GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 57,115
- 110,509
Nilisisitiza mno kama siyo sana kuwa Kocha Mpya Simba SC Roberto Olivieira akitua Simba SC aje na Watu wake anaowaamini na kamwe asiendelee na Hawa akina Mgunda, Matola na Meneja Rweymamu aliowakuta GENTAMYCINE nilimaanisha na kuna Hatari niliiona na leo imejidhihiri.
Nawaombeni rejeeni marejeo ya Picha za Azam Tv wakati Mbeya City wamesawazisha Goli la Kwanza na lile la Pili kisha kwa Umakini kabisa tizameni Body Language ya Kocha Msaidizi Mgunda na Meneja Rweymamu kisha mtanielewa vyema.
Kocha Msaidizi Juma Mgunda alikuwa anajifanya Kuumia Magoli kurejea ( Kusawazishwa ) huku anajificha Mdomo na anatizamana na Meneja Rweymamu na baadhi ya Watu wa Benchi la Ufundi na Kumcheka Kimoyomoyo Kocha Mkuu Roberto Olivieira kitu ambacho Kwangu ni very Unprofessional na kimenilazimisha nianze Kumdharau Kocha Msaidizi Mgunda.
Na ili Kuzuga / Kutuzuga kila Simba SC ilipokuwa ikipata Magoli yake Kocha Msaidizi Mgunda Kinafiki kabisa alikuwa anajifanya anaamka na Kushangilia kwa Nguvu ( Kihisia ) huku akikongeana Mikono na Kocha Mkuu Olivieira.
Uongozi wa Simba SC mmefanya Kosa Kubwa sana Kumleta Fundi na Mtaalam Roberto Olivieira kama Kocha Mkuu na kumuachia hawa Waswahili na Wapika Majungu Wenzetu akina Kocha Msaidizi Mgunda na Meneja Rweymamu.
Ile Shangilia yake ya Kihisia Kali Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Olivieira baada ya Mchezaji Pape Ousmane Sakho Kufunga Goli zuri la Tatu ilikuwa na maana Kubwa na kuna Jibu alikuwa akilitoa Kwetu Mashabki na hasa kwa Benchi lake la Ufundi alilonalo ambalo huenda akawa ameshalisoma na kuhisi kuwa amezungwa na Wanafiki wanaovalia Ngozi ya Kondoo huku wakijifanya Wanamchekea na Kumpenda wakati kumbe Wanafurahia Kufeli Kwake Kimbinu (kutokana na Ugeni wake) na Wanamchukia kutokana na Uzungu wake wakiamini kuwa kaja Kuwaharibia na hawatofaidika tena na Simba SC.