Nilichomshauri DK WILBROAD SLAA nilipokutana nae

Kwa nini hao 30%-40% wanaojitokeza wasichague CDM waichague CCM? Kikulacho ki nguoni mwako!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu endelea kumshauri babu madudu na utegemee pengine atakukubalia.
Akikubali imekula kwake anyway.

Swali la kujiuliza kwako, kama una akili ya kuchambua maswala, ni kwamba, kama CHADEMA wamekuwa popular na chopa kutengeneza inroads kwa uanachama watu waliokuwa CCM, Walioandikisha hiyo 2009 wako wapi?

Msijipe sababu ambazo na nyie wenyewe mnajua hazina mashiko.
Chances are hata daftari likiboreshwa kesho, wananchi wengi zaidi watachagua CCM, maana zaidi ya kulalama na polisi na maandamano, CDM haina mchango wowote kimawazo jinsi ya kuliendeleza ztaifa hili.

Msifikiri wTanzania ni wajinga, they know where their hearts lie.

Na kama ni wewe ulimshauri juu ya kukodi chopa tatu, matokeo yake mmeshayaona.

Waliboreshe basi wasipige chenga kama unaona hakutakuwa na madhara yoyote...
 
Kwa nini hao 30%-40% wanaojitokeza wasichague CDM waichague CCM? Kikulacho ki nguoni mwako!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa sababu CHADEMA imepata nguvu sana baada ya uchaguzi 2010,wengi wa wanao support CDM nu vijana walio kwenye hilo rika lililotajwa kama nimemuelewa vizuri mtoa mada.
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,
 
Ni vyema Mheshimiwa umetoa kauli,Natumai ujumbe umefika...
 
Huko kote mbali ungemshauri kwanza abadilishe M4C movement for Change na kutafuta neno la Kiswahili linaloeleweka na hapo ndio utakuwa mwanzo wa kuona kweli hawa wanawajali wananchi wa kawaida na sio wazungu! kama CCM, Nguvu Mpya Ari Mpya, Maisha Bora kwa kila Mtanzani n.k

vuguvuvu la mabadiliko ndo kiswahili chake mdau.
 
Nilipokutana na katibu mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa baada ya kushindwa vibaya na CCM kwenye uchaguzi ulioisha siku za karibuni nilizungumza nae mambo makuu mawili (wanajamvi mtaongezea mengine) ambayo pengine yamechangia ya huenda yakapelekea kutoa matokeo yaleyale kama hayatafanyiwa kazi.

i)Nilimkumbusha aangalie tofauti kubwa inayojitokeza baina ya wananchi wanaojitokeza kupiga kura na wale waliojiandikisha tofauti ni kubwa sana. Ni wastani wa 30%-40% ndio wanaojitokeza kupiga kura .Hata kwenye hizi chaguzi ndogo zilizopita hali ni hiyo hiyo. Nikamkumbusha hata 2010 Rais wa nchi alichaguliwa na watu wasiozidi mil 5 kati ya takribani watu mil 20 waliojiandikisha. Sasa ukitoa wale waliopoteza au KUUZA shahada zao kwa hiari baada ya kurubuniwa na wanasiasa(hasa CCM),pia ukiondoa wale wanaoshindwa kufika kwenye vituo vya kupiga kura kwa hofu ya vurugu zinazozuka muda mfupi kabla ya uchaguzi,sababu inayotolewa na wengi ambao hawajitokezi kupiga kura ni kutokuwa na imani na wagombea husika.

Hivyo inawezekana kabisa CCM ikawa inashinda hizi chaguzi kwa sababu tu watu wengi hawajitokezi kupiga kura na si kuwa wanakubalika kama wanavosema wenyewe. Nilimshauri waongeze bidii kwenye mpango mkakati yao,ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha na ya dhati ili wananchi wajitokeze kupiga kura kwenye chaguzi zijazo.Yanaweza yakapatikana matokeo tofauti na ilivyo sasa. Pia nilimtahadharisha kuwa wasitegemee CCM kulifanya hilo la kutoa elimu. Katibu mkuu wa CCM Mh A.Kinana aliwahi kutoa kauli kwamba anaridhika na mahudhurio katika chaguzi.Kwa CCM hata akitokea mpiga kura mmoja kati ya mia,ilimradi hiyo kura moja ni ya kwao hawana tatizo kabisa. Wanachotaka ni ushindi tu.

ii)Pia nilikubaliana nae kwamba kutoboreshwa daftari la wapiga kura kunachangia CCM kupata ushindi mkubwa ikiwa ni pamoja na chaguzi zilizoisha punde. Nimemtahadharisha kama wataenda kushiriki kwenye chaguzi za CHALINZE na KALINGA bila ya daftari la wapiga kura kuboreshwa watarajie KIPIGO KITAKATIFU kutoka CCM na pia nikamchekesha baada ya kumwambia aandae kabisa sababu za kuwadanganya wana CHADEMA kutokana na kushindwa kwao kwenye hizo chaguzi.

