Nilitiwa aibu ugenini sitasahau

Mdigokhan

JF-Expert Member
May 2, 2022
845
1,926
Bwana miaka ya nyuma Nikiwa zangu Tanga nishamaliza masomo afu nishafeli sielewi elewi kila kazi ninayofanya inagoma Nikaona ni vyema niongee na mama angu Ili nije dar kutafuta maisha.

Mama akaona nikija Dar ovyo ovyo nitakuwa TEJA ivo alimpigia simu kaka yake ambae mimi ni anko wangu na akamueleza vyote kuhusu mimi na mjomba alikubali nije Dar.

Kwa mala ya kwanza natimba dar Nilipokelewa ubungo na huyo mjomba wangu. Huyu mjomba wangu sinaga mazoea nae sana mana ni kauzu sana hana uchangamfu kabisa.

Alinichukua na gari yake mpk kwake Kawee Ilikuwa mida ya saa 9 jioni Ndio tunaingia kwake.

Ana nyumba nzuri ila ina ndugu wengi wa mke Ivo sikuwa na mtu ninaemjua zaidi ya anko tu mana hata mkewe sijawahi muonaga Before Wala watoto wake (Ni ile familia haitembelei watu) Basi Nikakalibishwa ile kikawaida sana yani kama kimtu flani ivi sijaulizwa za huko wala za huku yani kama vile Nilitumwa dukani ndio nimerudi wala Sijaulizwa umekula wala nini But nilioneshwa chumba changu nikaweka begi langu nikachili kungoja chakula cha usiku japo njaa ilikuwa inauma sana.

Basi buana usiku ukafika Nikaitwa Chakula Tena waliniita BONGE BONGE yani hata jina langu sijaitwa 😂 nikajua mjomba hajawaambia labda, Basi buana Tukajumuika Tukawa tunakula Ila macho ya watu wote Ni kwangu japo wananiangalia kwa kuibaiba.

Anko wangu hanaga story wala nini yani ni mtu Serious sana Basi aliposhiba chakula akaniambia ‘BONGE kuhusu kazi tutaongea kesho nikitoka kazini’
Then Akaenda zake chumbani kulala.

Kwanza nilimaind why aniite Bonge wakati anajua jina langu Inaonekana hata wale mule ndani alinitambulisha ivo kuwa mi ni bonge Daah ni sawa mi bonge ila naitwa furani 😂
Basi Pale sehemu ya kula Nikabaki na mke wake na watoto wake wa3 na ndugu wa mke wa4 na mfanyakazi (mfanyakazi nilimjua baada ya kuona ndio anatumwa tumwa huku akifokewa)

Basi Niliposhiba nikaaga naenda kulala,Mke wa anko akaitikia kwa kichwa. Nikaingia zangu chumbani nikiwazaa mmh ntatoboa hapa Ila nikasema Mi mwanaume ntakazaa.

Nikata kufunga mlango na Funguo ili nilale ila funguo hakuna ivo nilirudishia tu nikalala zangu fofofo Mana nilikuwa na uchovu

Palipokucha Asubuhi niliamka kitandani Kumelowa Sana Nikinusa ni mikojo afu mi nikijichek mkavuuu sijakojoa na nimelala peke yangu 😂😂 kojo kojo kweli aiseee Nilikaa mule ndani mpk saa 4 asubuhi Nikiwaza imekuaje.

Nikiwa na mawazo nikagongewa mlango Nikiitwa chai Na dada wa kazi basi nikanyanyuka nikaenda Oga kisha Nikaenda mezani kunywa chai ila huku nina mawazo kibao.

Nikiwa mezani nakunywa chai Gafla mtoto wa anko akamwita mama ake kwanguvu kule chumbani kwangu 😂Aisee hii sitasahau kamwe…

Mchana mzima Ni story mule ndani kuwa nimekojoa nimekojoa Ila kila nikiwaeleza sio mimi hawataki kuamini mana nililala peke angu Dah nilijisikia vibaya sana.

Nilishinda kwa unyonge japo nilihisi wao ndio walifanya ule ujinga but Sina pakuwasemezea…Ilipofika Usiku anko alirudi kutoka kazini tukasalimiana Akaingia chumbani kwake.

Muda wa msosi wa usiku tukala Na kila mtu alitawanyika Kulala…Sasa Nikiwa nawaza nalalaje huku chumbani na godoro linanuka mkojo Afu nigeuze godoro pia nikijilaumu kwanini sikulitoa juani, Mlango ukafunguliwa akaingia anko wangu Akanimbia Niweke vitu vyangu vyote kwenye begi kisha nimfate.

Nikapaki kila kitu changu kwenye begi nikidhani naamishwa chumba basi nikamfata akawa anaelekea getini Kufika getini akaniambia..

‘Fungua hilo Geti afu Funga’

Nikafanya kama alivosema Nikafungua afu nikafunga Akaniambia tena kwa ukali…

‘Fungua hilo geti afu funga we ukiwa nje ya Geti’

Basi Nikafungua Lile geti Then nikatoka njee nikafunga ‘Puuuuu’ sekunde 5 nikasikia komea Kwichi kwichii Nikawa nishafukuzwa ivo 😂😂

Nikatembea huku nalia aisee nilishindwa jizuia Nikawa naenda Nisipopajua mana Dar mgeni na Kawe mgeni…Tembea tembea yangu usiku ule Nikaja kudakwa na wanajeshi Pale Rugalo Mana nilipita sehemu sio na ni usiku….

Sisahau aisee yaani kwa anko nilikaa siku moja tu.

#Mwisho…
 
Walikufukuza kijanja pole
 
Kama uongo, kumsema hivyo anko wako ili iweje, umaharufu wa humu hauna faida Wala Nini.
 
Back
Top Bottom