Ni wasanii wachache wa HIPHOP wana stick na topic moja kwenye uandishi

Vesper-valens

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
5,282
7,377
Habari wakuu

Naomba niweke wazi hili , Mimi nafatilia sana music wa Bongo kwa ujumla tangu mwaka 2001 mpaka sasa
Napendelea zaidi Music wa Hiphop hvyo basi wasanii wengi wa hiphop bongo nimekua nikifuatilia sana ngoma zao za kipindi hiko na hata sasa

Hapa Tanzania tumebarikiwa vipaji vingi sana vya wasanii wa ku rap lakini ni wachache sana ukiwasikiliza word to word ukute wame stick kwenye topic husika kutokana na jina la nyimbo husika

Kwa uchunguzi wangu hii ni list ya Wasanii wachache nliowafuatilia na kuona uwezo wao wa ku stick kwenye topic husika ya nyimbo

Albert Mangwea

The late Albert Mangwea ni genious , tangu naanza kumskiliza kwenye "Ghetto Langu mpaka No beef ft TID , hakuwahi kutoka out of topic kwenye ngoma zake alizofanya mwenyewe hata alizo shirikishwa

LANGA ( Lyrical And Natural Gifted in Africa)

Huyu jamaa naye Tangu kwenye Wakilisha mpaka project zake kama solo artist ameweza ku maintain uandishi wake kwa kustick na topic husika iliyopo mezani
Mfano ngoma kama Ni Hayo tuu aliyoshirikishwa na FID Q aliweza sana ku stick na topic iliyokua inayongelewa mpaka mwisho wa verse

Hata hizi ngoma mbili alizoachia za mwisho Supply & Rafiki wa kweli ukiziskiliza utanielewa

Jay Moe

Juma mchopanga Kwanza jamaa ni super talented sema design kama wabongo hawajamuelewa sana, jamaa ana uwezo mkubwa sana wa ku stick na topic inayozungumziwa
Tangu naanza kumskia miaka ya 2001 mpaka sasa ngoma zake zote zimestick kwenye topic husika na hii ndo maana halisi ya Msanii

Afande sele

Huyu Mfalme wa rymes ,naye uandishi wake ume base kwenye kuandika kutokana na topic husika
Sikiliza ngoma kama , Mkuki moyoni, Dunia ina mambo, Simba Dume,
Au ngoma alizo shirikishwa kama
Elimu dunia ya Daz baba, Swahiba ya jebby utaweza kuelewa nnachokizungumza

Proffessor Jay

Huyu Kwangu ni Godfather wa Music wa bongo fleva, tangu naanza kumsikia mpaka sana huwez kukuta ngoma yoyote yuko off topic

Mwana FA

FA naye ni bingwa wa ku stick kwenye topic kwenye uandishi wake ,

Hao ni baadhi tuu ya wasanii wenye uwezo mkubwa ku stick kwenye topic

Kwa upande mwingine kuna wasanii wana flow kali , wana panchline lakini ukiwaskiliza Jina la nyimbo na verse haviendani kabisa , yani wanauwezo wa kuandika lakini wanavyoviandika haviendani na topic husika , hawa sometimes wana stick kwenye topic , sometimes wanakua off topic

FID Q

Huyu jamaa wengi hupenda kumuita conscious hata mimi nakubali jamaa yuko deep kwenye uandishi, Lakini moja kati ya weakness kubwa kwa huyu jamaa ni uwezo wa kustick kwenye topic husika
Niwape mfano kwenye wimbo wa CNN Ngwea ft FID Q licha ya Jamaa kukiri mwenyewe ilibidi afute verse aandike nyingine bado alikua OFF TOPIC
Ngoma ilikua inazungumzia kukesha na ku part lakini ukiskiliza verse ya FID Q ilikua out of topic kabisa yan jamaa alijisifia tuu

Kwa kifupi huyu jamaa ngoma zake huwa anaongea vitu vingi sana lakini unakuta jina na kilichondani ya nyimbo haviendani

Ngoma ambayo kidogo ali stick kwenye topic ni Sihitaji marafiki

Chidibenz

Huyu Mfalme wa Ilala ni mkali wa flow na punch lakini kwenye ku stick kwenye topic ni zero kabisa , huwa nashangaa watu wanaosema jamaa anajua freestyle hichi kitu nakipinga coz jamaa freestyle zake nyingi hata ukiskiliza hazina maana , ni kama anatafuta maneno yatakayo leta vina tuu hata kama hayana maana

Lord eyez

Jamaa kwa flow na punch yuko vizur lakini ukiskiliza verse zake word to word utagundua huyu jamaa naye ni wale wale wa kuandika tuu kuunganisha maneno ila ku stick kwenye topic jamaa hawezi

Hawa ni baadhi tuu lakini wapo wengi nimekosa muda ningewaelezea

Note

Haya ni maoni binafsi
 
Ebwanaee! Wewe jamaa gemu unaifuatilia vyema. Ni kweli hao uliowataja wako vizuri sana. Mr. Blue naye anajua sana hadi kwenye nyimbo anazoshirikishwa.

Ila hawa watoto wengi wa gemu ya sasa wana_rap rap tu kama Stamina. Wanaunga unga maneno .
Stamina ni moja kati ya ma rapper wa wabovu sana katika uandishi
Nasikitika kuna wanaomchukulia n rapper bora
 
Afu mbaya zaidi stamina anajiona ni moja kati ya Ma Mc bora wa Hiphop Bongo
Anakuambia ukimtoa Roma na fid haon rapper wakumtisha

Anyway kwenye sanaa na michezo kila mtu anamashabiki wake

Kuna watu huyo huyo stamina ndio favorite rapper wao

Kuna sijui umri au tuseme uzoefu ukiufikia unakuwa na mapenzi na maono yako then unaheshimu na ya wengine.

Mana mwisho wasiku hakuna kipimo kinachopima ukali (UKALIMETER)

Your G.O.AT is someone's flop
 
Anakuambia ukimtoa Roma na fid haon rapper wakumtisha

Anyway kwenye sanaa na michezo kila mtu anamashabiki wake

Kuna watu huyo huyo stamina ndio favorite rapper wao

Kuna sijui umri au tuseme uzoefu ukiufikia unakuwa na mapenzi na maono yako then unaheshimu na ya wengine.

Mana mwisho wasiku hakuna kipimo kinachopima ukali (UKALIMETER)

Your G.O.AT is someone's flop

Ladha ya muziki ipo sikioni mwa muhusika na sio REASONING

Kila kizazi kina ladha yake mkuu

Nilikua mpenzi kweli wa hip hop ya mbele lakini hizi za akina migoz, future lil baby meek hapana aisee
 
Back
Top Bottom