Mkuu MKJJ,
Hii mikwara ya akina Ndejembi na Kimaro ni ya kitoto, ya kijinga na imepitwa na wakati. Inawezekana wametumwa au wamekurupuka. Either way wanatia aibu.
MwanaCCM yeyote anayekidhi vigezo vya kugombea urais atakayeogopa kuchukua fomu kwasababu ya hii mikwara nae ni ****.
Sasa nasubiri kuona reaction ya Mheshimiwa Kikwete. Mi ningekua yeye, at the earliest opportunity ningesema something to the effect, "Ndugu wanaCCM wenzangu, nashukuru kwa support yenu, ila kwa wale wanaopiga mkwara wanachama wengine wasijitokeze kugombea urais ningewaomba wasitishe hizo kauli. Kazi niliyoifanya inaonekana na ndo itakua msingi wangu wa kuwaomba Watanzania kura zao niendelee kuwaongoza".
Hii ni fursa kwa Mheshimiwa kuonesha political maturity. Wale wanaotoa kauli za mkwara hawamsaidii bali wanamkwaza. Wamem-preempt aoneshe kwamba hahitaji kupigwa chepuo. Akikaa kimya atadhihirisha kwamba kweli yeye ni kiongozi dhaifu aliyeshindwa kazi aliyowaahidi wananchi na anahitaji kupigwa jeki.
The ball is in JK's court.
Wazo zuri sana hili, Lakini itakuwa vigumu sana kwa Kikwete kufanya haya. Miaka minne iliyopita imeonyesha kwa kiwango kikubwa utendaji kazi wa JK.