Nifikishieni Salam kwa KAKA Mkubwa!!

dguyana

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
423
110
Kaka, Ulisema hari mpya nguvu mpya na kasi mpya kaka, kwetu ni bala kasi yako hatuiwezi. Kaka kasi yako ni kali mno nadhani zaidi ya speed 220Km/H.

Kaka ulisema hali ya maisha itakuwa good kwa vijana na ile ahadi ya ajira 1m kwa mwaka. Hilo ni balaa yaani umetugeuka hata hizi ajira 40 kwa mwaka nazo unakaba? Kaka kufika 55yrs ni balaa. Sheria ndio inataka hivyo ila kwanini msituandae na kutushirikisha wafanyakazi wenyewe? Kwani zile hela zenu kaka?

Kaka hivi ni kweli huijui Richmond mbona we ndo kila kitu hapa bongo. Ukiamua hata mimi nisiende toilet kweli naweza nisiende ndani ya mins tu. Tuambie basi wale ni kina nani vile?

Vipi kuhusu wale mafisadi na siku 90 mulizowapa? Wadogo zenu tunasubiria kuona action mpaka leo picha halinogi. Hafi Jambazi kuu wala steringi picha la kihindi afadhali. Kule migodini mbona hali ni Mbaya sana wakati kila siku ndege zinakwenda south direct kutoka migodini. Kusoma sijui kabisa ila pale nadhani picha naiona kwani mungu kanijaalia macho.

Ile mikataba ya gesi mbona tunaisikia juu juu tu. Sio Richmond nyingine kweli? Mbona hatuwekani wazi jamani wakati sisi ndugu mmoja?
Kaka watu wanapiga si mchezo. Eti wanasema we dhaifu hata ukigundua utawachekea na kuwahamisha vituo. Huku TRA ni balaa hela mbele rushwa kama kanuni. Kule THA ndio kabisa, tunauza magari yetu pale pale port. Halmashauri ndio kabisa hata mawizarani ndio usiseme.

Nadhani yapo mengi ila kaka BIBI yangu na Shangazi hapa kwetu Pangani wanashukuru mungu kwa kuwapatia mti wa mhogo kuliko WEWE kaka. Yaani asubuhi uji wa muhogo na muhogo, saa kumi na mbili ni ugali wa muhogo na kisamvu cha chumvi hio ndio mpaka kesho tena. Msaidie basi kidogo japo ale maharage? Ila bibi anakumbuka kuwa alikupa KURA yake na sasa analaani kwani hata kwenda mjini hawezi tena nauli hana. Sio kama anafanya kazi hapana ila ungempatia ile VOUCHER ya mbolea akalima kidogo ingemsaidia. Sasa zile voucher washkaji zako wamepiga na msemo wao kuwa huwezi kuwafanya lolote wewe ni DHAIFU…

My Take:-Najua hupitagi hapa JF ila najua wewe rafiki yake unaesoma hii kitu utamwelekeza japo kidogo aachie maana tait mno.
 
Hata kama ye hapiti nadhani hata Ritz au zomba watamfikishia ujumbe
 
...... WEWE kaka. Yaani asubuhi uji wa muhogo na muhogo, saa kumi na mbili ni ugali wa muhogo na kisamvu cha chumvi hio ndio mpaka kesho tena. Msaidie basi kidogo......
Kaka hapo kwenye red..ndo maisha bora kwa kila Mtanzania
 
bora TRA waendelee na rushwa maana ah kuliko kulipia leseni laki 2 jamaa hao wakipita unawapa 60000 wanakaa kimya sasa huoni TRA wanatusaidia na sie wananchi, wanatuonea huruma kua kuliko utoe 100% kwenye kodi wewe ukimpa 40% anakuachia wote tunakua tumepata...hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania tuliyoambiwa...
 
Juzi nilifika TRA customs pale kutoa kakifurushi kadogo kutoka nje ya nchi. Cost yake ilikuwa 600,000/= ila jamaa akaniambia kaka embu fanya 50,000/= bila risiti mi nimechoka kwenda posta kukakua mizigo. DU sasa tukiwa watu kumi kwa siku inakuwaje? Ila ni kweli bora hawa kuliko wale wanaoweka sheria za PAYEE kubwa na sasa NSSF/PPF wanakula mazima.
 
jiunge katika vikundi au SACCOS ili ujumuike na wenzako muweze kupata mikopo ujiletee maendeleo.

hii tabia ya kulalamika na kuishia kulaumu haitusaidii kama taifa.
 
