saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,258
- 6,222
Juzi alikuja rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kutembelea nchi yetu kwa siku 3, wakati huo huo mfalme wa Uingereza Charles wa III aliitembelea nchi ya Kenya.
Ukilinganisha mapokezi unaona Rais wetu kama ni mwoga hana muda hata wa kuchat na mgeni wake, vile vikundi vya ngoma ni km havina kazi. Rais anamkimbiza mgeni wakati unaona kabisa mgeni angependa aangalie zile ngoma akipitia kila kikundi, nilitegemea rais wetu angempa muda wa kutosha na kumwelezea hata maana ya zile nyimbo. Tatizo letu ni nini, ni lugha?
Kama ndio kwanini ikulu isimpatie Rais course maalum na humo humo wamfundishe na communication skills. Hatujui hata hospitality (ukarimu wa kumpokea mgeni), rais hana confidence(hajiamini) kwanini. Rais na amiri jeshi mkuu kwanini usijiamini ndani ya Taifa lako, ongea na mgeni naye ajisikie yuko nyumbani siyo kumburuza na kuonesha uwoga usioeleweka.
Nenda katazame mapokezi ya Kenya, mfalme anapewa muda anaongea na wenyeji anapewa muda wa kutosha, hazongwizongwi na watu wa ulinzi. Jioni walikaa very friendly kwenye dhifa ya kitaifa muda wa kutosha. Leo alienda pwani ya Kenya, Mombasa kwenye beach(ufukwe) unaitwa Nyali, kaangalieni alikaa muda wa kutosha anaongea na watu vijana wa kawaida kabisa wa Kenya taratibu bila hofu, huwaoni hata walinzi wake.
Kuna maonesho madogo yaliwekwa pale, alikuwa anatembelea kila kimoja baada ya nyingine akiongea na wahusika vijana wadogo wamzingira wanamsindikiza bila woga wala hofu. Bila shaka yule mflame alifurahia ile hali na yale mazingira mazuri na mapokezi mazuri ya watu wanaojiamini, wanajieleza, wanaelezea maonesho yao.
Ingekuwa kwetu angezongwa na walinzii na kuburuzwa haraka haraka. Tatizo letu ni nini mpaka tujiamini? Ni lugha? Hata mlioko ikulu hamuwezi kwenda kujiongeza? Hebu saidieni nchi mkiwa kwenye hizo nafasi