Inafahamika mara ya mwisho daftari la wapiga kura liliboreshwa mwaka 2009 kuelekea uchaguzi 2010. Ni zaidi ya miaka MITANO sasa.Kuna idadi kubwa ya vijana kati ya miaka 18-28 hawamo kwenye daftari la wapiga kura ,achilia mbali waliopoteza shahada zao(inakadiriwa zaidi ya watu mil 5 hawamo).Ni idadi hii ya watu mil 5 ndio ilimuweka Rais madarakani.

Na nikamkumbusha ni hao hao vijana wengi walio kwenye hiyo rika nililotaja hapo juu ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA na ndio hao hao CCM kwa makusudi wanawanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura. Fahamuni suala la kucheleweshwa kuboresha daftari la wapiga kura halifanywi kwa bahati mbaya.Na hakika msipoangalia mtaendelea kujaza maelfu ya wananchi katika mikutano yenu ambao ndio hao hao walio kwenye hilo rika nililotaja hapo juu ambao hawamo kwenye daftari la wapiga kura. Ni juzi tu katibu mkuu wa CCM Ndugu A.Kinana alitoa kauli kwamba anaridhika na idadi ya wanaojitokeza kupiga kura na haoni sababu ya kuboreshwa daftari la wapiga kura.

Sina hakika sana kama Mh amenielewa ila ujumbe umfikie….!
sasa kama watu now hawajitokezi kupiga kura daftari likiboreshwa ndio watajitokeza kupiga kura !?
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,
Dr Slaa, kwanza niseme hoja ya Ochutz ina maana sana kwa wakati huu. Kama mliongea au la hilo soi hoja, hoja iliyopo ni mantiki ya hoja yake.

Ninakumbuka Mzee Mwanakijiji aliandika kuhoji upigaji wa kura Mbeya vijijini ambao ulikuwa ni asilimia 30.

Mwemyekiti wa NEC aliulizwa na hakuwa na jibu kwanini watu wajiandikishe asilimia 70 halafu wapige kura asilimia 30.

Huko nyuma kulikuwa na ushahidi wa ununuzi wa shahada za kupiga kura ambao uliisha kimya kimya bila ninyi wapinzani kufutailia.

Hoja ya Otchuz ni kuwa inawezekana kabisa kampeni zenu ni effective lakini mnashindwa 'technically'.

Unakumbuka baada ya kuanza kulinda vituo wizi ulibadili sura ya matokeo kwa kiasi kikubwa.
Je, mumeangalia kwa undani nini kinaendelea na asilimia ndogo ya wapiga kura?

Sidhani kama Otchuz kuandika katika gazeti kungeweza kuwa na impact kuliko ninyi wapinzani rasmi kulizungumzia suala hilo, hivyo ni muhimu ukaiona hoja yake bila kumjua au kuwa na prejudice dhidi yake

Utakumbuka kuwa tuliwahi kuwa na mjadala na hapa tena namnukuu Mwanakijiji kwa kusema kuwa vyama viwe na madaftari ya wapiga kura wao sambamba na la wapiga kura la NEC.
Je, mnajua wanachama wenu wangapi wanakwenda kupiga kura?

Laiti mngekuwa na daftari pengine mngekuwa na ushahidi mzuri sana wa kutahmini wapi tatizo lilipo.Hivyo ndivyo wanavyofanya wenzenu katika vyama vingine huko duniani. Hakuna kosa la kisheria kuandikisha wanachama wako na kuwafahamu.

Ni muhimu ukakubali kuangalia hoja bila kutanguliza hoja za nani anajua nani hajui.

Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Swala la kuboresha daftari la kupiga la mpiga kura ni muhimu ila swala la elimu ya uraia na Sera ni muhimu sana. Cmd inabidi iuze Sera zake kwa rika zote sio kutegemea kundi la vijana tu
 
Kwa sababu CHADEMA imepata nguvu sana baada ya uchaguzi 2010,wengi wa wanao support CDM nu vijana walio kwenye hilo rika lililotajwa kama nimemuelewa vizuri mtoa mada.
Therefore they are fighting the wrong battle!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ushauri mzuri muhimu ni elimu ya uraia watu waone ni haki ya msingi kujiandikisha na kupiga kura
 
Hayo yote anayajua, asichokijua ni kuwa ubaguzi ndani ya chama ndo THREAT kubwa. Kitila angekuwepo angefanya utafiti na kujua wapi wamekosea, lakini waliobaki wote ni propaganda uchumia tumbo.
Kwa ushauri huo unamaanisha kuwa watu wakizeeka wanaichukia CDM na kuipenda CCM, ambacho kwa mtazamo usio rasimi ni kuwa watu wanapoongezeka umri wanajitambua na kuanza kuona mbali na kutodanganyika.
Kwa mtazamo huo na ushauri CDM imepoteza dira, maana huwezi aminisha watu kuwa waliokufa, waliopoteza viparata vya kupigia kura, wagonjwa wasioweza kufika kupiga kura, wazee na vikongwe wasioweza kufika vituoni kupiga kura wote ni CDM.
Kwa kuwa waliobaki hawawezi kujitafakari, imekula CDM:wave:

