Nifanye nini...

Penny

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
575
48
Za leo wandungu, jamani naombeni mnisaidie mimi na kitu shingoni kimevimba na natakiwa kufanyiwa operation.

Ila kila mda ukifika na cancel nakuweka tarehe nyingine. Shida yangu kuu ni kuogopa kaputi.

Nisaidieni jamani, hivi eti kaputi huu ua na ni nini nifanye ili nitoe huu uoga.

Naukiwekewa mtu hujisikiaje haswa. Ntashukuru sana wapendwa kwa msaada wenu.
 
ungekuwa unahitaji kupona usingeomba msaada hapa ila ungeingia kufanyiwa opareshen
 
siku hizi wanakuchoma ganzi lakini unakuwa bado na fahamu zako, usiogope huwa haiumi....nenda ukatibiwe dear
 
za leo wandungu, jamani naombeni mnisaidie mimi na kitu shingoni kimevimba na natakiwa kufanyiwa operation. Ila kila mda ukifika na cancel nakuweka tarehe nyingine. Shida yangu kuu ni kuogopa kaputi. Nisaidieni jamani, hivi eti kaputi huu ua na ni nini nifanye ili nitoe huu uoga. Naukiwekewa mtu hujisikiaje haswa. Ntashukuru sana wapendwa kwa msaada wenu.

Pole Penny ....(kwanza umepotelea wapi?)

Hiyo ni dhana potofu. Aina ya ganzi utakayopewa itategemea na tatizo lako. Kama ni tatizo dogo, Dr atakupa nusu kaputi ya kuzuia maumivu kwenye eneo husika tu (local anaesthesia) ila kama tatizo ni kubwa kidogo basi utapewa nusu kaputi ya kukulaza kabisa (genaral anesthesia). Hata hivyo kwa technolojia ya sasa hilo si suala la hatari tena. Nakushauri uende haraka sana ukafanye hiyo operation badala ya kusogeza mbele kwani unazidisha matatizo.

Nakutakia upone haraka ili tuendeleze hili libeneke la hapa JF.
 
Penny pole sana, ila kama kaka mkubwa DC alivoshauri wala usiogope, si hatari kama unavyodhani ila kuacha huo uvimbe ni hatari zaidi ya kaputi/nusu kaputi.
i hv been there, there is nothing to be scared of...
 
Mdau pole sana kwa matatizo,naamini utafuata ushauri wa wadau,ila mtangulize Mungu na kuwa na imani,hakika utapona na kurudi Jamvini kuliendeleza Ribeneke,pole sana sie twakuombea Mungu muweza wa yote.
 
Kama upo bongo lazima hofu ikufike wangu lakini kama upo nje ya nchi punguza hofu. Cha msingi jikabidhi mikononi kwake muumba atakulinda wakati wa upasuaji na kukuponya kwa hilo. Nakuombea upate kupona mumy.
 
Kuna ukweli hapo. Kuna baadhi ya hospitali hawajali na ni hatari. Lakini kwa vile ni suala la uhai wako basi nakushauri utafute Dr anayeaminika. Itakuwa gharama kidogo lakini kazi yake inakuwa na uhakika. Njia rahisi ambayo imewahi kunisaidia ni kutafuta specialist pale Muhimbili na kukutana naye kwenye hospitali yake ya nje.
 
Endelea tu kuahirisha hiyo operation. Itafika siku hutakuwa na uwezo tena wa kuahirisha.
 
Chukulia kama ni kulala usingizi tu. Kwani hujui kuna watu wakisinsia hawaamki tena?
 
za leo wandungu, jamani naombeni mnisaidie mimi na kitu shingoni kimevimba na natakiwa kufanyiwa operation. Ila kila mda ukifika na cancel nakuweka tarehe nyingine. Shida yangu kuu ni kuogopa kaputi. Nisaidieni jamani, hivi eti kaputi huu ua na ni nini nifanye ili nitoe huu uoga. Naukiwekewa mtu hujisikiaje haswa. Ntashukuru sana wapendwa kwa msaada wenu.

Usiogope mamii japo ni mara yako ya kwanza..muhimu ufanyiwe hiyo opereshi kutoa uvimbe kwani huwezi jua unavyochelewa itakusababishia madhara gani makubwa..kaputi iko powa tu, maumivu kidogo utasikilizia baada ya kuisha!!!
 
Jamani asanteni sana kwa walionipa moyo. Maana naona kama wengine wanadhani na joke vile. Niko nchi za nje, nijibu swali kwa walioniuliza. Uoga lazima uupate kama ni kwa mara ya kwanza. Mimi niliitaji mtu mwenye uzoefu au Dr. kabisa anieleze jinsi huwa. Ila nashukuruni sn. Will let u know when am done. Thanks alot.
 
Pole sana Penny,

Dr atakueleza theory ya nusu kaputi na uzoefu wake kuhusu wagonjwa anaowaona. Anaweza asiwe na uzoefu wa yeye binfsi kwa sababu inawezekana tena sana, na yeye hajawahi kufanyiwa operation. Halafu watu wengine wanaweza kuwa ni Drs lakini si lazimwa wajitaje.

Suala la muhimuni kwako ni kufahamu kuwa nusu kaputi ni safe, na pia kuwa kuna risk lakini ni ndogo. Na risk yenyewe inategemea aina ya nusu kaputi utakayopewa pamoja na ujuzi wa timu itakayokufanyia operation. Hata hivyo recovery rate kutoka kwenye ganzi ya mwili mzima kwa hali ya sasa ni zaidi ya 98%.

Best wishes and hope you get over it soon.
 
Dear Penny,
pole kwa kuumwa. Penny hakuna haja ya kuogopa kwa sababu unaweza kupigwa sindano ya ganzi shingoni na ukafanyiwa oparation bila tatizo. Kwa sababu unavyozidi kusogeza tarehe ndivyo ugonjwa unavyozidi kukuwa. Mimi nakutakia upone haraka urudi JF Ukiwa mzima. BEST WISHES AND GET WELL SOON DEAR.
 
pole sana ... lakini mimi nakushauri nenda tu ukafanye operation usijali Mwenyezi Mungu yuko na wewe... usijali kabisa sala zetu ziko nawe...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom