Nilichogundua baada ya msiba wa Regia

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,763
Zaidi ya marehemu Regia kuwa mwanachama wa jf, pia alikuwa mwanasiasa. Wa chama gani, hapa ndio penye uzito wa mada hii. Ni ukweli usiofichika kuwa Regia alipendwa na kukubalika ndani na nje ya jf. Na alikubalika zaidi baada ya kujianika kuwa yeye ni nani na ana nia gani. Sote tukajua kumbe yule (nani tena?) ndio Regia?! Harakati zikaanza na mwisho akawa mbunge, japo si ule ubunge aliotarajia.

Akawa anatoa michango yake humu kwa mujibu wa ilani ya chama chake cha cdm na kina sie tukawa tunamsapoti kwa hali na mali. Japo walikuja wadau wa ccm na kusema yale ya chama chao lakini bado waliishia kupondwa na makopo. Nnape mmojawapo. Jf ikawa na mapenzi na Regia na chama chake.

Tuliposikia taarifa za msiba wake jf yote (ukiacha kundi la wachache wanaojulikana) ikazizima kwa kutoamini kilichotokea. Mengi yakaandikwa kumhusu Regia lakini mengi zaidi kuhusu maisha yake ya kisiasa maana ndio tumemjua zaidi hapo. Jf ikapanga mikakati na namna ya kumuenzi huyu dada kwa yele yote aliyoyaanzisha akiwa na nia ya kuyatekeleza, mojawapo likiwa ni kukusanya maoni ya nini cdm iwafanyie wananchi.

Moja ya azimio la mkutano wa marafiki wa Regia ni kuendeleza aliyoyaacha na wanajf wengi wanakubali hili. Kwa lugha nyingine kuendeleza yale mawazo ya kutekeleza ilani ya cdm, na hii imekuwa na impact kubwa sana kwenye nafsi za watu. Ndipo katika kuwaza na kutafakari nikagundua kuwa jamii inataka mabadiliko ya kimfumo. Regia hakupendwa kama yeye tu bali alipendwa zaidi kama mwana chadema. Tafakari...
 
Hivi ukianzisha mada tu........... hiyo Ndovu Lager inajitokeza !?
Naomba ufafanuzi tafadhali
:A S embarassed:
 
Same shit, different day!

Kuendeleza ilani ya CDM kwenye serikali ipi? Unanchekesha!

Hivi mwaka mmoja wa ubunge wa offer kuna kipi cha maana ?

kabla ya kupost uwe unani pm unaniuliza mengine unajishushia hadhi

Mkuu mbona hicho ulichogundua atukioni?

kumbe mko wengi? Ila bado mpo wachache. Ngoja tuje


Unabahati mbaya mkuu! thread imevamiwa na viwavi faster faster kabla ya GT hata m1. pole sana!
 
Hebu tupe matokeo ya mkutano wa jana! Nasikia JF memberz walikuwa hawafiki 10. Kweli nimeamini Regia alikuwa anapendwa ndani na nje ya JF
 
Hebu tupe matokeo ya mkutano wa jana! Nasikia JF memberz walikuwa hawafiki 10. Kweli nimeamini Regia alikuwa anapendwa ndani na nje ya JF

Naamini wewe na watu wa aina yako huwa mnaandika/mnasema kwanza and then (maybe) mnafikiri baadae. Ok, assuming ulichosikia ni cha kweli kwa hiyo una conclude kwamba Regia (RIP) alikuwa na marafiki wachache? Hivi wanachama wa JF ambao ni marafiki zake wako located sehemu moja? Masaburi ya mbwa wangu yangetoa kitu cha maana zaidi ya upupu wako huu!
 
Naamini wewe na watu wa aina yako huwa mnaandika/mnasema kwanza and then (maybe) mnafikiri baadae. Ok, assuming ulichosikia ni cha kweli kwa hiyo una conclude kwamba Regia (RIP) alikuwa na marafiki wachache? Hivi wanachama wa JF ambao ni marafiki zake wako located sehemu moja? Masaburi ya mbwa wangu yangetoa kitu cha maana zaidi ya upupu wako huu!
Huwezi kuandika bila kutumia hayo maneno machafu? Au umeishiwa cha kuonge unajazia jazia?
Ninachoamini mimi 70% ya wana JF ni wakazi wa DSM! Chakushangaza jana waliokuwepo ni wana familia tu na memberz pungufu ya 10, pamoja na promo yote iliyofanywa!

Apumzike kwa amani dada yetu Regia..maisha yanaenelea kama kawaidia!
 
Back
Top Bottom