Ni zawadi gani nzuri, inayoweza kumfurahisha na kumuachia kumbukumbu ya furaha mkeo/mumeo aliyepitia changamoto kali kipindi cha nyuma?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,482
40,496
Nawaza zawadi ya kumpatia mke wangu kama 'surprise' tu, kutokana na changamoto alizopitia mwaka jana, mwezi kama huu, mpaka ikafikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi.

Alifiwa na mzazi wake aliyempenda sana; aliyekuwa akimuuguza muda mrefu.

Kabla ya mzazi wake hajafariki, ndani ya wiki mbili hivi, 'wife' akafanyiwa upasuaji mkubwa, hajamaliza hata wiki, akatakiwa kufanyiwa tiba ya mionzi. Ile kuanza tu tiba ya mionzi, mzazi wake akafariki.

Ndani ya muda mfupi, vichwa vilikuwa vimevurugika sana; lakini tuliweza kuhimili ingawa changamoto zilikuwa nyingi.

Sasa nawaza, nimpe zawadi gani itakayomsababisha kutoa machozi ya furaha, iwe kama 'surprise'.

Kama gari, yeye siyo mpenzi sana, hata lililopo huwa halitumii; kama ni nyumba, anaweza asione kama zawadi, kwa sababu itakuwa kama sehemu ya familia (yeye na watoto).

Nawaza, zawadi ambayo yeye ataiona inamgusa yeye tu.

Karibuni kwa mawazo.
 
Zawadi ni muhimu sana kuboresha mahusiano.

Sio lazima zawadi za gharama kubwa, Wakati mwingine hata zawadi ya Ice cream au Ubuyu wa Zanzibar atafurahi.

NB: inategemea na mpenzi uliyenaye, mwingine ukimpelekea zawadi hizi ndogo ndogo anakutupia usoni 🤪
 
yani unaacha kutoa sadaka ya shukurani kwa mungu unawaza kutoa zawadi kwa mkeo
 
Zawadi ni muhimu sana kuboresha mahusiano.

Sio lazima zawadi za gharama kubwa, Wakati mwingine hata zawadi ya Ice cream au Ubuyu wa Zanzibar atafurahi.

NB: inategemea na mpenzi uliyenaye, mwingine ukimpelekea zawadi hizi ndogo ndogo anakutupia usoni 🤪
Kwa mfano, nikimfanyia hafla itakuwa na maana
 
Tafuta eneo zuri ambalo limetulia hasa hotel zilizopo kwenye mbuga za wanyama huko au hoteli zilizo karibu na mwambao wa ziwa lolote kwenye Beach nzuri na tulivu, kaeni chini nunua chakula anachokipenda na kaa mkao wa kumwangalia kisha mwambie namna unampenda mwambie hata kama kutakuwa na changamoto ya zile zilizopita bado utaendelea kuwa nae tumia siku hata 3 na ikiwezekana zima hata simu tumia mda huo kuongea nae, kama ni mkristo nunua zawadi Bible mpe mwambie nakupa neno la uzima baki nalo duniani na mbinguni
 
Wazo zuri, kuna ulazima wa kwenda na watoto/timu yangu?
 
Back
Top Bottom