Nilichokiona udom

MKURABITA

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
317
126
Ndugu wana JF, mtakumbuka kuwa hivi karibuni Chuo kikuu cha Dodoma UDOM wametangaza nafasi nyingi za ajira, ambazo mwisho wa kutuma maombi itakuwa tar. 10 Sept.

Leo nimepeleka barua ya maombi ya rafiki yangu. Nilichokiona pale masijala ya UDOM mpaka nimeogopa. Nimekuta wahudumu wakichambua barua kulingana na nafasi za kazi. Kwa ufupi ni kwamba maombi ni mengi kupita maelezo. Na kwa dokezo nililopewa na mmoja wa wahudumu, kuna uwezekano mkubwa ili kukata mzizi wa fitina, kuwaita wote walioomba na kuwapa written paper kabla ya kushortlist watakaofaulu na kuwaita kwenye oral interview.

Ushauri wangu wote waliotuma application UDOM: Kama utaitwa kwenye intervie, ni vizuri ujiandae kifedha kwani kuna uwezekano kipindi hicho watu wakawa wengi sana hivyo kukawa na scarcity ya malazi na gharama kupanda kwani Dodoma bado Hotel na Guest Houses si nyingi.

Nimegundua leo kuwa huu mfumo wa Serikali kutaka kila mtu aende University utaighalimu nchi. Ni vema wangejenga vyuo vingi vya ufundi ili kupunguza msongamano wa kila mtu kutaka kuajiliwa. Ikumbukwe kuwa vyuo vikuu vyetu vingi vina programmes na mitaala ambayo haimjengi mtu kujiajili.

Nawatakia kila la kheri wote mlioomba ajira.
 
Ndugu wana JF, mtakumbuka kuwa hivi karibuni Chuo kikuu cha Dodoma UDOM wametangaza nafasi nyingi za ajira, ambazo mwisho wa kutuma maombi itakuwa tar. 10 Sept.
ni kweli kabisa mkuu upo sahihi.
Leo nimepeleka barua ya maombi ya rafiki yangu. Nilichokiona pale masijala ya UDOM mpaka nimeogopa. Nimekuta wahudumu wakichambua barua kulingana na nafasi za kazi. Kwa ufupi ni kwamba maombi ni mengi kupita maelezo.
hii ni kawaida mkuu kutokana na idadi kubwa ya watu kukaa mtaani bila ajira, wala usiogope kama ana vigezo rafiki yako atapata ajira tu
Na kwa dokezo nililopewa na mmoja wa wahudumu, kuna uwezekano mkubwa ili kukata mzizi wa fitina, kuwaita wote walioomba na kuwapa written paper kabla ya kushortlist watakaofaulu na kuwaita kwenye oral interview.
mkuu hao wahudumu wao wamejuaje?, nadhani haiingii akilini kuita watu WOTE kufanya mtihani kabla ya kushortlist!. itakua ni kupoteza muda na kuwaingizia gharama zisizo na msingi waomba ajira, kama ni kweli hili UDOM jipangeni bana.
Ushauri wangu wote waliotuma application UDOM: Kama utaitwa kwenye intervie, ni vizuri ujiandae kifedha kwani kuna uwezekano kipindi hicho watu wakawa wengi sana hivyo kukawa na scarcity ya malazi na gharama kupanda kwani Dodoma bado Hotel na Guest Houses si nyingi.
kama ni malazi tu ya watu kufanya interview, nafasi kwenye loji, gesti hausi, hoteli ZITATOSHA mkuu usiogope!. na hata udom pale wana hosteli za maana sana baadhi ya taasisi zinapofanya mikutano yao huenda kukodisha hosteli pale, wana vyumba vya kumwaga mnooooo. PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA!, watu "wao" hawatakosekana ambao tayari wameshapeleka vimemo, nguvu ya Mungu inahitajika zaidi namaanisha maombi!. kila la khei mpwa kwa rafiki yako!.
 
usiogope ktk wale wengi na wewe lazima uwepo, cha msingi Mkabidhi Mungu
 
Hakuna kuogopa mkuu, pambana mpaka mwisho, ajira ni ngumu sana!
 
Hizo ni mbwembwe zao tu. Nyie mloomba kazi jipangeni vema kwa interview ndio dawa.
 
Ndugu wana JF, mtakumbuka kuwa hivi karibuni Chuo kikuu cha Dodoma UDOM wametangaza nafasi nyingi za ajira, ambazo mwisho wa kutuma maombi itakuwa tar. 10 Sept.

Leo nimepeleka barua ya maombi ya rafiki yangu. Nilichokiona pale masijala ya UDOM mpaka nimeogopa. Nimekuta wahudumu wakichambua barua kulingana na nafasi za kazi. Kwa ufupi ni kwamba maombi ni mengi kupita maelezo. Na kwa dokezo nililopewa na mmoja wa wahudumu, kuna uwezekano mkubwa ili kukata mzizi wa fitina, kuwaita wote walioomba na kuwapa written paper kabla ya kushortlist watakaofaulu na kuwaita kwenye oral interview.

Ushauri wangu wote waliotuma application UDOM: Kama utaitwa kwenye intervie, ni vizuri ujiandae kifedha kwani kuna uwezekano kipindi hicho watu wakawa wengi sana hivyo kukawa na scarcity ya malazi na gharama kupanda kwani Dodoma bado Hotel na Guest Houses si nyingi.

