Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Watanzania wengi hawaelewi kwamba suala la kutekeleza miradi mikubwa nchini kwa kutumia fedha yetu ya ndani sio suala la kujivunia wala kujisifia hata kidogo. limetuletea maumivu makali katika karibu kila sehemu ya uchumi, hasa wakati wa Magufuli.
Miradi ya Magufuli aliyojivunia kutumia fedha za ndani ni kutia ndani ununuzi ndege, Reli ya SGR, Umeme wa Stiegler, daraja la baharini, Uwanja wa Chato, kuhamia Dodoma, nk.
Tanzania ni nchi masikini, sasa jiulize ikiwa fedha za miradi mikubwa kama hii sehemu yake kubwa ni fedha za ndani, fedha hizo zitatoka wapi? Katika nchi zote ambazo hazina vyanzo vikubwa vya fedha kama mafuta, miradi mikubwa kama hii hutekelezwa kwa fedha za mikopo ya nje na ndani.
Ili kupata fedha za ndani kwa wingi, Magufuli alifanya yafuatayo hapa chini, hatua ambazo zilituumiza sana. Ni kweli kuna mambo yanayotuumiza Samia ameyarithi toka kwa Magufuli, lakini si kwa kiwango kile cha wakati wa Magufuli.
Hivyo basi, Watanzania tunapaswa kuamka na kutambua kwamba, unapokopa leo, ukalipa baadae, unalipa wakati uchumi wako umekua kutokana na mkopo uliochukua, na maumivu ya kurejesha mkopo taratibu yanakuwa si makubwa ukilinganisha na kama ungewakamua wananchi fedha za ndani.
Kwa hiyo si vibaya kwa Samia kukopa ili kutekeleza miradi mikubwa kwa manufaa ya maendeleo ya taifa. Kama kuna lawama tunapaswa kumtupia raisi Samia ni pale atakapokuwa akikopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) na sio matumizi ya miradi yenye kuinua uchumi (capital expenditure).

- Wananchi na biashara zao kubanwa kodi kwa kila namna, kiasi kwamba hata biashara nyingine kufa kutokana na mzigo wa kodi
- Kutafuta vyanzo visivyo rasmi vya fedha kama vitambulisho vya wamamchinga ili kuongeza pato la serikali
- Kuanzisha kodi ya miamala ya simu kama Mpesa na vifurushi
- Kuanzisha kodi za kuchukua fedha ATM za benki
- Kutoa agizo kwa polisi kwamba wafanye kila namna kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa njia ya faini za barabarani
- Kubana nyongeza za mishahara ya wafanyakazi serikalini na maruurupu mengine ya wafanya kazi ili fedha ziende kwenye kutekeleza miradi mikubwa
- Kuondoa sherehe za kitaifa hata za matukio muhimu katika historia ya nchi
- Kupunguza kwa kiasi kikubwa bajeti za maendeleo ya serikali za mitaa - hii ni kutia ndani bajeti za miradi midogo midogo katika miji na majiji kiasi kwamba kunakuwa na athari mbaya ya mzunguko wa fedha na kila mtu anaanza kulia hali mbaya
- Kubana mikopo ya elimu ya juu ya wanafunzi, kwa mfano kusema wale waliosoma shule fulani hawastahili mikopo
- Kubana misaada ya Watanzania walioathirika na majanga kama matetemeko na kupunguza bajeti ya majanga ya kitaifa na hata kuwaambia wananchi wakipatwa na majanga watajijua
- Kutopunguza bei ya mafuta hata pale ambapo bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka kwa kiwango kikubwa ili sehemu kubwa ya faida katika biashara ya mafuta ya magari ilirudi serikalini
- Kubana safari za kikazi za wafanyakazi kwa kisingizio cha kubaki kazini ili kuwajibika
- Kubambikia kesi za uhujumu uchumi wafanya biashara wakubwa na kuwaambia kwamba wakitaka wasifungwe basi inabidi watoe malipo ya "makubaliano" ambapo ni kama kusema waihonge serikali
- Kunyang'anga mamlaka ya Bunge kupanga matumizi ya fedha za serikali na kuiweka chini ya uamuzi wa raisi
- Kupandisha ushuru wa bidhaa zinazoagizwa na wananchi toka nje kama magari kwa kisingizio cha "price uplift" ili fedha zaidi ziingie serikalini
- Nk, nk, nk