Nilipokutana na katibu mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa baada ya kushindwa vibaya na CCM kwenye uchaguzi ulioisha siku za karibuni nilizungumza nae mambo makuu mawili (wanajamvi mtaongezea mengine) ambayo pengine yamechangia ya huenda yakapelekea kutoa matokeo yaleyale kama hayatafanyiwa kazi.

i)Nilimkumbusha aangalie tofauti kubwa inayojitokeza baina ya wananchi wanaojitokeza kupiga kura na wale waliojiandikisha tofauti ni kubwa sana. Ni wastani wa 30%-40% ndio wanaojitokeza kupiga kura .Hata kwenye hizi chaguzi ndogo zilizopita hali ni hiyo hiyo. Nikamkumbusha hata 2010 Rais wa nchi alichaguliwa na watu wasiozidi mil 5 kati ya takribani watu mil 20 waliojiandikisha. Sasa ukitoa wale waliopoteza au KUUZA shahada zao kwa hiari baada ya kurubuniwa na wanasiasa(hasa CCM),pia ukiondoa wale wanaoshindwa kufika kwenye vituo vya kupiga kura kwa hofu ya vurugu zinazozuka muda mfupi kabla ya uchaguzi,sababu inayotolewa na wengi ambao hawajitokezi kupiga kura ni kutokuwa na imani na wagombea husika.

Hivyo inawezekana kabisa CCM ikawa inashinda hizi chaguzi kwa sababu tu watu wengi hawajitokezi kupiga kura na si kuwa wanakubalika kama wanavosema wenyewe. Nilimshauri waongeze bidii kwenye mpango mkakati yao,ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha na ya dhati ili wananchi wajitokeze kupiga kura kwenye chaguzi zijazo.Yanaweza yakapatikana matokeo tofauti na ilivyo sasa. Pia nilimtahadharisha kuwa wasitegemee CCM kulifanya hilo la kutoa elimu. Katibu mkuu wa CCM Mh A.Kinana aliwahi kutoa kauli kwamba anaridhika na mahudhurio katika chaguzi.Kwa CCM hata akitokea mpiga kura mmoja kati ya mia,ilimradi hiyo kura moja ni ya kwao hawana tatizo kabisa. Wanachotaka ni ushindi tu.

ii)Pia nilikubaliana nae kwamba kutoboreshwa daftari la wapiga kura kunachangia CCM kupata ushindi mkubwa ikiwa ni pamoja na chaguzi zilizoisha punde. Nimemtahadharisha kama wataenda kushiriki kwenye chaguzi za CHALINZE na KALINGA bila ya daftari la wapiga kura kuboreshwa watarajie KIPIGO KITAKATIFU kutoka CCM na pia nikamchekesha baada ya kumwambia aandae kabisa sababu za kuwadanganya wana CHADEMA kutokana na kushindwa kwao kwenye hizo chaguzi.

Inafahamika mara ya mwisho daftari la wapiga kura liliboreshwa mwaka 2009 kuelekea uchaguzi 2010. Ni zaidi ya miaka MITANO sasa.Kuna idadi kubwa ya vijana kati ya miaka 18-28 hawamo kwenye daftari la wapiga kura ,achilia mbali waliopoteza shahada zao(inakadiriwa zaidi ya watu mil 5 hawamo).Ni idadi hii ya watu mil 5 ndio ilimuweka Rais madarakani.

Na nikamkumbusha ni hao hao vijana wengi walio kwenye hiyo rika nililotaja hapo juu ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA na ndio hao hao CCM kwa makusudi wanawanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura. Fahamuni suala la kucheleweshwa kuboresha daftari la wapiga kura halifanywi kwa bahati mbaya.Na hakika msipoangalia mtaendelea kujaza maelfu ya wananchi katika mikutano yenu ambao ndio hao hao walio kwenye hilo rika nililotaja hapo juu ambao hawamo kwenye daftari la wapiga kura. Ni juzi tu katibu mkuu wa CCM Ndugu A.Kinana alitoa kauli kwamba anaridhika na idadi ya wanaojitokeza kupiga kura na haoni sababu ya kuboreshwa daftari la wapiga kura.

Sina hakika sana kama Mh amenielewa ila ujumbe umfikie….!
 
Wewe usichoelewa nini? Ujumbe umemfikia ndio maana ametoa kauli...
Umeanza lini kuandika mitandaoni?Kujieleza kidogo tu kunakupa kazi.Ungemwambia "ujumbe umemfikia",unaposema ujumbe umefika ni kama una acknowledge kwa upande wako...kwamba ujumbe umekufikia.
 
Back
Top Bottom