Nifanyeje Rejesho linaponishinda?

Njopa

Senior Member
Nov 18, 2010
192
30
Wanajamvi naomba ushauri wenu! Nina rejesho la mkopo ACB ambalo toka awali nikipewa mkopo nilishtuka kuwa itakuwa shida, ikanipasa kuchukua kwani nililazimika kwani muda wote wa miezi 4 nafuatilia mkopo nilijua ni kama nilivyoomba kwamba nirudishe kwa miaka 2. Mpaka siku naitwa kwenda kuchukua mkopo nakuta imeandikwa rejesho ni ndani ya mwaka mmoja! Nilipatwa kigugumizi, mara kadhaa nikamuomba afisa mikopo iwapo tunaweza kurekebisha hilo, yeye alidai kuwa alisahau kuwaambia kamati kuwa ni miaka 2? lakini hata fomu zangu nilijaza hivyo, hata hivyo hakuna mahali nilipewa taarifa labda kuwa bwana mkopo wako utakuwa mwaka mmoja nipate kujishauri, kumbe nikajikuta nasaini kwani ni pesa nilikua naihitaji mnoo kwa biashara yangu ambapo, tayari nilikua nimechelewa kuipata ili kuilenga Krismas na sasa mbele ilibaki mwaka mpya tu. Lakini baya zaidi hivi sasa hat biashara yenyewe imefungwa kufuatia ukorofi wa mwenye nyumba!

Najiuliza nifanyeje? Mie nilikua na haya
1. Niende Benki nikaongee nao kwamba warefushe muda wa marejesho kuwa miaka 2, kwa kufanya hivyo naweza rejesha hata kwa mshahara wangu
2. Nipate msaada wa kisheria ili wasinifilisi dhamana yangu ili utaratibu wa malipo hapo juu Na. 1 ulazimishwe kisheria

Naomba Ushauri wenu
Asante
 
Kawasiliane na meneja mikopo wa bank husika sio afisa wako mtaelewana tu. Ila hakikisha unaonana naye kabla ya siku ya rejesho kufika umpe real situation.

Duc in Altum
 
Pole sana mkuu..kaza buti kaongee na meneja mikopo hapo ACB mbona hii benki huwa wakofair tu.
 
sasa si ungeinvest katika biashara ingine?.
sio lazima usubiri xmass ndo ufanye biashara
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom