Niko kwenye Jeshi la akiba la wanajeshi wa Tanzania, Utaninyimaje haki ya uraia EX-POLICE wako?

Unatuambia wote tuweke picha zetu tukiwa tunalitumikia taifa?

Nyinyi ndio mnadhalilisha watz walioko nje na kuonekana malimbukeni wasiojua tz ipo wapi na inakwenda wapi?

Umeanza tabia ya William Malecela? Ishi utumwani kwa heshima bila kubughudhi wanaolijenga taifa, subiri tukomboe nchi kisha tutakukaribisha urudi Kikombo kwa Baba yako Mzazi Mzee Gustaulo Lukosi, hali yake kimaisha bado ni mbovu hasa akikumbuka kuwa katika maisha yake alizaa jitu kama wewe na anasikia upo mzima unashinda mitandaoni kuwatusi watz.
 
mimi naona ntaumwa baadae....nafikiria kuongea na wakili wangu amshauri chris tuandamane dhidi ya serekali dhalimu ya ma intarahamwe ccm hadi watupe uraia pacha...Chris umeona hasara ya elimu ndogo kuongoza elimu kubwa??

Chriss ni mkereketwa wa chama cha kijani. CCM kwake hawana baya
 
Ndugu zanguni,

Leo nimeamka asubuhi na kuangalia kwa makini cheti changu cha kuhitimu mafunzo ya upolisi nilichokipata mwaka 1991 kule CCP moshi.

Katka mafunzo yote, mimi pia nilipitia field craft (mafunzo ya kivita) ambapo nilipewa ujuzi wa kuweza kupambana nikiwa mstari wa mbele hata pale risasi zikiniishia nilifundishwa namna ya kupambana nikiwa na singe tu. Pia nilijifunza kutumia silaha zote zilizokuwepo wakati huo kwenye majeshi ya Tanzania, kuanzia SAR, UZI, SMG(AK47), LMG, RPG, mpaka mizinga mikubwa kama recoiless na ile ivutwayo na magari.

Baada ya kumaliza mafunzo tulikula kiapo cha utii na uaminifu kwa wanajeshi wa Tanzania. Ambapo katika hicho kiapo tunaapa kuwa watiifu kwa amiri jeshi mkuu na kuilinda nchi yetu wakati wote na mahala popote wakati wote wa uhai wetu. Kwa kula kiapo hicho ina maana hata kama nimeacha kazi au nimestaafu, ikitokea dharura nitaitwa mara moja kazini...

Hii ni kuwajulisha tu kuwa kama Malawi au Rwanda wakileta za kuleta basi mimi nitakuwa mmoja kati ya wanajeshi wengi tu ambao wako reserve tutakaokwenda kuripoti mara moja kwenye kambi yoyote ya jeshi la wananchi iliyokaribu nami na kukabidhiwa Bunduki yangu, kombati, kibuyu cha maji na begi lililojaa basic needs za mwanajeshi akiwa front line.

Sasa leo unasikia watu wanatukejeli sisi Diaspora kuwa hatuna sababu ya kupewa haki ya uraia wakati wao hata hawajawahi kulifanyia lolote tafa lao zaidi ya kulihujumu kila kukicha.

Ningependa kuwauliza wale wote wanaotubeza na kutulaumu kwa nini tulichukua uraia mwingine, Mimi wakati niko bongo baada ya kuacha kazi jeshi la polisi ambalo lilikuwa linalipa mshahara duni miaka hiyo mlitaka nifanye kazi gani? Nilijaribu kutafuta kazi kila sehemu nikawa sipati kwa sababu sikuwa na ujuzi mwingine zaidi ya ujuzi wa kutumia silaha kali. Na kazi ambayo ningeweza kupata ilikuwa ni ulinzi tu kazi ambayo hata siku moja nisingeweza kuifanya, huwezi kutoka polisi ukaenda kuwa korokoroni hiyo ni kujidhalilisha.

KWA HIYO MLITAKA UJUZI WA KUBEBA BUNDUKI NIUTUMIE KWENYE UJAMBAZI AU?

Ni wakati sasa mtusikilize..

https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=-KQ4zoyitWo#t=0

_44511344_d27792fe-178d-4b7b-98c4-b1c9d34c88f0.jpg
Lukosi, kwamwene bee. unajua tatizo ambalo mimi sielewi ni kwanini mnang'ang'ania sana uraia wa nchi mbili ili muwe watz na wa huko mlikopata uraia mpya kwa kuikana Tanzania (kuisaliti kabisa Tanzania mchana kweupe). hivi, ni kwamba mnajuta kuukana utz sasa mnahangaika kurudi muwe raia kama wengine, au vipi, siwaelewi. ninyi kwamfano wewe mwalukosi si muingereza wewe, shida iko wpai hapo? unapungukiwa nini? kwasababu hauna passport ya tz? si uukane tena huo uingereza ili upate utz ili ufurahie utz? hivi mnajua mlifanya kitu kibaya sana kuisaliti tz? halafu kwanini sisi watz tunaoipenda tz yetu hata kama kuna umasikini tunapigana hivyohivyo kwanini tupoteze muda wetu kuwafikiria ninyi maforeigner badala ya kufanya mambo mengi ya muhimu yanayoisaidia nchi yetu?why should we trust you kwamba mkiwa na passport mbili hata tatu mtakuwa sio wasaliti kwa watz, wewe hapo kama ni muingereza una haki zote kama muingereza utashindwaje kuisaliti tz kwaajili ya uingereza kama mlivyoisaliti mara ya kwanza mlipoikana mbele ya wazungu kwamba hamtaki kamwe kuwa watz tena? au kwasababu unatuma vihela vichache kwa ndugu zenu hapa au wewe unatuma kule iringa ili ndugu zako wawe na hela ya kununua kuku wale wasile mbwa kama walivyozoea wahehe? na je? do you think you are that important to Tanzania hata tuwafikirie na kupoteza muda kuwadiscuss?
 
kama wewe lukosi ulishaenda hadi chuo cha polisi kule moshi na ukapiti amafunzo ya jeshi na bado ukaisaliti tz kwa kuikana, ulijifunza nini huko sasa na mafunzo hayo yalikusaidia nini? mnajuta kuikana tz na sasa mle matunda yake.
 
Chris Lukosi nadhani mlifundishwa uzalendo kama first priority subject. Hata hivyo sasa hivi uandikapo thread hii kuna mchakato wa katiba mpya ambayo itakuja na jibu la suala lako

Ahsante kwa kuendelea kuipenda nchi yako ya kuzaliwa, ndio uzalendo

Mzalendo gani anakimbia nchi kisa mshahara mdogo jeshini? Ataweza kupigana front line kama si mvumilivu kiasi hicho?
 
Last edited by a moderator:
Tuwaamini vipi nyie mlioikana nchi yenu kisa mishahara midogo? je wakulima pia wakiukana utanzania kisa bei duni ya mazao yao kutakua na nchi? njooni tu kama watalii kutusalimia
 
Tuacheni unafiki. Hata sisi hapa mjini siyo kwetu. Wazazi wetu walikimbilia mjini kutafuta maisha. Kama wa diaspora ni wasaliti, basi hata sisi ambao hatuna asili za kizaramo hapa mjini pia ni wasaliti. Maana tumeikimbia mikoa yetu na vijiji vyetu na tusiitwe tena wachaga, wanyakyusa, wahaya n.k.
 
Back
Top Bottom