Nilimpotezea huyu mwanamke kwa hii kauli ya kishenzi

Mbona swali la kawaida sana hilo kwa mtu umpendaye!

Unaonekana ni mtu mwenye stress sana wewe, wale watu wa mihasira hasira hivi...
Hata hivo nna hasira kweli mkuu.. Huwa sipendi mtu awe kinyume na nnachomwambia.. Hata niliyenaye sasahiv anajua.. Hata mama pia anajua hilo.. Inawezekana ni weakness pia.. But ndo nilivo
 
kwanza mleta uzi anaitwaje, ?
NAANTOMBE MUSHI. Oke tuendelee...!
UNAKOSAJE PESA MWISHO WA MWEZI, ? alistahili adhabu ulompatia japo umechelewa kutupa story au umemumisi
Hahahaha.... Niliingia facebook jana nikakuta friend request yake ndo ikabidi nikumbuke kilichotokea miaka minne iliyopita
 
Huyo hakuuliza swali Bali alishangaa Mana ulimzoeza kila mwisho wa mwezi unamtoa hela
Mi naona alijisahau tu na alikuwa na kiwewe cha kufanya hiyo shughuli yake zaidi ya kujihangaisha kujua kwamba atumie lugha ipi inayofaa
 
Dooh, bado anakukumbuka bc msalimie sana wifi, ! ikiwezekana mlete na huku aje atusalimie
Aaaah.. Ni zama zimeshapita maana hata hivo tayar nna family na mtoto so automatically hana nafasi tena kwangu.. Btw ni mtu poa sana
 
Niende moja kwa moja kwenye mada,

July 2015 asubuhi ya saa nne nikiwa nimetoka kwenye dawati langu naelekea washroom, nilikutana na binti mmoja kwenye corridor akiwa na bahasha ya kaki mkononi. Yeye ndo alianza kunisalimia na baada ya kumsalimia akaniambia "Bro samahani nimekuja kwenye interview ya legal officer sijui unaweza kunielekeza?"

Kwa sababu interview room ni office fulani ipo ndani, ilibidi nijitolee kumpeleka kwanza mapokezi halafu mimi nikaelekea washroom.

Baada ya kurudi washroom, nilimkuta akiwa kwenye bench anasubir. Inaonesha kweli kulikuwa na interview zinaendelea maana mda ule niliona tena watu wengine kama wawili wamekuja pale.

Nikaamua nijivute kwenye kiti nimuulize mawili matatu, maana alikuwa ni binti tu mzur ameumbika.

Baada ya story mbili tatu nikagundua ndo alikiwa amemaliza chuo mwaka huo huo 2015 so hapo kuna mtu tu alimpigia pande maana hata cheti alikuwa bado hana.

***

Wakati huo nilikuwa ndo nimeanza kazi kwenye moja ya bank kubwa sana hapa nchini.

Baada ya story mbili tatu akaniambia yeye amesoma UDSM na kwa sababu na mimi pia nilisoma UDSM story zikaanza kutiririka.

Mimi: Hivi, Prof Mgongo Fimbo bado yupo? Nasikia mtata sana jamaa yule...

Yeye: Hahahahahahaaaa Yupoo!!

Ikawa hivo, bla bla blaa nyingi.. Ikaishia nikachukua namba zake kwa nia kwamba nitaendelea kuwasiliana nae.

***
Bahati mbaya ile kazi aliikosa kwa kigezo cha uzoefu maana ndo kwanza alikuwa amemaliza chuo.

Kwa kipindi kifupi cha mawasiliano ya hapa na pale na kuzidi kumsoma nikagundua ni binti tu mwenye maadili na kizuri zaidi alikuwa ni msabato na alikuwa ameshika dini mno.

Mi kimoyoni nikawa namfikiria kama mke mtarajiwa maana ki ukweli yule binti ni mzuri. Alikuwa ni black girl fulani hivi baba yake ni Mnyamwezi na Mama yake ni mkurya. Guu kama lote na shape heeeeh debe halafu hee toto ameshika dini.

Nikasema hapa hata mama Mushi akileta za kuleta eti hataki mnyamwezi ningempinga kwa sauti kubwa.

