Nilipenda nisipopendwa

Apr 7, 2012
32
5
wana jf wenzangu naombeni ushauri nilimpenda kijana ambaye hakunipenda, alinipotezea muda wangu na kunifanya shuleni nisifanye vizuri. kwa kifupi alinitesa sana alikuwa akiongea na mpenzi wake mbele yangu anamkiss mbele yangu mimi ananiambia shiiip! nimeamua kuachana nae mungu amenijaalia nimempata mwingine bahati mbaya anajuana nae hivyo ananiharibia kwa mpenzi wangu mpya,anamforwadia msg za awali za mapenzi nilizokuwa nikimtumia yeye anasema mm bado ninamtaka sasa mpenzi wangu huyu mpya ananionesha. sasa huyu wa zamani nimfanyeje? vitendo vyake vimenichosha
 
Pole sana Jasmin kwa hayo yaliyokukuta. Ni jambo ambalo ningependa kukushauri ni kujaribu kuzungumza naye kumueleza ukweli na ikibidi kuwa mkali maana wanaume wengine wengine wana vichwa vigumu kama nazi na pia umueleze mpenzi wako kuhusu huyo mpenzi wako wa zamani cuz itakuwa rahisi zaidi kwa mpenzi wako kukuelewa na kukuamini endapo atasikia habari hizo kutoka kwako kuliko akisikia habari hizo kutoka kwa mtu mwingine. Kuwa makini dada yangu, usipoziba ufa, utajenga ukuta. Ni hayo tu kwa leo. Kama utakuwa na tatizo jingine, tafadhali usisite kuwasiliana nami.
 
we young master unamaanisha nini asisite kuwasiliana na wewe? hapa anatafuta ushauri wa wana jf wote mbona kama unataka kumonopolize tatizo,
 
ngoja kwanza niende nikachome sindano nikirudi ntakushauri vizuri tu!
 
je mpenzi wako mpya anajua kuwa huyo kaka ulikuwa unatoka nae? Kama hukuwahi kumwambia keti zungumza nae kuhusu uhusiano uliokuwa nao na huyomtuma msg........

Mwanaume wa ukweli atakuelewa.
 
Naona wengi wametoa ushauri mzuri sana. Kweli, kaa chini mwambie ukweli huyo mpenzi wako wa sasa, mwambie nini kinachoendelea, usimfiche chochote. Halafu, huyo mwanaume wa zamani anaonekana mshamba sana, how come alikuwa anakutesa kihivyo? Yaani anaongea na simu na mpenzi wake mbele yako? Tatizo kuna wanaume wengine wakijua mwanamke amekufa kimapenzi wanaitumia hiyo chance vibaya. Pole sana dada.
 
yaani we acha tu ndugu yangu yaani aliniumiza vibaya sana.
 
Ni ukweli tu utakoa kuweka huru. Tatizo la ukweli ni kuwa hauaminiwi na watu wengi, ukweli hukuongezea matatizo, ukweli huumiza lakini ni ukweli tu ndio utakao kuweka huru. Mpe kweli huyo Bwanao mpya kumhusu huyo KARUMEKENGE aliyekataa kupendwa. Nategemea mafanikio mema katika kuuandaa na kuusema ukweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom