Nilitaka kumuua mke na mtoto wa 'my best friend' kwa risasi!

Poleni kwa kunisubiri!

Mshikaji unatuweka sana! Vipi mkuu, au ndio ethics za kijeda? Unatujasirisha sasa ngoja nikuitie koma koma yako hata kama umeshindwa namna ya kumalizia unasema tu! Oyaaaaaaaaa, Mwanamalundi njoo huku CHAI CHUNGU anatuyeyusha! Ahahahahahaaaaaa!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
nimekaa kama guest weee mpaka nimechoka kusubiri..CHAI CHUNGU kiboko duu.
hebu rudi banaa wengine tusije otesha vibarua majani bure
 
28:Nilimkodolea my best jicho la kumuaga maana kulikua na sekunde zisizozidi 50 ili niwe nimeshamsafirisha ahera huku nikijipa moyo mgumu wa kubaki na siri hiyo peke yangu mpaka siku ya mwisho wa maisha yangu ili nikaijibu kwa M/mungu.

Akiwa hajui ili wala lile mwanaume nilichomoa machine kutoka mfukoni kwangu kisha kwa kasi ya ajabu kilitokea kitu ambacho sikukitegemea kukiona kabisaaa...................
 
28:Nilimkodolea my best jicho la kumuaga maana kulikua na sekunde zisizozidi 50 ili niwe nimeshamsafirisha ahera huku nikijipa moyo mgumu wa kubaki na siri hiyo peke yangu mpaka siku ya mwisho wa maisha yangu ili nikaijibu kwa M/mungu.

Akiwa hajui ili wala lile mwanaume nilichomoa machine kutoka mfukoni kwangu kisha kwa kasi ya ajabu kilitokea kitu ambacho sikukitegemea kukiona kabisaaa...................

aiseee we kiboko nlinuna mpaka nimecheka mwenyewe
 
Mimi ni muajiriwa wa JWTZ Kikosi cha 202 Faru Tabora. Nilipokutana na binti mrembo wa ki-singida nikampenda na kumueleza azima yangu kwamba namuitaji kifamilia na akanielewa. Na tukawa ktk mahusiano.

Lakini sababu alikua mwanachuo hatukuwa na haraka ya ndoa mpaka atakapo maliza chuo mwaka 1 baadae. Nilimuuliza kama ana boy friend maana nimekuta mlango umeshafunguliwa so niliitaji kujua hatima ya huyo aliyefungua mlango. Akasema sii mkweli na alishaachana nae kitambo. Nikasema ok, fine. Nilitaka kumjua mwenyeji wake Tabora na akaniambia amekuja likizo kwa sister wake pande za chemchem.

Nilimuomba anikaribishe kwao ili nipafahamu hakuwa na kikwazo juu ya hilo. Baada ya kufahamiana vizuri kiasi tuliendelea kula tunda, siku1 tukiwa chumbani kwangu huku tukiangalia albam alishangaa kuiona picha ya mtu fulani niliyepiga nae picha tukiwa depo...aliniuliza kuhusu huyo mtu na nikamwambia yes namfahamu vema ni my friend wa kitambo sana. Nilimuonyesha na picha nyingine za utotoni.

Cha ajabu majina na kazi yalikua tofauti na alilonitajia yeye alisema anayemjua anaitwa MASIGITI na ni TICHA WA SEC pale SINGIDA, na mimi ninayemjua ni John Manyama na ni askari wa JWTZ NGERENGERE MOROGORO. So tuliamua kupuuza na kuamini kwamba duniani ni 2x2...... binti alikua akienda chuo SINGIDA na alikua akija Tabora mara kwa mara.......siku 1 niliamua kumtafuta my friend Manyama ili nimpe taarifa hizi,lakini kwa bahati mbaya mawasiliano yalikua magumu sana.Zilipita siku,wiki,miezi mara binti akaniambia yu mjamzito.Nilifurahi sana na nikapanga safari ya kijijini kwetu ili kuwajulisha juu ya mimi kuoa mtoto wa kinyiramba.Kwa mila za kikwetu nilijua kabisa kwamba itakua ngumu wazazi kunikubalia.Lakini nikapiga moyo konde nikaelekea kwa wazazi wangu MUSOMA-MARA.