**
Ki ukweli yule binti sikutaka kumtakia kwamba nampenda kwa wakati huo. Japo nilikuwa nimeshakufa na kuoza kwake.

Ili kuhakikisha hakuna Bwege anatia mguu na kumyumbisha ikabidi nimpe treatment kama mpenzi wangu. Kwa kuwa wakati huo alikuwa hajapata kazi bado so nikawa najitoa kisawasawa.

Messages na maphone ilikuwa kila wakati nikipata chance lazima nimchek. Kila mwisho wa wiki jpili ilikuwa lazima nimtoe out. Nguo, saa na vipoch vya kutosha..

Mi sielewi mambo ya kisheria sana, ila alikuwa pia akihudhuria school of law pale mawasiliano akaniambia kuna uwezekana mkubwa akamaliza mwishoni mwa mwaka huo huo na ku graduate.

****
Cut long story short,

Yule binti alikuwa amefaulu hiyo mitihani yake ya school of law. So kilichokuwa kinafuatia hapo ni kufanya sherehe ya graduation.

Mimi alinipa taarifa na kuniambia kwamba ndugu zake wote watakuwepo siku hiyo na kwamba tayar walikwisha mchangia pesa kwa ajili ya kufanya sherehe.


Maandalizi ya graduation yake yakiendelea, nakumbuka siku moja akanipigia simu asubuhi sana. Nakimbuka ilikuwa ni siku ya tarehe 29 (Siku mbili baada ya mshahara).

Note: ukweli ni kwamba japo hii siku ilikuwa ni ya mwisho wa mwezi ila mshahara wote ulioingia nilikuwa nimempa mwenye nyumba kwa kuwa ndo ulikuwa mwisho wa mkataba so nikawa nimekubaliana na mwenyenyumba kuongeza tena kama miezi 6 (Nililipa kama laki 9) . So nikawa nimebakiwa na kama laki 3 na nusu)

Maongezi ya ile simu ya asubuhi ya tareh 29 yalikuwa kama ifuatavyo.

Yeye: Mushieehh.. Umeamkaje baba! (kwa zile huduma nilikuwa nampatia
alitokea kunizoea nadhani alihisi tumeshazama kwenye mapenzi tayar wakati sikuwa nimemtamkia)

Mimi: Nimeamka poa ndo najiandaa kwenda kazini mama akee.

Yeye: Naomba uniongezee laki 3 nimepungukiwa na bajeti ya maandalizi ya sherehe. Kwakuwa nilikuwa nimebakiwa na laki 3 na nusu tu, nisingeweza kumpatia hiyo pesa (Ukweli ni kwamba laiti ningekuwa na hela ningempatia bila hata kujiuliza mara mbili) ikabidi nifunguke tu

Mimi: Daah leo nipo vibaya mama sina hiyo hela kabisa.


Yeye: UNAKOSAJE HELA NA LEO NI MWISHO WA MWEZI?

Hakika sikutegemea hili swali la kipuuzi namna hii. Nilimchukia ghafla na kumtoa moyoni ndani ya mda mfupi.

Sikutaka kumuonesha nimekasirika kwa mda ule na pia sikutaka kumjibu swali alilouliza. Ikabidi nimjibu tu

Mimi: Anyway, embu ngoja nifanya utaratibu then baadae ntakujulisha.

Nilitaka kujipa mda wa kuandaa mazingira ya kulipa kisasi cha kuulizwa swali la kipumbavu.

Kwa kuwa nilimuambia ntafanya utaratibu, mchana wake akanipigia simu ila sikupokea.

Usiku akapiga tena kama tano na sikupokea vile vile. Niliapa kukata mawasiliano once and for all.

Kesho yake vile vile akawa anapiga simu. Na mimi nikaacha kupokea vile vile.

Nikahisi hapa huyu atakuja ghetto maana haikuwa kawaida yangu kutokupokea simu zake.

Mchana wa siku ya pili nikamtext "Nimepata dharura naelekea Moshi mara moja kuna mambo ya kifamilia"

Akajaribu kupiga saa hiyo hiyo, mi sikupokea tena. Tuma message zake nyingi tu na sikumjibu.

