Nilichojifunza hong kong

nyembea

New Member
Oct 22, 2012
1
2
HONG KONG, ni sehemu ya China inayojitegemea na kujiendesha yenyewe. Ina bunge lake, mahakama na serikali yake. Mahakama za Hong Kong zinafanya kazi kwa uwazi mkubwa sana na hakuna rushwa iliyoripotiwa kwa zaidi ya miaka 30.

Hong Kong ina sarafu yake (dola ya Hong Kong). Lugha kuu ni Kichina na Kiingereza. Uchumi wa eneo hili ni imara na wenye kusimama imara daima.

Miundo mbinu yake hakika haina mfano wa kuigwa: barabara, reli (za kasi na za kawaida ziitwazo TRAM), bandari na kadhalika.

Elimu yake imejiweka kisawasawa na huduma za kijamii ni bora na za kuigwa.

Sheria mama ya Hong Kong inaitwa the Basic Law. Sheria zingine hutungwa na bunge lao. Sheria za China kuu hazitumiki Hong Kong.

Hong Kong inafanan kabisa na Zanzibar na Tanganyika. Ni wakati muafaka kwa Tanzania kuangalia jinsi China na Hong Kong zinaishi na kuhusiana ili kuepuka muungano usio na tija na wa kulindwa na bunduki kama huu.
 
Hujajifunza lolote basi......hebu soma historia na jiographia ya Hong Kong na kisha soma ya Zanzibar. BTW huko Hong Kong kuna uamsho?
 
Hivi ulienda kama mtalii au nani?Kama ni kama mtalii basi hizo taarifa zako ni sahihi.....:happy:
 
Wenzio tumeishi huko miaka kibao na hatujasema. Wewe kufika tu mara moja basi Makelele....

Hongera hata hivyo kwa kufika na kuturushia hayo uliyoyaona maana siwezi kusema umejifunza.

Huwezi kujifunza kwa muda mfupi maana inabidi au usome sana au ukae na wenyeji wengi wakupe story kamili.

China na Hong Kong ni story tofauti. Wao walikuwa nchi moja ila sisi hatujawahi kuwa nchi moja na Zanzibar.

Hakuna udini ambao umejaa Zanzibar na mwisho, Wa Hong Kong ni Wasomi na wameendelea na hivyo kuelewa kwao kuko juu zaidi ya hawa waliouwa kwa kudhani Sheik katekwa na POLISI kumbe kajificha tu na akajifichua. Huu upuuzi huwezi kuufanya HK. Kuna wale waliojifanya kukimbia eti China wataharibu nchi na wakaenda UK, Canada na USA. Ila Asia ilipopata tetemeko la uchumi, HK nayo ikakumbwa ila Mchina akaja na kusema "Mwanangu usiwe na wasiwasi, hela hizi hapa za kutosha." HK akapona na hana wasiwasi kabisa na tatizo la uchumi.

Kutoka hapo ndiyo watu wote waliokimbia wakaanza kurudi na kuona Hakunaga kama kuishi kwenye himaya ya CHINA.

Kwa sisi Zanzibar, tofauti na China ni kwamba Serikali ya Tanganyika ndiyo inataka muungano ila sisi Wa Tanganyika, tunauogopa huu muungano na mwenge kama ukoma. HATUTAKI MUUNGANO sisi.

SET ZANZIBAR FREE.

 
Last edited by a moderator:
hongkong.jpg


Mie sijafika nimejifunzia google, kukatika umeme kwao ni swala la historia,
hawakumbuki hata ni lini umeme ulikatika...
 
hongkong.jpg


Mie sijafika nimejifunzia google...

Dah!!wenzetu kwa kweli wanafurahia maisha kwa uzuri huu hawawezi kamwe kufikiria mambo ya kipuuzi kama udini...hivi kwa umeme unaotumika hapo pichani na vi megwati 800 vya ngeleja na sosipita vingewasha hata ghorofa moja hapo???baba mwanaasha ww nenda tu katalii sisi wala hatuhitaji haya maendeleo bhana....aaagh.
 
Back
Top Bottom