CCM.jpg

Hii hapa
 
:biggrin1: duh huyo jamaa anaweza kua anapata laki 5 kwa siku kwa style hiyo.. mi naonaga ni bora hela yangu nimpe mwananchi mwenzangu(mfanyakazi wa tra) itamsaidia na yeye kulipia watoto wake shule kuliko kupeleka hela serikalini alafu hizo hela ndio wanazitumia kulipia posho wabunge watoro na safari zisizokua za lazima za Rais
 
jiunge katika vikundi au SACCOS ili ujumuike na wenzako muweze kupata mikopo ujiletee maendeleo.

hii tabia ya kulalamika na kuishia kulaumu haitusaidii kama taifa.

SACCOS hizo hela za kuweka huko wanatoa wapi
Na mwananchi ambaye kula yake tuu ni tabu mbolea ya kulimia voucher wamechukua wakubwa hata hiyo ya kuchangia kwenye saccos ataipata wapi
kwani umeambiwa saccos ni bure kujiunga au hakuna kiingilio na michango kukuza mtaji wa hiyo saccos
Sasa kama anakosa 1000 ya unga wa mahindi na mia tano ya kununua maharage hata ale ugali wa maharage ya kuchemsha hiyo ya kiingilio na mchango wa saccos atapata wapi
 
Kaka mwenyewe unaemwambia mbona ana earphones masikioni anakula music wa 50 cent, sidhani kama anakusikia
 
jiunge katika vikundi au SACCOS ili ujumuike na wenzako muweze kupata mikopo ujiletee maendeleo.

hii tabia ya kulalamika na kuishia kulaumu haitusaidii kama taifa.

Inawezekana ukawa wewe ndie kaka yangu. Hiyo mifuko uliyoeweka mbona kama mmewekeana? Wanaochukua pesa za maana ni hao hao kaka wakubwa. Nipe mfano wa mtu yeyote ambaye hizo SACCOS zimemsaidia ambaye leo hii hajaadhirika na mwenendo wa nchi yako?

Unakopa unafungua genge la nyanya nani atakuja kununua? Mi namashaka na wewe.
 
Mkuu ukifungua genge la kuuzia nyanya askari mgambo wa city na manispaa zetu wanakuja wanamwaga kisa eti unafanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa ukiwauliza yaliyoruhusiwa ni yepi utaishia kupata mkong'oto
Na wengine hata vile vitu vyako wanamwaga kwenye vyombo vyao wanapeleka kwao eti kisa wamekukamata ukifanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa
Mikopo ya kaka mkubwa ilienda kwa wale wenye majina na sauti
Sasa wewe mlalahoi huna jina wala hufahamiki nani akupe mkopo
Ukienda kukopa hata saccos unaambiwa njoo na hati ya nyumba au kiwanja au wadhamini wenye mali isiyohamishika
Sasa huku kijijni kwangu nani mwenye hati wakati naishi kwenye kibanda cha nyasi
Na mali isiyohamishika ya huku kijijini ni ipi zaidi ya hiki kibanda changu cha tope na kuezekwa kwa nyasi
 
Haya yote 9. Ila Kaka anajua kweli anachokifanya ni shida na mbaya kwa TZ ya sasa? Au ndio bado anawasingizia washauri?
 
JK: Tumegundua mtandao wa kuuza binadamu

na Christopher Nyenyembe, Mbeya

amka2.gif

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa Tanzania kwa kushirikiana na nchi nyingine zimefanikiwa kugundua mtandao wa biashara haramu ya binadamu wanaosafirishwa kupitia mpaka wa Malawi kwenda nchi za Ulaya na kuuzwa kwa lengo la kupatiwa uraia na kazi.

Kikwete amedai kuwa kundi linalofanya biashara haramu ya binadamu limejikita kila nchi ambako huwapokea wananchi wa Ethiopia na Sudan Kusini na kuwapitisha kwenye njia za panya hadi Malawi.

