Nikajiingiza MSALANI...

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,181
409
Ilikuwa mwaka 2008 kipindi hicho nilikuwa naendesha lory ya mizigo almaarufu kama FUSO.,
Basi sikuhyo tulikuwa tunatoka maeneo ya mufindi iringa kuchukua mbao tupeleke Dar...

Tukiwa njiani tunarudi, nyuma ya gari naloendesha kulikuwa na Randlover ya jeshi ikiomba nafasi wapate kupita, na walionekana wanaharaka kwavile walitufikia wakiwa na kasi ya ajabu, lakini kutokana na barabara kuwa mbaya ilikuwa inaruhusu kupishana gari mbili kwa shida kidogo.

Basi tukashauriana tusiwapishe hivo nikawa nachezesha gari kila upande watakao taka kupita, " piteni juu " walisema makuli waliokuwa kwenye lory yetu, bilakujua kuwa jamaa wamekasirika kiasi gani tukaendelea na safari kwa mtindo huo.

Mbele kama kilomita kumi gari yetu ikapata pancha tairi ya mbele na kutulazimu kusimama, bila hiyana wajeda nao wakasimama na kututaka tupande kwenye gariyao, ilikuwa majira ya saa 7 mchana, walitupeleka kambini nakutuweka juani mpaka saa9 alasiri, kisha wakatupatia soda cocacola kilammoja, tulipomaliza tukaletewa ndoo mbilimbili za maji na kuamriwa kwakutumia vizibo vya soda tuzokunywa tujaze maji zile ndoo ndio itakuwa pona yetu, duuh tulikesha mpaka keshoyake saa5usiku, nalijuta mbona, mpaka leo nikiona magari yawale jamaa huwa nawapisha hatakama wako mbali, sidhani kama ntarudia ile mchezo....

Nyc sunday to all jf members...
 
Teh teh jamaa nomaa....
Mi mwezi uliopita nikiwa kigoma tukapanga na jamaa zangu twende Manyovu kutembea...wakati tuko njiani tukavutiwa na mabonde na milima...tukaamua kusimama tupige picha..
Lol kumbe tuliko park gari opposite ni kambi ya jeshi..na jamaa walikuwa wamesimana kwa nje ila tukajua wanangoja usafiri...wakatuacha tukapiga picha hadi tukamaliza...tulipokuwa tunarudi kwenye gari ndo wakatufuata wakatupeleka ndani na gari letu...
Lol yalitotukuta humo nomaaaa
 
hawa jamaa huwa sijui wakoje....visa vyao ni vingi sana....vya mateso kwa raia....
 
kuna mlevi mmoja wa pale savey alivamia kambi ya jehi ya makongo anauza miguu ya kuku.
Ilikuwa mwaka 2005, jamani kuanzia siku hiyo pombe zake zinatambua wajeda.

Walimpa kama sufuria la kilo 5 amalize peke yake akashindwa. Imagine mtu kalewa analazimishwa aruke kichura chura, hana hamu.
 
afu mwaka 1996,walipita uwanja wa mazoezi ya mpira wa miguu wa mtaani kwetu.

Vijana wa mazoezi wakawazomea na kukata fujo kiasi, wajeda walikuwa 2. Baada ya kama nusu saa likaja karandinga limejaa, hapo ndo nilijua hao watu wamepinda.

Walipiga karibu mtaa mzima, wake kwa waume, vijana, watoto kwa wazee, hata mimba ikizubaa inapigwa.

Yaani, mie hata huwa siwaelewi wanawaza nini.
 
afu mwaka 1996,walipita uwanja wa mazoezi ya mpira wa miguu wa mtaani kwetu.

Vijana wa mazoezi wakawazomea na kukata fujo kiasi, wajeda walikuwa 2. Baada ya kama nusu saa likaja karandinga limejaa, hapo ndo nilijua hao watu wamepinda.

Walipiga karibu mtaa mzima, wake kwa waume, vijana, watoto kwa wazee, hata mimba ikizubaa inapigwa.

Yaani, mie hata huwa siwaelewi wanawaza nini.

Wale jamaa nawaogopa mpaka leo,
 
Back
Top Bottom