Wakuu ngojeni kidogo hapo hapo nakuja kuendelea na story hii yenye majonzi na huzuni mkubwa.....................

TUENDELEENI SASA:
Nilifika kijijini kwetu majira ya saa 4 usiku,wazazi wangu walifurahi sana kuniona na akachinjwa mbuzi usiku huo huo ili nitengenezewe ili kitu yetu inaitwa "KICHURI" baada ya kula nikenda chumbani kwangu kupumzika, asubuhi na mapema nilikata shauri kwenda nyumbani kwao my best wangu tuliyepoteza nae mawasiliano ili nijue ni vipi ntampata? Maana hatukua na mawasiliano tangu tulipopangiwa vituo vya kazi. Cha ajabu baada ya kufika kwao nikaambiwa kwamba walikuwa wanategemea labda mimi ntakua na taarifa nae maana inasemekana kwamba alitoroka jeshi na anatafutwa maana alitoroka na baadhi ya vifaa vya jeshi.

Taarifa hii ilinikumbusha tukio 1 pale kambini kwetu Tabora nilipoitwa kuhojiwa kuhusu inshu fulani fulani hivi ambayo huwa ni upelelezi wa kijeshi,lakini walibaini kwamba hata mimi sijui kitu.Walitegemea wangepata taarifa zake kupitia kwangu maana we was big friend kiukweli,nikawaambia sijui chochote kabisaaaa kuhusu John,i will be back again........

Niliporudi nyumbani niliwaeleza story nzima kuhusu safari yangu na wakanikubalia ombi langu maana tayari binti alikua tayari ni mjamzito.

Tulipanga baadhi ya mambo na nilipewa kazi ya kufatilia kujua wataitaji mahari(ng'ombe)kiasi gani.Becouse nilienda na picha basi ilifanyika tathimi kupitia picha kwamba tuandae ng'ombe 25-30.

Nilifurahi sana maana niliona ni jinsi gani wazazi wanavyonipenda.

Baada ya maongezi hayo walinigusia swala la my friend aliyetoroka jeshi. Waliniomba pia nisaidie kutoa taarifa au kumtafuta na nimuombe ili arudi jeshini maana ni aibu sana kutoroka jeshini na sasa wazazi wake wanasemwa vibaya kijijini hapa kwa kutomlea mtoto wao ktk ujasiri mpaka aona kazi ni ngumu jeshini mpaka katoroka....


NOTE:
WAKUU STORY HII INAENDELEA...
Hayatuhusu. This is your private business.
 
There are currently 271 users browsing this thread. (64 members and 207 guests)..... By the way hii story imeisha au bado anasimuliaaa... Mmh.. subira ya vuta heri ngoja nisubiri waiunganishe maaana utamu unakatika katika sana lol
 
Jaman wewe Mjeda, CHAI CHUNGU sijui Shingongo OR whatever your name is. Hebu malizia hii Isidingo sio tuendelee na mambo mengine. Yaani the one thread I read page after page an bado haijaisha tu! Mzizi Mkavu, please tag me akirudi maana hapa leo nina dalili za kutopika chakula cha mchana
 
Last edited by a moderator:
nimekuja kuchungulia kama mjeda tayari umerudi...maana daaahh hii super glue yako ni hatari inagandisha mbaya.
 
There are currently 299 users browsing this thread. (69 members and 230 guests)
 
Mjeda kachemsha mi nawaambia, hii hadithi iliishia mahali kaporwa demu kwisha. Sasa anatafuta namna ya kuimaliza kininja aonekane swazniga

Nyie mfuatilieni tu mpoteze muda na bando zenu
 
Back
Top Bottom