Sikumjibu, sikumjibu, sikupokea simu zake tena, sijui ni kwa namna gani nilimuumiza moyo wake. Na ndo mwisho wa uhusiano na binti.

Mwaka jana nikikutana na binamu yake Mlimani City akaniambia 'Roselyn' anafanya kazi kwenye shirika moja kubwa ila yupo kikazi kenya.

Nilifurahi kwa kuwa ameendelea na maisha yake na amepiga hatua. Yawezekana hakuwa mtu sahihi kwangu au mimi sikuwa mtu sahihi kwake.

But yote kwa yote, swali aliloniuliza lilikuwa ni la kipuuzi.
Mwanaumen mwerevu huwa haishiwi pesa. Ungempa jibu halisi tu kuwa umelipa kodi ya nyumba na bajeti imebana, ungeweza kumpa hata hiyo 50,000 angeshukuru.

Tatizo lako ulijinyanyapaa mwenyewe na kujiondoa. Inferiority complex yako itakugharimu, na hilo jibu tegemea toka kwa mwanamke yeyote makini, kuwa smart kutoa jibu smart na sio kukimbia. Huyo dada hakukosea chochote kukuuliza kutegemea na ulichokuwa ukimfanyia na uelewa wake juu ya kipato chako



Ulikosea sana.
 
Swali la kawaida sana mbona unless kuna mengine hujatuambia.

Hata kama kweli ulikereka hai-make sense kumpoteza mwenye una malengo naye na ume-invest kwake kisa mistake moja tu tena ndogo kama hiyo

Huyo mkamilifu umeshampata sasa?
 
Sema hawa viumbe wengi wapo hivyo, don't expect much from them.

Siku kama mbili tatu hivi zimepita nilipiga story na wadada wawili sio watz, mmoja akasema anaweza mvumilia mwanaume akifulia mwezi mmoja tu, na mwingine akasema anaweza enda miezi miwili tu.

Wewe ungemchukulia hivyo hivyo, ukampanga akapangika, ndio vile tunafanyanga.
 
Nilijiuliza maswali mengi sana.
1. Inamaana ni kwanini haeshimu ninachomuambia?
2. Je hajui kuna siku kwenye maisha unaweza kuwa broke?
gia uliyoingia nayo kwake ilikuwa sio, yaani umemjengea mazingira we gari la mshahara a.k.a kimwaga makono...akikohoa tu unazitapika na pengine hata hakukuhurumia kuwa unavuja jasho ili kuzipata - angelijua hilo angefaa zaidi kuwa mke ila mpaka hapo ulishamharibu - sio kila kitu apate hata kama una mil 100 benki kuna muda anapaswa kujua kuwa kuna majukumu mengine pia, nikupe mfano kdg kuna binti kipindi fulani nilikua nae, sasa alikua akiwa na hitaji natuma hapo hapo instantly siku moja akaniambia shem wako anaomba laki moja kuna sehem anaenda mwazime atarudisha jioni, nikamtumia instantly sikuiona kurudishwa hiyo jioni, me nikanote tu, kama mwezi hivi shem akakwama nikaombwa tena 50 nikamwambia hiyo pesa haipo aisee huyu kaka yako asiyeheshimu jasho langu hapana atafute kwingine tu - ila nikajifunza ni vile mimi nilivyoweka mazingira kwa binti alikua anaona me atm yake
 
Hata hivo nna hasira kweli mkuu.. Huwa sipendi mtu awe kinyume na nnachomwambia.. Hata niliyenaye sasahiv anajua.. Hata mama pia anajua hilo.. Inawezekana ni weakness pia.. But ndo nilivo
Hufai kuwa kiongozi, your are not diplomatic! Unatumia bastola kuua nzi...haifai!
 
Sasa si maisha yako yatakuwa ni ya kuwapoteza uwapendao...

Wanawake kwa kawaida hawavutiwi sana na mwanaume mwenye hasira hasira, maana humuona ni mtu asiyejiamini..
Hata hivo nna hasira kweli mkuu.. Huwa sipendi mtu awe kinyume na nnachomwambia.. Hata niliyenaye sasahiv anajua.. Hata mama pia anajua hilo.. Inawezekana ni weakness pia.. But ndo nilivo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom