Mudi Salah
Member
- Jul 5, 2022
- 48
- 32
Torati 23:19-20Amani iwe nanyi.
Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!
Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.
Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.
Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!
Asanteni