Nimegundua leo kuwa huu mfumo wa Serikali kutaka kila mtu aende University utaighalimu nchi. Ni vema wangejenga vyuo vingi vya ufundi ili kupunguza msongamano wa kila mtu kutaka kuajiliwa. Ikumbukwe kuwa vyuo vikuu vyetu vingi vina programmes na mitaala ambayo haimjengi mtu kujiajili.

Nawatakia kila la kheri wote mlioomba ajira.

Chukulia shahada ya kwanza ni kiwango cha elimu tuu (education level); some one to be able to be effectively used at work plance he/she has to go for speciliazation like MBA, MSc, CPA, etc
 
NAME OF POST:Teaching Staff (viz.
Professors, Associate Professors,
Senior Lecturers, Lecturers) in
University of Dodoma,
Tanzania .
Departments: Petroleum
Engineering, Mining Engineering,
Mineral Processing Engineering,
Geology, Physics, Mathematics,
Statistics, Chemistry, Law,
Economics.
ELIGIBILITY:
Name of
the Post Qualification Monthly Salary (in
Tshs.)
Professors
• PhD Degree plus Masters and
Bachelors Degree with
appropriate GPA’s
• Must have at least 10
publications since his/her last
promotion.
• 80% of the publications i.e.
papers, articles must be
published in international or
referred journals.
• 60% of those publications,
must be single authored or he/
she is the main author in case of
the co-authored paper
• Must have at least 4 papers in
refereed international journals
4,390,300.00
Associate
Professors
• PhD Degree plus Masters and
Bachelors Degree with
appropriate GPA’s
• Must have at least 10 points of
publications since his/her last
promotion.
• 80% of the publications i.e.
papers, articles must be
published in international or
referred journals.
• 60% of those publications,
must be single authored or he/
she is the main author in case of
the co-authored paper
• Must have at least 4 papers in
refereed international journals
4,203,300.00
Senior
Lecturers
• PhD Degree plus Masters and
Bachelors Degree with
appropriate GPA’s
• Must have at least 6
publications since his/her last
promotion.
• 50% of the publications i.e.
papers, articles must be
published in international or
referred journals.
• In case of the co-authored
paper, 50% of those
publications, he/she must be the
main author.
3,829,300.00
Lecturers • PhD Degree plus Masters and
Bachelors Degree with
appropriate (GPA ≥ 4.0 for
Masters by Coursework and
dissertation plus an upper
second class undergraduate level
degree). OR
• PhD Degree plus Masters by
Research plus GPA ≥ 3.8 at
Bachelor Degree level.
• For unclassified degrees overall
average of B grade and above. 2,935,800.00
*** Exchange rate 1 USD
equivalent to Tshs. 1,590.00
LOCATION:Tanzania.
LAST DATE:13 Aug 2012 .
www.shiningjobs.com/jobs/details_govt_jobs/government-jobs-details-04081202-EdCIL%20(India)%20Limited.html
 
Natafuta jina la Human Resource Manager wa Udom, nimegugo bila mafanikio. Kwa yeyote anayemjua na personal contact zake basi anipatie wadau.
 
last time nilivyokwenda ilikuwa balaaa...i hope this time itakuwa more worse...ila wakiniita nimo..na nitalala stand tu kama last time
 
ni kweli kabisa mkuu upo sahihi. hii ni kawaida mkuu kutokana na idadi kubwa ya watu kukaa mtaani bila ajira, wala usiogope kama ana vigezo rafiki yako atapata ajira tu mkuu hao wahudumu wao wamejuaje?, nadhani haiingii akilini kuita watu WOTE kufanya mtihani kabla ya kushortlist!. itakua ni kupoteza muda na kuwaingizia gharama zisizo na msingi waomba ajira, kama ni kweli hili UDOM jipangeni bana. kama ni malazi tu ya watu kufanya interview, nafasi kwenye loji, gesti hausi, hoteli ZITATOSHA mkuu usiogope!. na hata udom pale wana hosteli za maana sana baadhi ya taasisi zinapofanya mikutano yao huenda kukodisha hosteli pale, wana vyumba vya kumwaga mnooooo. PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA!, watu "wao" hawatakosekana ambao tayari wameshapeleka vimemo, nguvu ya Mungu inahitajika zaidi namaanisha maombi!. kila la khei mpwa kwa rafiki yako!.

Labda umejibu thread hii ukiwa nje ya nchi ama basi tu umeamua kubisha. Last time hicho ndicho udom walichofanya yaani kuita applicants wote kuja kufanya written interview. Karibu watu alfu 3 na kitu walitokea. Matokeo yake usafiri wa Dar - Dodoma ulikuwa mgumu, malazi Dodoma yalikuwa ya taabu nk. Tahadhari aliyoitoa mleta thread iko well founded.
 
Mh! Hali mbaya, kwa mtindo huu elimu ya kusoma sana siku hizi haina dili, cha msingi mtu ukipata "BASIC" tafuta kijiwe ujihifadhi kwanza
 
kama haumini mimi nilikua hombolo ilikua ni balaa na kwa sasa tunasubiria maumivu, lakin nahisi tutapata, lakini mbona kuna factor nyingi za kushortlist kwa nini wawajaze watanzania sehemu moja hali ya kuwa wengine wanakopa hiyo nauli pamoja na gharama nyingine ni bora ukadhurumiwa kwenye shortlist kuliko kwenye interview so inauma sana
 
matatiz tulia na kuwa na imani ipo siku utafanikiwa so omba mungu naamini we ni muumini wa dini fulani, hata ukimuona hr kama mungu hajataka upate utakosa tu
 
Back
Top Bottom