NIDA Kama Mtu hana kitambulisho cha kuzaliwa lazima alipe 5,000/= kwa hakimu kuapa?

MrIsidori

Senior Member
Apr 3, 2014
191
83
Watu wengi waliokwenda kujiandikisha Kitambulisho cha uraia huku Moshi Vijijini Kata Ya Kibosho Kati wamerudi baada ya kuambiwa kama hawana vyeti vya kuzaliwa walipe shs 5,000/= hakimu ili waape!
 
Huko mahakamani hizo 5,000 za Kuapa zina EFD's risiti,au makarani wanapata za kubrush viatu?
Nimeuliza tu jameni,tusitafutane!!!)))
 
Tena wanawasaidia tu, fomu ya Mahakamani "Affidavity" Ni elfu 10 na sio 5, taratibu kwenda kulipia benk ila ukifanyiwa f5 jua mmegawana gharama!
 
Watu wengi waliokwenda kujiandikisha Kitambulisho cha uraia huku Moshi Vijijini Kata Ya Kibosho Kati wamerudi baada ya kuambiwa kama hawana vyeti vya kuzaliwa walipe shs 5,000/= hakimu ili waape!
Cheti cha kuzaliwa unapewa bure? Cheti kuzaliwa f10 hata hiyo ya Mahakamani ni F10 maana inasimama badala ya hicho cheti, punguzeni kulalamika, inatakiwa walipie f10 benki, kama wanalipa f5 wanatoa ya kiwi tu na sio gharama halisi!
 
Mitanzania inapenda lalamika kweli.
Sasa mtu hata cheti cha kuzaliwa hana afu anataka apate NatId
 
Ninachofahamu ili upate kitambulisho cha uraia unatakiwa uwe na kiambatanisho kimojawapo kati ya hivi kitambulisho cha kura,cheti cha kuzaliwa,bima ya afya,cheti cha elimu ya secondary,cheti cha elimu ya secondary ya juu......Hiyo habari kwamba ni lazima uwe na cheti cha kuzaliwa si kweli.....Mama yangu alitumia kitambulisho cha kura kupata hicho cha uraia yeye hana kitambulisho cha kuzaliwa
 
Labda kama sharia za kupata Kitambulisho cha uraia zimetofautiana sehemu na sehemu
 
Back
Top Bottom