye hasuki nywele, alikua anaitwa Mary.

Popote alipo asipungukiwe na lolote na Mungu ampe wepesi kati changamoto zote.
 
Haaaa unamkumbuka afande gani alikuwa wa kuogopwa sana

Na yale mashamba ya embekasy dah hatari
 
Dah hivi kwann watu wa hivi
Ndio inakuwaga kimoja na hatufanikiwe kuonana dah
 
Daaah hii story yangu nitakuja kuisumulia siku moja humu.nakumbuka the day nilivyopiga mguu kutoka tengeru Arusha mpaka melerani machimboni Alafu mfukoni sina Hata cent.alafu nimefika machimboni kule Hali ya kule iliniogopesha Yaani sikuingia Hata ndani migodini niliishia nje nikaamua nirudi tengeru hapo ubao unaniiuma ni balaa nakumbuka wakati nimefika mbuguni madukani hapo ndo narudi tengeru nilimuazima simu jamaa mmoja niweze kuongea na brother wangu anisaidie Hata elfu mbili niweze kupata chochote Sasa nikawa na mawenge kama jamaa atakubali kuniazima simu ule usiku kwa sababu nilikuwa nimechakaa appearance yangu ilikuwa ya kiizi izi Lakini jamaa aliniazima simu nikawa naongea na bro nikawa sijaamini Maana nilikuwa niko karibu yake alafu ona sijamini akaniambia ww Sogea tu mbali ongea na kama yako ukimaliza niletee simu nilifanya hivyo baada ya kumaliza nikamrudishia simu nikamshukuru sana nakumbuka jamaa alitoa jero lake akaniambia dg Kanywe soda nafikiri aliniona kwamba napitia kipindi kigumu baadaye nashukuru bro wangu alinitumia elfu nane maana aliniambia nitafute sehemu ya wakala kwa hiyo akanitumia huko baadaye baada ya kutoa hela nikarudi nimshukuru yule jamaa kwa alichonifanyia lakini sikumuona nikajirahumu kwa nini sikuomba Hata aniandikie namba yake kusema kweli nakumbuka fadhira za yule jamaa mpaka leo kiukweli alinifanyia makubwa naomba mungu amuongezee huko aliko.pia sita sababu fadhira za mama yangu wa Arusha mama manka wakati niko Arusha ulinilea kama mwanzo mimi mtoto wa kinyakyusa niliogopa kuendelea kuwa mzigo kwako mama yangu nakumbuka nilivyopendwa na Wanao waliniona kama Ndg Yao najua huko uliko unajiuliza kwa nini sijakutafuta mpaka Sasa Yaani tangia nirudi Mbeya sijawahi kumaliza kukufikiria mama yangu I remember the day nilivyokuambia mama Arusha nilikuwa sina ndg lakini nafurahi nimepata ndg Sasa katika mkoa huu.ulipenda unyenyekevu wangu upole wangu nafikiri kwa kipindi kile nilijiona na mama Sasa angalau ambaye Abakaliki hisia zangu hii ni baada ya miaka kama miwili mimi mtoto wa mama kumpoteza mama.nilishaweka ahadi mama yang ndani ya moyo wangu lazima ni taifa Tia Jambo kubwa familia yako haijalishi nini kitatokea anyway Sasa Hivi niko Mbeya wakuu ambako Ndo nyumbani kwetu nitakuja na mkasa wa maisha yangu kuanzia niko nyumbani mbeya mpaka nilipokuwa arusha nafikiri watu watajifunza mengi kupita mimi.Arusha ni Kati ya mkoa ambao utabaki na kumbukukumbu zangu daima ukiachana na Mbeya
 
Story nzuri but jitahidi uruke nafasi aya zionekane na vituo km mkato , nukta, funga na fungua semi
 
Nilikuwa nimefaulu form five nikapangiwa shule moja ya serikali mkoa fulani hivi, nimetoka kijijini,kusafiri toka mkoa wangu hadi huo wa shule ni masaa 12, sijawahi kwenda, unafika mkoani afu unapanda magari ya wilayani.

Mungu alinisaidia nikafika mkoani saa 12, nikataka kuunganisha magari ya kwenda wilaya hiyo shuleni, stand magari hakuna yote yameenda, nikaenda nje ya mji eneo la mwisho kabisa barabara ya huko wilayani ili nidake gari yeyote, nilikaa hadi saa mbili usiku sikupata gari yeyote. njia hiyo ni barabara ya vumbi (miaka hiyo).

