Nikiandikiwa Notification barabarani nataka kuappeal naenda wapi

Wandugu habari za leo nilikuwa nataka kujua kama nimeandikiwa notification kwa makosa ya barabarani na sijakubaliana nayo naenda wapi ili kuappeal. Maana naona kuna makosa mengine siku hizi unaandikiwa tu nilikuwa nataka kujua kisheria raia wakawaida kama mimi anaweza kufanya nini ndani ya sheria. Msaada wenu wataalamu ni muhimu

Nasimama pembeni hapa kusubiri majibu ya waungwana maana hata Mimi niliwahi kukumbwa na kadhia hiyo.
Alinipa Kifurushi nikalipe, lakini nilimbana kwa Maswali aniambie hasa kosa langu lipi mpaka aniandikie adhabu alishindwa kutoa jibu la kuridhisha.
Mwisho kwa nguvu ya Sare na nembo ya neno Polisi mwanamama yule akaniandikia nikalipe, sikutia neno lakini nilijua nilimshinda kwa hoja.
 
Wataalamu tunaomba msaada mbona kimya mada muhimu hii kwenye maisha yetu ya kila siku
 
Nenda kwenye kituo cha askari aliyekukamata, omba kukutana na OC Traffic, mweleze yaliyokusibu, usiporidhika na atakayokwambia, omba kuonana na OCD, naamini muafaka utapatikana. -
 
Wandugu habari za leo nilikuwa nataka kujua kama nimeandikiwa notification kwa makosa ya barabarani na sijakubaliana nayo naenda wapi ili kuappeal. Maana naona kuna makosa mengine siku hizi unaandikiwa tu nilikuwa nataka kujua kisheria raia wakawaida kama mimi anaweza kufanya nini ndani ya sheria. Msaada wenu wataalamu ni muhimu
Hiyo notification ukiisoma ina sehemu mbili ambapo unatakiwa kusaini sehemu moja, kama unakubali makosa uliyoandikiwa unasaini mahali panapoonesha kukubali makosa na kama unakataa kuna sehemu ya kuonesha hivyo. Ukikataa maana yake ni kuwa polisi watakupeleka mahakamani ili wathibitishe makosa hayo (na hiyo nadhani itakuwa ndio hiyo rufaa kama unavyoiita)
Hivyo sehemu pekee ya kupinga notification ni mahakamani. Saini ile sehemu ya kukataa makosa
 
Ndugu kwa Dar sasa hakuna hiyo anaweka namba kwenye machine inatoa notification ambayo unatakiwa kuilipa ndani ya wiki ndio nilikuwa nauliza kama ukubalini nayo unaenda wapi kupinga maana inachukuliwa tu kama umekubali ukisema hujakubaliana jaamaa anaandika anakupa risiti ya wewe kwenda kulipia, Zamani ilikuwa na mahali unakubali au kukataa kwa Dar hiyo option haipo

Hiyo notification ukiisoma ina sehemu mbili ambapo unatakiwa kusaini sehemu moja, kama unakubali makosa uliyoandikiwa unasaini mahali panapoonesha kukubali makosa na kama unakataa kuna sehemu ya kuonesha hivyo. Ukikataa maana yake ni kuwa polisi watakupeleka mahakamani ili wathibitishe makosa hayo (na hiyo nadhani itakuwa ndio hiyo rufaa kama unavyoiita)
Hivyo sehemu pekee ya kupinga notification ni mahakamani. Saini ile sehemu ya kukataa makosa
 
Hapo ni kulipa tu kama kakuonea Mungu atamlipa ukisema uende uko unakoenda utazunguka utajikuta unaghalamika mqra 2 na mda ushapoteza
 
Back
Top Bottom