Mjibu kila kitu hapana...
Angalia atakavyo react... Halafu ni PM nikufahamishe nini cha kufanya
after that...
"Mh!"Sasa tatizo liko wapi hapo?? Mbona una complicate mambo madogo tuu hayo.. Kinachokufanya uchukie muda wote huo ni nini? Huwezi kusema majibu anayo..Wewe ndie mwenye majibu yote hayo.. Mjibu mpenzi wako hayo maswali maana najua hakukurupuka kukuuliza hayo..! Wanawake tunapenda kuhakikishiwa kila siku kama tunapendwa na tutaolewa.. Upo hapo???
"Mh!"
wanawake huwa mnakua tayari mna alternative,hivyo unataka uhakikishiwe ili uchague<wakati kwa mwanaume huwa anahitaji muda zaidi wa kuwa na uhakika na mtu atakemuoa.sasa huo mvutano ndio huwa unaleta shida.lakini nyie wanawake ni wakorofi kwasababu huwa mnalazimisha sana majibu hata kwa muda ambao sio muafaka.
Jamani hivi watu wengine wameumbwaje? mbona mambo madogo unacomplicate kiasi hicho!?kitu kidogo unakikuza kosa lake ni lipi?Kwani ungemjibu hayo maswali ungepungukiwa nini? Mwanaume hawi hivyo bana khaaaa!:flypig:
nimeona niombe ushauri wenu wa dhati kuhusu hili;
nina mpenzi wangu ambaye anajua nampenda sana nami vilevile nampenda sana.
kisa ni hiki kifuatacho:-
siku moja ndani ya mwezi wa june, mpenzi wangu alinipigia simu usiku na kwa bahati mbaya sikupokea simu yake kwa sababu nilikuwa nimelala hivyo baada ya muda mfupi akatuma sms iliyokuwa na maswali kibao na magumu ambayo sikuweza kupata majibu ya haraka haraka kama alivyotaka nimjibu na hili ndo limenipelekea kuomba ushauri toka kwenu. Message hiyo ilisomeka kama ifuatavyo:-
naomba unijibu kwa ufasaha kutoka moyoni mwako
meseji hii ilileta shida na mpaka sasa tuko katika mgogoro mkali sana maana mimi nilireact kwa nini asiniulize nini kimesababisha nisipokee simu yake yeye akaniuliza maswali ambayo majibu yake anayo???
- je uko tayari na umeridhika kuwa nami kama mkeo mtarajiwa?
- unanipenda kweli?
- uko tayari kunioa?
- haunidanganyi?
- umenipenda jinsi nilivyo pamoja na udhaifu nilio nao? Please naomba majibu
Nawaombeni mnisaidie ili tuondoe kutokuelewana tulikonako.
Usifanye inshu kuwa simple kiasi hicho kaka. Kama ndivyo kwa nini aniulize baada ya kunipigia sikupokea????