Mama mmoja alikuwa kama miaka 55 au 60 hivi, aliniona akasema mwanangu nimekuona umesimama muda mrefu, twende ukalale kwangu asubuhi utapata gari. akanichukua, nadhani alikuwa mjane kwasababu sikukuta mwanaume pale, akaniandalia maji ya kuoga nikaoga, akaniandalia chakula nikala, akanionyesha sehemu ya kulala mojawapo ya vyumba vyake pale, I was so blind, hata angeamua kunifanyia ubaya wa kunipora ada (kwasababu ilikuwa mfukono) angeweza, angeamua kunifanyia ushirikina angeweza, angeamua kuninyonya damu au chochote, ila alifanya ukarimu kama anamfanyia mwanae kabisa. asubuhi akaniamsha, akanipa maji ya kuoga, akanipa chai, akanisindikiza hadi barabarani, nikapata gari nikaenda zangu. Mama huyo alikuwa hanijui, nimemaliza shule, nimepata kazi, nishajitegemea, kwenda ule mkoa specifically nikamwone, (after like 10 years), alishakufaga, na pale nyumbani kwake palishauzwa pamebadilika kabisa sio kama pale nililala siku ile. iliniumaaa, na inaniuma hadi leo. sijawahi kufanyiwa ukaribu kama ule na sitakuja kusahau. kuna wanadamu wengine hapa hapa duniani wanaweza kukukarimu wakati ule upo kwenye shida na wakagusa palepale ulipokuwa na uhitaji, ni kama malaika wametumwa na Mungu waje kukusaidia kabisa. sitakuja kusahau. Mama huyu ndiye aliyenipa mzigo, nikimkuta mtu yupo kwenye shida na nikajihakikishia kabisa kwamba haigizi na hana namna ila kusaidiwa, huwa sisiti kufanya hivyo, hadi imefika mahali mke wangu ananichunga mno manake anajua naweza kugawa pesa kwa kila mhitaji asipokuwa makini.
 
Hivi kwanini kila mtu aliyesaidiwa kwa ukarimu asimilia 100 akitaka kwenda kurudisha fadhila
Lazma kutatokea mazingira wasionane na muhusika

Pili mm naamini watu wazuri duniani bado wapo
 
Siwezi kusema ule ulikua ni msaada ila ila upendo alionionyesha yule dada mpaka leo natafakari bila majibu na bahati mbaya sina matarajio ya kukutana nae tena hata ningemwambia asante!

Mwaka 2006 Veta kihonda Morogoro, tulikua tumekaa wavulana kama nane, karibu wote walikua wachokozi , wahuni, na kila aina ya usumbufu wa vijana wa kiume.

Alipita dada mwanafunzi mwenzetu mbele yetu, moja wetu akamuta , yule dada akaja, alikua anakula pipi , wakimwambia tunaomba pipi yako, alijibu mpo wengi na pipi imebaki moja itakuwaje, mmoja wetu aka mwambia amchague mmoja wetu anayempenda ampe, yule dada alifunga macho akaja upande wangu akanipa mimi!

Ilinistaajibisha sana kwa vile mimi nilikua mtu nisie na swagga yoyote, mkimya na muoga sana, hata salamu kumsalimila mtu hususan wanawake nilikua mwoga!

Wakati wakiambiana na kuombana pipi mimi sikua nao kifikra kabisa, maana ninajijua sikua na mbele wala nyuma, nilikua nimekaa nao lakini sikua nimestahili kwa mwonekano na taswira yangu, nguo zangu na viatu nilikua duni sana japo ni uniform za shule lakini zilikua zimechakaa, sikua na sababu yoyote ya kuvutiwa na mtu kwa vyovyote.

Lakini dada watatu sijui aliona nini kwangu na kunipa thamani ile tena mbele ya watu wananicheka kila siku na kunibeza, sikuwahi hata siku moja kumsalimia dada wa watu lakini sijui ninini kilichomfanya akanithamini vile!

Wenzangu wale baada ya hilo wakamcheka eti amechagua huyo boya kwa vile hawezi kukusumba kwa lolote!

Hatukuwa na muda mrefu tuka maliza masomo, sikuwahi kumuona tena tokea hio 2006 , hata sikuwahi kujua ni mwenyeji wa wapi maana shule ile ilikua inachukua wanafunzi toka mikoa mingi.

Jina lake tu na taswira ya mwonekano wake ndio nimebaki nayo mpaka leo, alikua mweupe ambeye hasuki nywele, alikua anaitwa Mary.

Popote alipo asipungukiwe na lolote na Mungu ampe wepesi kati changamoto zote.
Upendo wa kweli hauangalii mwonekano wa mtu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom