Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 733
- 1,677
Ni kwamba hawa watu wa mtaani kwetu wananiiga au na wao uchumi umewapiga kama Mimi.
Ni hivi niliwahi kuandika Uzi hapa nikisema nimeamua kuwatoa watoto wangu English Medium na kuwaleta Kayumba baada ya uchumi wangu kuzorota. Then nikaja nikaanzisha Uzi kuhusu FAIDA binafsi nilizo zipata baada ya kuwahimishia watoto wangu Kayumba.
Leo nimeenda shuleni kulikuwa na kikao cha wazazi. I was surprised KUKUTANA na watu zaidi ya kumi ambao na wao watoto wao walikuwa wanasoma English Medium na sasa wamewahamishia Kayumba.. Nilishindwa kupata jibu je ni kwamba hawa jamaa wana niiga Mimi au na wao uchumi umewapiga kama Mimi?
Kati yao kumi ni mmoja ndio Nina uhakika kwa asilimia mia kwamba amewahamishia watoto wake Kayumba kwa sababu ya kunigeza Mimi au at least kuwa inspired na Mimi.
Niliambiwa na mtu kwamba huyu jamaa aliwahi kusikika bar akiwaambia watu anawarudisha watoto wake Kayumba kwa sababu uchumi umekuwa mgumu. Akasema " Kama ( jina langu) nimewarudisha watoto wangu Kayumba yeye ni nani asiwarudishe?
Ni hivi hapo mtaani kwetu ( uswahilini) Mimi ninachukuliwa kama kijana mwenye uwezo kifedha.
Ila ukweli ninaujua Mimi mwenyewe ninapitia kipindi kigumu kiuchumi.. Ndio maana niliamua kuwarudisha watoto wangu shule ya Kayumba.
Mimi kuwarudisha watoto wangu Kayumba ilikuwa ni habari iliyo enea mtaa mzima..
Najua baadhi ya watu watakuwa wamefurahi kwa sababu kwao hilo linamaanisha anguko langu..
Hata hivyo leo nimekuja kugundua kwamba, Kumbe ni watu wengi tu hapo mtaani ambao walikuwa wanasomesha watoto wao English Medium walikuwa wanaumia kimya kimya ila walikuwa hawajui cha kufanya kwa sababu walikuwa wana ogopa macho na maneno ya watu ndio maana wengi wao walikuwa wanaishi kwa stress ilimradi ionekane watoto wao wanasoma English Mediums.
Nilipo watoa watoto wangu English Medium.na kuwaleta Kayumba, wazazi wengi wamefuata njia, now wanawatoa watoto wao English Mediums na kuwaleta Kayumba..
Nilicho kigundua kuhusu watanzania wengi ni kwamba wengi wanafanya mambo kwa ajili ya kujionyesha kwa watu. Kwa ajili ya approval and validation from other people.
Kwako ewe Mtanzania. Fanya kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Ishi maisha yako halisi usiishi kuwa impress watu.