Nilitembea naye kweli, akapata mimba... Lakini natatizwa na hili

Mbwa dume

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
5,539
9,081
Tukiwa tumebakiza siku au masaa kadhaa kuuaga mwaka 2022 nakuja mbele yenu na hiki kisa:

Kuna kabinti flani kalikuwa kanasoma chuo flani hapa Dom nilikuwaga na mahusiano nako miaka ya nyuma badae tukaja kuachana kama mnavyojua vidada vya chuo huwa vina mambo mengi.

Sasa mwanzoni mwa mwaka huu akaanza kurudisha mawasiliano na mimi tukawa tunachat mara moja moja akadai huwa ananimiss sana anatamani japo tupange siku tuonane tupeane utamu.

Nakumbuka ilikuwa tarehe 6 mwezi wa nne nilipata safari ya kwenda mkoa flani kucheck kama naweza kuwekeza biashara yangu ya majeneza huko, nikiwa huko nikawasiliana na huyu binti nikamjuza kwamba ntakuwepo hapo kwa siku kama tatu(kipindi hicho alikuwa anaishi mkoa huo baada ya kumaliza chuo)

Nilipomjuza kwamba niko maeneo hayo alifurahi sana akaomba kuja kuniona nikamkubalia hivyo akapanda basi kutoka eneo alipokuwa mpaka kufika mjini nilipofikia mimi ni umbali wa masaa matano hivi.

Ili kufupisha story alikuja tukapiga story kwa jinsi ambavyo tulikuwa na muda mrefu hatujaonana kila mmoja kammiss mwenzake tulijikuta room tunapiga show na tulilala mpaka kesho yake ambayo nakumbuka ilikuwa Karume day tarehe 7 April.

Kulipokucha ndo ananiambia eti tumesex siku mbaya ambapo anadai aliingia period tarehe 24 March hivyo kufikia hiyo tarehe tuliyofanya mapenzi tarehe 6 kuamkia tarehe 7 April ilikuwa siku ya 14 kwenye mzunguko wake hivyo anahofia kuwa kanasa mimba!

Nikamuuliza kwa nini hakusema kabla akasema eti kutokana na alivyokuwa kanimiss halafu alipofika tulikunywa kidogo hivyo anadai alijisahau amekuja kustuka asubuhi kwamba alikuwa tarehe mbaya!

Tuliagana nikaendelea na mishe zangu then nikarudi Dom tukawa tunawasiliana mara moja moja baada ya siku kadhaa akanambia amepima ana mimba na ana uhakika ni yangu!

Sasa mnamo jana tarehe 27 December huyu binti kanitaarifu kajifungua mtoto wa kike.

Nimekaa nikawaza kabla ya kuchukua maamuzi yoyote nifanye utafiti kwanza ili nisije kuwa napigwa na kitu kizito!
Najua humu kuna watu wenye uelewa tofauti hata wataalamu wa masuala ya uzazi pia wapo(japo wale wazee wa michambo pia wapo)

Naomba msaada wa kitaalamu kwa wenye uelewa wa haya mambo:

Inawezekana nisex na mwanamke siku ya 14 ya mzunguko wake ambao una siku 28 then aje kujifungua mtoto wa kike?

NB: Ikumbukwe kwamba alianza period tarehe 24 March na nikafanya naye mapenzi usiku wa tarehe 6 April na amejifungua tarehe 27 December mtoto wa kike!
 
Kwa haraka haraka kwa miezi ni kajifungua kabla ya muda sema ni siku kama 3 au 4 zilikuwa bado. Ila hilo sio swala.

Tatizo linakuja kuwa baada ya kukinasa akawaza haraka wa kumwangushia jumba bovu na akiamini utakubali ni wewe so akarejesha mawasiliano na wewe na uzinifu wako ukaona mbunye imejileta yenyewe so ukumbushie enzi zenu 😆😆😆 bila kuwaza.

Pili anakwambia mlikunywa akasahau wakati huo alishakwambia amekumiss mkumbushie enzi.
Rudia kusoma hiyo thread yako kisha jiamulie

Na wewe hata kustuka. Hapa "Kulipokucha ndo ananiambia eti tumesex siku mbaya ambapo anadai aliingia period tarehe 24 March hivyo kufikia hiyo tarehe tuliyofanya mapenzi tarehe 6 kuamkia tarehe 7 April ilikuwa siku ya 14 kwenye mzunguko wake hivyo anahofia kuwa kanasa mimba!"

Hamna
 
Toka mkutane hadi mtoto kuzaliwa ni miezi mingapi?
Kama tarehe ya mwisho kuingia hedhi ilikua 24 March huo ujauzito una miezi tisa (week 39 na siku 6) so ni sawa kama alikutana nae, makadirio ya tarehe ya kujifungua 15-29 december. Issue ya tarehe 14 kuwa ni mtoto wa kiume izo ni probability tuu inaweza kua wa kike pia.

Kwa hayo maelekezo kama hakua kakutana na mtu mwingine huyo ni mwanao ila sasa hawa viumbe hawaaminiki fanya kama unaweza kapime DNA ujiridhishe. Asante
 
Sasa kufuatilia kibali inahitaji fedha za kigeni!?? Hiyo sio shida sana kwako sababu hauna ndoa naye, ww unaenda unaeleza maelezo yako watakuelewa!

Wanazingua sanasana wanandoa ili kuepusha magomvi!
Nashukuru kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom