NIlichojifunza: Serikali Vs Upinzani na Media

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
Serikali ina utajiri wa technical team, aidha wanaamini katika chama tawala au hawaamini, lakini wako ndani ya serikali ya Chama cha Mapinduzi. Wote hawa wako busy wakifanya makuu, huku wakiwa na mda mchache sana wakuelezea makubwa na mafanikio waliyoyafikia. Serikali hii inafanya na imefanya maajabu mengi sana, ila haijui kujipigia debe.

Vyama vya Upinzani ukilinganisha na CCM, hawana utajiri mkubwa wa wataalamu walio chini yao moja kwa moja, kiutendaji moja kwa moja, labda tu wako wafuasi wa vyama vya upinzani wanaofanya kazi chini ya serikali ya CCM. Ila vina muda mwingi sana wa kupiga kelele, kukosoa, na hata kuongea hovyo kuhusu Serikali, wakiwekeza udhaifu wa Serikali katika kujitangaza na kuelezea manufaa waliyofikia.

Ushauri, Serikali iufumue mfumo wake wa vyombo vya habari.

Wawatumie Vijana kuiuza serikali na kutangaza mafanikio yake, iachane na mfumo wa kizamani wa namna ya kueleza mafanikio.

TBC kwa ujumla ilikuwa ya Tido Mhando, sio hii ya sasa, imepoteza umaarufu. TBC ya Tido Mhando ilieleimisha umma historia, maendeleo na mafanikio ya nchi, vijana wengi walianza kuipenda nchi yao na kuimarisha uzalendo wao. TBC isiwe ya kuelekezwa na Wazeee tu, bali iweze kuwafikia watu wa rika zote.

TBC1 iimarishwe iwe na speed na news coverage moto sio slow kama ilivyo sasa, kiwango kiwe cha kimataifa, ikiwezekana Afrik Mashariki muwe wa kutegemewa. Watangazaji wazee mkubali kuwa mageuzi ni ya lazima ndani ya TBC.

TBC2 ndio kabisa, sijui mnafanya kitu gani unique mnachoweza kuzidi Clouds au EFM? TBC2 ingeweza kutumika vizuri sana kuchanganya burudaninna elimu, mfano documentary muhimu za kizalendo hazipo tena, na za kuelimisha watoto wetu hawataziona tena.

Ingawa chombo hicho kinatakiwa kutambua wajibu wake kama chombo cha Srikali, bado kinatakiwa kifike mahali kisiwe chombo cha CCM, bali cha Serikali ya wanchi wote, na kiweze kuimarisha mtizamo wa jamii dhidi ya serikali, siuo kufanyia kazi mazoea.

Seirkali iongeze vitendea kazi na ijue umuhimu wa media zake na kuhakikisha zinaleta ushindani kama kipindi cha Tido Mhando. Kama uongozi hauonyeshi matumaini ubadilisheni na wafanyakazi wapelekeni huko mkoani leteni watu wenye fresh mind makao makuu.
 
Unamaanisha nini hasa,Radio Uhuru,Gazeti la Uhuru havitoshi kupiga propaganda?
Radio Uhuru na Gazeti ni vya Chama! Lazima viongee yao ya kisiasa wanayojisikia.

Chombo cha Serikali kinapaswa kiwe proffessional, stratergic na kikubalike na watu wote kama chombo cha Umma.
 
Back
Top Bottom