Niliyoyakuta Keko

kunonu

Member
Jun 28, 2020
88
121
Kunonu Teknolojia walinituma nikampelekee mteja 'memory card' ya kamera. Nikiwa namsubiri mteja tuonane, macho yangu yakashuhudia ya kwenye 'muvi'. Mwanamke aliyembeba mtoto mdogo mgongoni huku kichwani kabeba ndoo angavu iliyojaa 'juisi za kandoro'. Akasimamishwa na mwanaume mmoja aliyeonakana ametoka 'lanchi'.

Huku akiongea na simu, mwanaume akatoa 'nyekundu' moja akampa yule mwanamke. Yule mdada akatua ndoo ampe 'juisi', lakini yule mwanaume alitikisa mkono ishara ya kutosheka na akaendelea na safari.

Yule mdada hakuamini kilichotokea, aligeuka kumwangalia jamaa zaidi ya mara mbili pasi macho kugongana. Alivuka barabara na kugeuka tena, jamaa aliendelea tu.

Nikajisemeza moyoni, ivi zile 'juisi za kandoro' hata zingeuzwa zote bado zisingefikia ile hela. Na yule mdada angetumia muda gani kumaliza huo mzigo? Na vipi kuhusu mtoto, na hili jua kali la jiji la Wazaramo?

Nikajiambia nikiwa mkubwa nataka niwe kama yule 'braza' wa Keko.

Simulizi hii imedhaminiwa na Kunonu Teknolojia , wauzaji wa memory cards, USB Flash Drives hard disks na SSDs.

Wasiliana nasi #0629831936 au #0765542197 tukuletee bidhaa yako popote Tanzania.
sadaka.jpg
 
Japokuwa umeichagiza hii habari kama kianzio ili watu washawishike kusoma tangazo lako la biashara,ni vizuri binadamu kusaidiana.

Inasemwa unapomsaidia mtu kama huyo wala hela utakayompa hataijengea nyumba au kununulia gari ila utakuwa umempunguzia maumivu na kumfariji wakati akisubiri mafanikio yake kesho na hii ni sadaka ambayo Mungu anaiona moja kwa moja,hata humu JF wapo watu wanafungua mada wakiwa ktk shida kama mtu una uwezo saidia tu 5K yako utakayompa haimsaidii zaidi ya kushibisha tumbo lake tu.

Wakati mwengine unakuta mlemavu wa macho anatembeza viberiti (nilimkuta K/koo) au mama mtu mzima anauza vitu kama limao au tangawizi (nilimkuta mmoja makutano ya Msimbazi &Twiga anakuwepo asubuhi) msaidie wala bidhaa yake usiichukue maana amejaribu kutokuomba akaona afanye kitu ili kuishi ukimsaidia umemfariji sana.
 
Back
Top Bottom