Rais Kikwete alisema hayo juzi jioni Ikulu ndogo mjini hapa, alipokuwa akijibu baadhi ya maeneo ya taarifa ya mkoa huo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ikihusu kuongezeka kwa kundi la wahamiaji haramu wanaopita katika mkoa huo kila wakati na kunaswa.

Kandoro alisema tatizo hilo linazidi kukua siku hadi siku huku kukiwa na idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wanaonaswa mara kwa mara na idara ya uhamiaji wakisafirishwa ndani ya malori na kuvushwa kwenye mpaka wa Kasumulu kuelekea nchi jirani ya Malawi ambako huko nako upo mtandao unaowapokea.

Akiizungumzia hali hiyo kwa kina, Kikwete alisema kuwa mtandao huo si kwamba ni wa wahamiaji haramu tu isipokuwa umegundulika kuwa unafanya bishara haramu ya binadamu, na kwamba kila anayefanikiwa kumvusha mtu mmoja hulipwa kati ya dola 10 na kuendelea.

“Hii biashara si ndogo kama mnavyofikiri; inawahusu watu wazito na wenye fedha ambao wakifanikiwa kuwafikisha watu huko Marekani, wanapatiwa uraia wa kuishi na kutafutiwa kazi za kufanya.

“Tulipowahoji tuliowakamata Dodoma wanasema hapa Tanzania wanapita tu na sisi hatuwezi kuruhusu wapite, tukiruhusu tutakuwa tunapingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupiga vita biashara haramu ya binadamu,” alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo alisema kuwa idara ya usalama inafanya kazi kubwa ili kubaini mianya inayotumiwa na wafanyakazi wasiokuwa waaminifu walioko mipakani ambao nao kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na usafirishaji huo.

“Hivi ninapoongea na ninyi wengine wako hapa hapa wananisikiliza,wanapuuza ninachokisema kwa kuwa nao ni miongoni mwa watu wanaofanya biashara hiyo haramu.

“Hili tunalifanyia kazi na kama mna habari tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayefanya biashara hiyo hali iliyotusaidia kutambua kwa undani mtandao mzima,” alisema Kikwete.

Hata hivyo, Kikwete aliwaomba wananchi mipakani wasaidie kuwafichua watu wanaofanya biashara hizo na kuacha kuwapokea na kuwahifadhi watu wasiowajua majumbani mwao ili waweze kupata chochote kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Alisema kuwa umaskini kwa kiasi kikubwa unawafanya watu wafikie mahali pa kuuzana ili tu mtu apate dola 10 kwa siku na kusisitiza kuwa wale watakaobainika wakijihusisha na biashara haramu za binadamu wenzao watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili Tanzania isiwe nchi inayolaumiwa kwa kosa hilo.

Aliiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo chini ya Mwenyekiti wake, Kandoro, kuhakikisha kuwa inafanya kazi ya ziada ili kukomesha biashara hiyo hasa katika mipaka ya Kasumulu na Tunduma na kwamba serikali imechukua hatua ya kuondoa vizuizi vya barabarani kwa kuwa vilikuwa vikiwanufaisha zaidi watumishi wa umma waliopewa kazi hiyo na kushauri mbinu zaidi za kiintelijensia zitumike.

Chanzo: JK: Tumegundua mtandao wa kuuza binadamu

My take:
Inawezekanaje Rais wa nchi anatamka wazi kuwa hapo alipo wapo wahalifu wanamsikiliza na kupuuza juu ya uhalifu anaozungumzia na wahalifu hao wanaachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote. Mkuu wa nchi anapoongea maneno kama hayo anataka asaidiwe vipi ama anatoa ujumbe gani kwa wananchi ilhal vyombo vyote vya dola viko chini yake?. Kweli Tanzania tumekwisha labda ashuke malaika kuikoa nchi yetu!!

Kaka yako dhaifu wala hakuna haja ya kumshauri kitu, umeona kasaini kimya kimya mswaada wa sheria ya mafao ili kuwabana zaidi na sasa hata kisamvu hakitapatikana, bora tujiajiri
 
JK: Tumegundua mtandao wa kuuza binadamu

na Christopher Nyenyembe, Mbeya

amka2.gif

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa Tanzania kwa kushirikiana na nchi nyingine zimefanikiwa kugundua mtandao wa biashara haramu ya binadamu wanaosafirishwa kupitia mpaka wa Malawi kwenda nchi za Ulaya na kuuzwa kwa lengo la kupatiwa uraia na kazi.

