Nilivyo Nusurika Kuliwa Tigo Kisa Mke Wa MTU...

Forest Hill

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
2,123
4,209
Habari zenu waungwana,bila Shaka mpo salama Poleni Na Heka Heka za sikukuu...

Kuna story nataka kushare nanyi,ni tukio la kweli lilinitokea tarehe 28/12/2015.....Mkasa unaanza nipo Ubongo ndani ya Bus la Abood naenda Morogoro kwenye Mambo ya Utafutaji,,.Seat kama ya 3 Mbele yangu kakaa binti mrembo Sana,, black beaut,ana Short Hair...Muonekano wake,nywele zake,ukanifanya Kidume nijiongeze nikakae nae Seat Moja..kweli nikafanikiwa,kufika pale nikaita Gazeti Mwananchi Jumamosi,nimsome Gaston Nunduma,,nikamuagizia binti Ijumaa Lol,then Nikachombeza "bila Shaka nataka kujua Nini kimemtokea Nuh Mziwanda' Omg binti kachangamka story After story..Tukazoena,Tunacheka,Jokin,Playing and stuffs,.kidoleni Kavaa Pete ya Dhaabu Kama ya ndoa,nikamuuliza Vipi???Umeolewa???Akasema "Hapana,Yupo Morogoro anakaaa Misufini Kwa Dada yake,anasoma Sua..nikamwambia Nimvue Pete then Nimvalishe Tena,akakataa..Akasema Pete Huwa Havuagi,nikiangalia ipo Pale kwenye Kidoleni Mpaka imeweka Alama,,nikaona it's Okay,uroho Na tamaa ukanifanya niwe kipofu wa akili...Nikaimba Ngonjera Mle,mtoto akaelewa Tuka exchange Numbers,Kufika Stand ya Msamvu Kidume Nikakodi Taxi,.me Nilikua Naenda Forest Hill,Mtaa wa Sinai,binti anaenda Misufini,tukampa lift Hadi Bush Bar Njia ya kwenda Sua,then Nikasepa...

MAWASILIANO.

Utata ukaja hapa,ikifika mida ya saa Tatu Usiku,Simu yake Haipatikani Anasema Dada yake Hataki awe anatumia Simu Usiku.. sometimes hata Mchana Simu hapokei,texts hajibu..Moro Nilikua nakaa Two weeks..,nikakutana Nae Town mara mbili,,Nashera Hotel Mara Moja..Tukapanga Siku ya Kwenda Kufanya Matusi...Nakumbuka ilikua jumamosi Ya mwisho me kua Morogoro,,Tukapanga Hadi Eneo la Kukutana,,Kumbe Yule mwanamke Kaolewa and Mume wake Kastukia Mchezo,Kampanga kua kila ninachomwambia,akubali...waweke Tego mwisho wa siku Wanile 0712**....Nilipanga nikutane nae saa Sita Mchana,,,Mwanamke Kafika Mapema,nje kuna Mume wake na Masela..wanasubiri niingie,,wanifanyie roho mbaya..Muda huo Me Nipo Mzumbe kuna jamaa zangu nafanya nao Biashara,nikawa Nachelewa hadi saa Nane,,sijafika Town...waka Panick wakajua nimestukia Mchezo..Ghafla Simu ikaita,kwenye Screen number ya Yule mwanamke,,nikawaaga wale Marafiki nikawaambia "Oi wazee,shemeji yenu ananisubiri Town Ngoja niwahi,,,Napokea Simu najua naongea na bebe,,upande wa pili Sauti ya Kidume yenye Jazba,,besi,Hasira Anafoka "wewe Mseng** Bahati yako P*m* zako,leo show ungeiona,ukome kufatilia wake za Watu,,Nitaku**** nikuue nikaozee Jela... Jamaa kaongea mengi,,me sijajibu Mwisho Nikamwambia Brother,wrong Number...Tangu pale Nikafuta Ile Number..,Nikawaambia Makini Sana,Nikigundua Mwanamke Kaolewa,Hata Salamu nakua Muoga Kumpa.....MWISHOOOOO
 
Bado hujawa mtunzi mzuri.story yako inaonekana kabisa ni ammature. Imekaa kitoto toto sana. Ukitaka kutunga story kama hii unapaswa utulie sana na uwe na akili.lakini ukitumia akili za kuvukia barabara tu ....aaargh.sisi wenye uelewa tunajua.
 
Hajui hata kutunga kuendana na uhalisia. Maana yake jamaa ni kilaza. Nani sasa hivi anajua kinachoendelea kwenye magazeti tena mtoto wa kike?
Mastory ya kizaman unatuketea leo watu wako busy na smartphone ukamnunulie gazet la ijumaa??
 
Ahahahaha, mkuu Nouma sana mke wa mtu ogopa sema wengine wanajilaisisha sana sijui inakuwaje
 
Back
Top Bottom