Nikilima Soko vipi? Unalima soko lipo? Tuliambiawa tuanzie sokoni.

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,917
Ukikutana na wale wafundisha ujasiriamali utasikia anzia sokoni tafuta soko ukisha pata sasa nenda shambani kalimie.

Unakuta sasa wakulima tunaogopa sana kulima baadhi ya mazao kwa sababu hatuoini soko,hatuioni ikiuzwa pemheni ya barabara na hapa ndio tunajikuta asililimia 98 tunalima traditional crops, yaani vitu vinavyo fanana, tukiambia tutaje mazao ya kulima theni tupewe mtaji asililimia 98 hadi 100 tutataja vitu vinavyo fanana.

Turudi kwenye Soko liko wapi,Kwanza tukubaliane kwamba kinacho anza ni products na baadae kuanza kutafuta wanunuzi.Hainzi soko na baadae products.

Mfano,Bagharesa anazalisha juice ya Embe na Pera sijui na nini vile,tuchukulie anazalisha juice ya mapera wewe unataka au una mpango wa kulima Mapera kwa ajili ya juice unamfuata Azam na kuwaomba kikao ili uwaulize kama ukilima Mapera watanunua, Ukweli ni kwamba hawatakupokea na huwezi pewa kikao kabisa, Ila ukaenda kwa Azam na Sample ya Mapera yako na ukawaomba kikao hapo mnaweza kaaa mkaongea biashara sasa.

Hakuna mnunuaji atakupa soko bila sample, bila kujiridhisha na products yako,ndio maana hata huko nje huwa watu wanatuma sample za Products kwanza ili kushawishi wateja.

Unapo pima soko mfano soko la ndani,Tafuta hata Sample ambayo sio yako ili kupima mwitikio au kuona upepo. Mfano unataka kuzalisha Mayai ya Bata kwa ajili ya kuuza,hata kama hujaanza kufuga tafuta Mayai sehemu paki vizuri nenda nayo kwenye Market kwenye Super market kubwa,Mahoteli makubwa waonyeshe na waambie ni products yako,Usikie muitikio wao.

Kama ni nyama ya Bata tafuta Bata Chinja vyema nenda na sample kwa wateja na waambie hii ni products yako unafuga,Hata kama ukweli ni kwamba hujaanza kufuga.

Unashamba lako unataka kuanza kulima aina fulani ya zao, una wasiwasi na soko,tafuta Sample ya hilo zao hata kama utaagiza nje ilimuladi iwe ndio aina unayo taka kulima nenda nayo kwa wateja.

Kuna wakati na jamaa angu tulikuwa tunataka kuzalisha Strawberry,Sasa hatuna products lakini, na mbegu tulikuwa tuagieze Kenya,tulicho fanya tukaagiza Matunda ya strawberry kutoke Kenya tukawa tunaenda nayo kwa wateja kuwaonyesha na kweli tukawa tunapata oda na wengine kutuambia wiki ijayo au kesho tupeleleke mzigo,sasa mzigo hatuna,tulicho kuwa tunafanya tulikuwa tunaacha fake number.Ila kutoka pale tunakuwa tusha pata picha ya soko kabisa.

Hakuna mnunuzi atakupa soko bila kuona unacho zalisha.

Swala kwamba anzia sokoni kabla ya kuzalisha sio kweli,ni lazima huko sokoni uende na sample kwanza.Kwenye Hoteli za kitalii hata mayai wanataka upeleke sample kwanza wayapasue pasue waangalie ndio waone kama yana kidhi viwango.
 
Ahsante, umefahamika vyema.

Unachokisema kipo hata katika biashara nyengimezo za uzalisaji, ni lazima uwe na products ndio utafate soko, walau kwa kuanza kuzalisha kidogo kujaribu, ili kupima upepo.
Lakini ni jambo linalohitaji uthubutu.
 
Ahsante, umefahamika vyema.

Unachokisema kipo hata katika biashara nyengimezo za uzalisaji, ni lazima uwe na products ndio utafate soko, walau kwa kuanza kuzalisha kidogo kujaribu, ili kupima upepo.
Lakini ni jambo linalohitaji uthubutu.
Kabisa mkuu
 
vipi kuhusu masoko ya bei za jumla yan kwa mfano naitaji kuuza magunia 40 ya mpunga nauzia wap ?
 
Back
Top Bottom