Kikwete amedai kuwa kundi linalofanya biashara haramu ya binadamu limejikita kila nchi ambako huwapokea wananchi wa Ethiopia na Sudan Kusini na kuwapitisha kwenye njia za panya hadi Malawi.

Rais Kikwete alisema hayo juzi jioni Ikulu ndogo mjini hapa, alipokuwa akijibu baadhi ya maeneo ya taarifa ya mkoa huo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ikihusu kuongezeka kwa kundi la wahamiaji haramu wanaopita katika mkoa huo kila wakati na kunaswa.

Kandoro alisema tatizo hilo linazidi kukua siku hadi siku huku kukiwa na idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wanaonaswa mara kwa mara na idara ya uhamiaji wakisafirishwa ndani ya malori na kuvushwa kwenye mpaka wa Kasumulu kuelekea nchi jirani ya Malawi ambako huko nako upo mtandao unaowapokea.

Akiizungumzia hali hiyo kwa kina, Kikwete alisema kuwa mtandao huo si kwamba ni wa wahamiaji haramu tu isipokuwa umegundulika kuwa unafanya bishara haramu ya binadamu, na kwamba kila anayefanikiwa kumvusha mtu mmoja hulipwa kati ya dola 10 na kuendelea.

"Hii biashara si ndogo kama mnavyofikiri; inawahusu watu wazito na wenye fedha ambao wakifanikiwa kuwafikisha watu huko Marekani, wanapatiwa uraia wa kuishi na kutafutiwa kazi za kufanya.

"Tulipowahoji tuliowakamata Dodoma wanasema hapa Tanzania wanapita tu na sisi hatuwezi kuruhusu wapite, tukiruhusu tutakuwa tunapingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupiga vita biashara haramu ya binadamu," alisema Rais Kikwete.

Hata hivyo alisema kuwa idara ya usalama inafanya kazi kubwa ili kubaini mianya inayotumiwa na wafanyakazi wasiokuwa waaminifu walioko mipakani ambao nao kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na usafirishaji huo.

"Hivi ninapoongea na ninyi wengine wako hapa hapa wananisikiliza,wanapuuza ninachokisema kwa kuwa nao ni miongoni mwa watu wanaofanya biashara hiyo haramu.

"Hili tunalifanyia kazi na kama mna habari tumefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayefanya biashara hiyo hali iliyotusaidia kutambua kwa undani mtandao mzima," alisema Kikwete.

Hata hivyo, Kikwete aliwaomba wananchi mipakani wasaidie kuwafichua watu wanaofanya biashara hizo na kuacha kuwapokea na kuwahifadhi watu wasiowajua majumbani mwao ili waweze kupata chochote kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Alisema kuwa umaskini kwa kiasi kikubwa unawafanya watu wafikie mahali pa kuuzana ili tu mtu apate dola 10 kwa siku na kusisitiza kuwa wale watakaobainika wakijihusisha na biashara haramu za binadamu wenzao watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili Tanzania isiwe nchi inayolaumiwa kwa kosa hilo.

Aliiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo chini ya Mwenyekiti wake, Kandoro, kuhakikisha kuwa inafanya kazi ya ziada ili kukomesha biashara hiyo hasa katika mipaka ya Kasumulu na Tunduma na kwamba serikali imechukua hatua ya kuondoa vizuizi vya barabarani kwa kuwa vilikuwa vikiwanufaisha zaidi watumishi wa umma waliopewa kazi hiyo na kushauri mbinu zaidi za kiintelijensia zitumike.

Chanzo: JK: Tumegundua mtandao wa kuuza binadamu

My take:
Inawezekanaje Rais wa nchi anatamka wazi kuwa hapo alipo wapo wahalifu wanamsikiliza na kupuuza juu ya uhalifu anaozungumzia na wahalifu hao wanaachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote. Mkuu wa nchi anapoongea maneno kama hayo anataka asaidiwe vipi ama anatoa ujumbe gani kwa wananchi ilhal vyombo vyote vya dola viko chini yake?. Kweli Tanzania tumekwisha labda ashuke malaika kuikoa nchi yetu!!

Huo ndio udhaifu alosema Mnyika. Kaka nchi kweli imekushinda.
 
Back
Top Bottom