Nifanyeje Rejesho la Mkopo linaponishinda?

Njopa

Senior Member
Nov 18, 2010
192
30
Wanajamvi naomba ushauri wenu! Nina rejesho la mkopo ACB ambalo toka awali nikipewa mkopo nilishtuka kuwa itakuwa shida, ikanipasa kuchukua kwani nililazimika kwani muda wote wa miezi 4 nafuatilia mkopo nilijua ni kama nilivyoomba kwamba nirudishe kwa miaka 2. Mpaka siku naitwa kwenda kuchukua mkopo nakuta imeandikwa rejesho ni ndani ya mwaka mmoja! Nilipatwa kigugumizi, mara kadhaa nikamuomba afisa mikopo iwapo tunaweza kurekebisha hilo, yeye alidai kuwa alisahau kuwaambia kamati kuwa ni miaka 2? lakini hata fomu zangu nilijaza hivyo, hata hivyo hakuna mahali nilipewa taarifa labda kuwa bwana mkopo wako utakuwa mwaka mmoja nipate kujishauri, kumbe nikajikuta nasaini kwani ni pesa nilikua naihitaji mnoo kwa biashara yangu ambapo, tayari nilikua nimechelewa kuipata ili kuilenga Krismas na sasa mbele ilibaki mwaka mpya tu. Lakini baya zaidi hivi sasa hat biashara yenyewe imefungwa kufuatia ukorofi wa mwenye nyumba!

Najiuliza nifanyeje? Mie nilikua na haya
1. Niende Benki nikaongee nao kwamba warefushe muda wa marejesho kuwa miaka 2, kwa kufanya hivyo naweza rejesha hata kwa mshahara wangu
2. Nipate msaada wa kisheria ili wasinifilisi dhamana yangu ili utaratibu wa malipo hapo juu Na. 1 ulazimishwe kisheria

Naomba Ushauri wenu
Asante
 
Mbona hamjifunzi jmn bank zinafilisi kwann msijiunge saccos au vyama vya ushirika mkopo wa muda mrf na riba ya asilimia ndogo na una milikI hisa pia.

Hiyo moja, pili kama umejiassses ukaona huwez kurudisha mkopo ndani ya mwaka 1 kawaombe wabadilishe muda au rudisha mkopo na riba uapply upya, utakuwa umepata hasara ya riba. Kuliko kujivalisha hilo bomu likakulipukie mbele ya sfr
 
Andika barua kuonesha kwamba ni kosa lao kukupa mwaka mmoja badala ya miwili kama inavojieleza kwenye fomu yako...and next time njoo ukope kwenye bank zetu za Kiislam hazina riba. Raha mustarehe
 
Andika barua kuonesha kwamba ni kosa lao kukupa mwaka mmoja badala ya miwili kama inavojieleza kwenye fomu yako...and next time njoo ukope kwenye bank zetu za Kiislam hazina riba. Raha mustarehe
kwa hiyo nikikopa 1m,narejesha 1m....
 
Jami watu hatuishi kulalamika benki mara oooh riba kubwa,haya saccos et masharti mengi ,dats napend sna vicoba hasa vile vya kuvuna ulichopanda eee,unaweka unachopata si ulipe ulichochukua ,siku huna unangaa sharubu ,
 
Tunashkuru saana kwanza kwa kutudanganya kwamba Bank wamekosea kuandika.

Hembu weka hapa,umekopa kiasi gani,ili kujua kama Bank hiyo inatoa miaka miwili kwa kiasi hicho
 
Mbona hamjifunzi jmn bank zinafilisi kwann msijiunge saccos au vyama vya ushirika mkopo wa muda mrf na riba ya asilimia ndogo na una milikI hisa pia.

Hiyo moja, pili kama umejiassses ukaona huwez kurudisha mkopo ndani ya mwaka 1 kawaombe wabadilishe muda au rudisha mkopo na riba uapply upya, utakuwa umepata hasara ya riba. Kuliko kujivalisha hilo bomu likakulipukie mbele ya sfr
kashakula mkopo tatizo..lol
 
nami yaliwahi kunikuta, endele akulipa kila unachopata mbali na vitisho unavopata, kama umevuka nusu usiogope endele kuongea nao utamaliza tu.
 
Kama uko kwenye nyumba ya kupanga, kula kona... Teh teh... No way, be honest to them and you will ultimately pay them. Even though watakuletea varangati la kufa mtu mpaka mfikie kwenye point ya kuheshimiana...
 
File for bankruptcy...your debtors will get a court order not even to contact u...if u meet qualifications..onana na mwanasheria uone inaendaje hii
 
Pole sana ndugu yangu... muhimu hapo ni kukomaa kulipa hata kama ni kidogokidogo. ACB watakusumbua na kukuchimba mikwara kiasi kwamba kama una tatizo la unene huna haja ya kufanya mazoezi maana utapungua automatically. Walipe kila muda wa rejesho hata kama ni kidogo. Usiwakimbie.
 
Mkopo ulikuwa siyo wako..... mkopo ni wa biashara na biashara ndiyo inatakiwa ilipe mkopo...... business is a separate entity from the owner of the business..... same apply to business liability

tafakari na ujiongeze
 
Back
Top Bottom