Niliwahi kusikia umeme wa chooni una nguvu, lakini hadi leo hakuna mwanasayansi hata mmoja aliyewahi kuvuna kinyesi tupate umeme

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,295
21,437
Tangu miaka ya zamani tuliaminishwa hivyo"

Kwamba karo la choo likiwa na kinyesi liwauwezo wa kuzalisha Megawatt za kutosha!

Sijui kwanini hadi Leo wanasayansi wapo kimya!

Yamkini tungekuwa na STIEGLERS ndogo ndogo kila mtaa!
 
Kwa kutumia Landfill gas, na sio hio tuliyokuwa tunaaminishana kuwa unadumbukiza batteries za gari zilizoungwa na waya, waya huo ndo unaunga ndani🤭
 
Kwa kutumia Landfill gas, na sio hio tuliyokuwa tunaaminishana kuwa unadumbukiza batteries za gari zilizoungwa na waya, waya huo ndo unaunga ndani🤭
Fafanua kidogo mkuu
 
Tangu miaka ya zamani tuliaminishwa hivyo"

Kwamba karo la choo likiwa na kinyesi liwauwezo wa kuzalisha Megawatt za kutosha!

Sijui kwanini hadi Leo wanasayansi wapo kimya!

Yamkini tungekuwa na STIEGLERS ndogo ndogo kila mtaa!
Kwani hujawahi kusikia Muhimbili wamegundua dawa ya kisukari lakini hadi leo hawajamtibu mgonjwa hata mmoja kwa dawa hiyo
 
Unless unasemea tanzania ila kwa wenzetu mbona kawaida kwa maeneo ya remote areas. Pinda mwenyewe shambani kwake anatumia umeme wa kinyesi cha ng'ombe
Tofautisha Bio gas inayotoka kwenye kinyes cha ng'ombe, HAPA tunazungumzia kinyes cha binadam
 
kwa lugha rahisi fikiria mfumo wa dynamo ya baiskeli ambayo inawasha taa kwa kuzungushwa na tairi ya baiskeli. Ili umeme upatikane ni lazima chombo kizungushwe kwa namna yoyote au kwa kutumia tairi, mkono, au maji yaendayo kasi au upepo au mvuke uendao kasi sana boilers huchemsha maji. maji yakichemka sana hutoa mvuke ambao unapitishwa ktk mambomba maalumu kuelekezwa kuliko dymo ndogo au kubwa kulingana na matumizi ya umeme.

Ukiacha umeme wa maji kama wa mtera au kidatu, kuna umeme wa upepo. na kuna umeme wa maji kutoa mvuke nao unapatikana kutoka vyanzo vya Makaa ya mawe. Nyuklia. Vinyesi. Uchafu wa katani vyote hutumia nishati ambayo itachemsha kwanza maji na baadae maji kutoa mvuke na baadae mvuke kupitia mabomba maalum kuzungusha motor au mtambo wa kufua umeme. Zaidi ya hapo kuna umeme wa radi nk
 
Tofautisha Bio gas inayotoka kwenye kinyes cha ng'ombe, HAPA tunazungumzia kinyes cha binadam
Hata kinyesi cha binadamu kinazalisha biomethane ambayo ni RNG inatumiaka kuendesha generator za kuzalisha umeme. Kitu amabzo inabidi ujue hata nuclear reactors zinazotumia uranium, siyo kwamba uranium inazalisha umeme, bali inazalisha joto linalotumiaka kutengeneza mvuke ambao utazungusha turbines ilikuzungusha generator izalishe umeme, kama ilivyo kwenye hydroelectric plants.

Hata kinyesi kinazilisha biogas ambayo inatumika kuendesha generators.
 
Hizi ni consipiracy tuu. umeme wa mavi ni just betri za redio unazitumbukiza chooni lakin hazigusi kinyesi. so kutokana na joto battery zinakua active muda wote hadi zife.

Ni hicho tuu

Dah, nilikuwa nadumbukiza betri na kuzamisha kabisa chooni halafu nyaya nakonekti ndani ila hakuna umeme wala nn. Kumbe nilikosea!
 
Kwa kutumia Landfill gas, na sio hio tuliyokuwa tunaaminishana kuwa unadumbukiza batteries za gari zilizoungwa na waya, waya huo ndo unaunga ndani
Hii mimi nilijaribugi kabisa..sema kwa kutumia bettery za redio..lakini sikupata result
 
Dah, nilikuwa nadumbukiza betri na kuzamisha kabisa chooni halafu nyaya nakonekti ndani ila hakuna umeme wala nn. Kumbe nilikosea!
Sasa kwani wewe si unakili...ya kufungua Kvant TU.. hata ya kuchamba mavi HUNA
 
Hizi ni consipiracy tuu. umeme wa mavi ni just betri za redio unazitumbukiza chooni lakin hazigusi kinyesi. so kutokana na joto battery zinakua active muda wote hadi zife.

Ni hicho tuu
Nilisikiaga hizo hadithi kutoka kwa wajuba enzi hizo nipo shule ya msingi "ukiunganisha nyaya na bulb unaweza kuwasha taa, tena unaweza kuunguza hata nyumba inategemea na vyakula wanavyokula" wakanipa na ushuhuda kabisa. Nyumba yetu ilikua haina umeme nikajiambia leo naenda kuwafanyia surprise nyumbani akirudi kutoka shamba wakute umeme, na kutokana na misosi tunayogonga pale nyumbani hatuwezi kutoa mzigo unaoweza kuunguza nyumba, so I was okay kufanya yangu.

Nikapita kwa mwanangu mmoja akanipa waya na kile kiholder cha bulb na switch, halafu tukaenda kuiba bulb nyumba moja hivi. Baada ya kupata vifaa Bwana Nikola Tesla nikaingia mzigoni nikaunganisha kila kitu baada ya kumaliza nikaenda chooni ila changamoto choo kipo mita 200 kutoka nyumbani lakini sio kesi kama ikikubali si sishindwi kung'oa wiring ya nyumba ya mtu na kupata wire kama nilivyopata bulb tu. Nikatumbukiza waya kwenye shimo la choo kila nikiwasha switch kitu hola.

Ikabidi nisitishe zoezi nimfuate technician mwenzangu anipe mawazo tunafanya nini? Jamaa akaniambia umeme ulikua mwingi bulb iliungua tena nina bahati ningepigwa shoti, inabidi tupate bulb nyingine. Jamaa akachomoa kwao tukarudi site engineer akaingia mzigoni maana nilishakua na hofu ya kupigwa shoti ngoja nimuache mtaalamu afanye mwenyewe. Ila issue ikabaki vile vile taa haikuwaka. Tukasitisha zoezi huku tukiamini bulbs zinaungua. Ila kurudi kwao kurudisha bulb ikawaka ndio nikajua nilikua napigwa kamba tu.

Ndoto yangu ya kufurahisha wanandugu na umeme wa kinyesi ikaishia pale.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom