Nifanye nini kumudu maumivu ya kushuhudia siku za mwisho za uhai wa mke wangu?

Mkuu nilikupa dawa umepuuzia, narudia teba hizi dawa nina uhakika nazo kwa asilimia 100, kuna mtu alishapona na dawa zangu akiwa kwenye stagge aliyopo mkeo. Jaribu kumpa, ale stafeli hata 5 kwa siku na majani yake yawe ndo maji ya kunywa lita 2 au zaidi kwa siku. Utaokoa maisha ya mkeo
Humu jf ukimfundisha mtu dawa anadharau wakati tatizo ni lake.
 
HATIMAYE AMEAGA DUNIA BAADA YA MAPAMBANO YA MUDA MREFU NA SARATANI YA MATITI ILIYOSHAMBULIA MAPAFU YAKE.

ALIYETOA NDIYE AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
nimesikitika sana ndugu yangu!
pole sana brother pole sana, si vyepesi lakink pole.
mwenyezi Mungu ajalie kupumzika kwa amani amjalie kukutana nae siku ile ya ufufuo wa wote.
awape nguvu nyingi mfanye msiba mkiwa imara na thabiti.
kwa Mungu sote tumetoka na na tutarejea wakati mmoja.
pole mno kaka.
 
HATIMAYE AMEAGA DUNIA BAADA YA MAPAMBANO YA MUDA MREFU NA SARATANI YA MATITI ILIYOSHAMBULIA MAPAFU YAKE.

ALIYETOA NDIYE AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
Pole sana mkuu, Mungu akutie nguvu. Nikupe tu neno la faraja kuwa hii Dunia ni njia na sisi tunapita, hakuna njia tunaweza epuka kifo. Zika mkeo na ushukuru kwa yote.

NB: Nimetoka kuzika ndugu wa karibu sana jana kwa huu ugonjwa wa cancer so naelewa maumivu na gharama za kuuguza. Huu ugonjwa ni KIBOKO
 
Mungu awe pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu.
BWANA ametoa BWANA ametwa jina la BWANA lihimidiwe.

ni heri uaminifu ukawepo na lambi lambi ikapita kwa ajiri yake mfiwa,tumekuwa nae pamoja tangu mgonjwa mpaka mauti inamfika mke wake kipenzi.

Ni'pendekezo kwa atakae guswa akaona vyema basi yafaa kumchangia.dunia ni mapito na hichi ni kipindi kigumu mno sikia kwa jilani yako tu.
 
Pole sana mkuu, Mungu akutie nguvu. Nikupe tu neno la faraja kuwa hii Dunia ni njia na sisi tunapita, hakuna njia tunaweza epuka kifo. Zika mkeo na ushukuru kwa yote.

NB: Nimetoka kuzika ndugu wa karibu sana jana kwa huu ugonjwa wa cancer so naelewa maumivu na gharama za kuuguza. Huu ugonjwa ni KIBOKO
Aisee pole sana
 
HATIMAYE AMEAGA DUNIA BAADA YA MAPAMBANO YA MUDA MREFU NA SARATANI YA MATITI ILIYOSHAMBULIA MAPAFU YAKE.

ALIYETOA NDIYE AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
Pole sana Mkuu kwa magumu yote uliyopitia; wakati wa kumuuguza mkeo na hatimaye kifo chake.

Zingatia tu kwamba wote ni wapita njia hapa Duniani na mwisho wa siku tutakufa. Endelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani!
 
Kupitia hii nimeumia sana nahisi nina hatia kwa sababu dawa najua lakini inakua ngumu kusaidia watu. Najitolea kwa mwenye tatizo la kansa aniambie dawa ntamuelekeza na atafanyia huko aliko anionyeshe vipimo na nijue iko stage gani ntamuelekeza dawa na awe na nia ya dhati na sio kebehi au kujaribu.
 
Pole mkuu. Kuna watu Mungu anawatumia kuwaombea watu. Jaribu kwenda makanisani utaweza kupata msaada. Usikate tamaa. Mungu bado yuko na anasikia maombi. Ninaomba mtu atakayekuomba pesa kumwombea mpendwa wako huyo si mtumishi wa Mungu. Yesu alisema mmepewa bure toeni bure. Maombezi ya mtumishi wa Mungu ni bure na ni Mungu anaponya.

Angalia maneno haya chini ya kukufariji;

Njoni kwangu (Yesu), ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. (Mty 11.28-30).

Mathayo 8:17 “ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” Yesu alichukua udhaifu wetu na magonjwa yetu akayapeleka pale msalabani, kila aliye na imani na akimuamini Yesu atakuwa mzima.
Biblia inasema “Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” Huhitaji kuugua au kuwa mgonjwa wakati Yesu alikufa ili wewe uweze kuwa mzima.
MAOMBI:
1. Mwambie Mungu achukue mizigo yako ili wewe uweze kuwa huru.
• Bwana chukua mizigo yangu kwa maana wewe umesema nikupe mizigo yangu na wewe utanipa pumziko Bwana chukua mateso yangu mimi nataka kuwa huru.
TANGAZO:
Chochote kilichokufa katika maisha yako kikafufuke kwa Jina la Yesu,
Kila kazi za ibilisi zilizofanyika kwako kupitia kuzaliwa kwako leo ibilisi akakuachie kwa Jina la Yesu.
Chochote kilichokushikilia kwa miaka mingi ambacho kimetokana na kuzaliwa kwako kikaha
kwa Jina la Yesu.
Nguvu yoyote ya umasikini au ya mateso ambayo imekufuatilia kwa miaka mingi leo ikaondoke kwako kwa Jina la Yesu.
Maneno yoyote yaliyotamkwa kinyume na Baraka zako au kinyume na mapenzi ya Mungu kwako nayafuta kwa Jina la Yesu; wewe UMEBARIKIWA.
 
Habari zenu wakuu!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii, ijapokua hali hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu.
Ahsanteni

Pole Prospilla, Jiweke karibu na Mungu na muhimu wote kuwa na matumaini mtakutana tena baada ya muda mchache.

Mfarijiane kwa maneno haya:-
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima.
Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa.

Wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima wa milele.

Lakini wewe, enenda zako mpaka mwisho. Utapumzika, nawe ndipo mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekewa.
 
Habari zenu wakuu!

Kuna uzi nilileta humu (jukwaa la afya) kuelezea namna mke wangu anavyopambania uhai wake kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Kwakweli matumaini ya mke wangu yanazidi kufifia sana, naona kwa sasa anakaribia mwisho wa uhai wake.

Napata hisia kali sana ambazo ukisoma hapa huwezi kuzihisi mpaka labda upatwe na jambo kama hili.

Najua wapo wazoefu waliopitia hali kama hii, ijapokua hali hii kila mmoja anaweza kuimudu kwa namna yake ila najua walau wanaweza kusaidia namna ya kumudu hisia hizi.

Kwa ambaye hujapitia nyakati kama hii kwa mpendwa wako, sijui hata nikusimuliaje!

Sijui kwa namna gani nitaweza kumudu kusahau hii hali ndugu zangu.
Ahsanteni
Mbona ile namba niliyokupa hukumtafuta yule mtu angekusaidia hata ushauri alikua na mgonjwa Wa cancer kashafanyiwa mionzi na operation sasa hivi anaendelea vizuri sana, nilimuuliza Jana kwamba Kuna mtu anamgonjwa kama wako nilpatia namba yako akupigie uweze kumsaidia jinsi ya kufanya akaniambia hujamtafuta na yuko tayari kukusaidia hata mchango Wa kipesa kama huna uwezo.
 
Mgonjwa amefariki
 
Mkuu mbona sijaona namba? Ahsante sana lakini
 
Mbona ile namba niliyokupa hukumtafuta yule mtu angekusaidia hata ushauri alikua na mgonjwa Wa cancer kashafanyiwa mionzi na operation sasa hivi anaendelea vizuri sana, nilimuuliza Jana kwamba Kuna mtu anamgonjwa kama wako nilpatia namba yako akupigie uweze kumsaidia jinsi ya kufanya akaniambia hujamtafuta na yuko tayari kukusaidia hata mchango Wa kipesa kama huna uwezo.
Mkuu Hii mitandao ina mambo mengi ya kushangaza, tenda tu jinsi nafsi ilivyokusukuma baada ya kusoma bandiko na uende zako.

Pole sana mfiwa!
 
Back
Top Bottom