barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,324
- 29,586
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kupitia kanuni za kuendesha bunge maalum, anasema hayo??? Sina comment.
Nitakwambia kile ninachokifahamu kwa maarifa yangu madogo tu niliyo nayo.Ingekuwa vizuri kwa wale wanaosema katiba ni mbovu wa-identify kifungi kipi ni kibovu kuliko kutoa blanket denial.
Hii mbona ipo wazi sana hii ni katiba bora kabisa sote tunajua hivyo
Naunga mkono hoja ya Mahalu.
Wewe unautajili gani wakati hata chai mpaka kwa mama yako halafu unajifanya unapesa,Nimesema mtu anayepinga katiba hii ni chizi.
Bahati nzuri kila mtu hapa jamvini anafahamu kuwa wewe ni mwendawazimu na kila ukisemacho hakiaminiki!Wewe unautajili gani wakati hata chai mpaka kwa mama yako halafu unajifanya unapesa,Nimesema mtu anayepinga katiba hii ni chizi.
Ni Katiba bora Afrika Mashariki
Profesa Mahalu anawanyooshea vidole wale wanaodai kuwa Katiba ilipitishwa kiujanja ujanja na kuwa hata uandishi wake haukuwa bora, akisema kuwa huo ni wongo.
Ni waongo wanaodai kuwa Katiba ilipitishwa kiujanja, nilikuwa pale, tulikuwa na wasomi waliobobea katika uandishi na sheria, hakuna mahali ambapo palipindishwa au kipengele kilichobadilishwa kiujanja. Hatukubadili chochote, anasema.
Anasema Katiba hiyo iliyopitishwa ni bora na yenye viwango ambavyo hata majirani zetu Kenya, Uganda na Rwanda, wanaitamani.
Tumeitengeneza katika viwago ili kila kitu kiende sawa, bila hivyo tusingeweza kufanya lolote. Tumefanya kazi kubwa kuunda Katiba pendekezwa na watanzania hawana budi kujivunia hilo, anasema.
Chanzo: Mwananchi
wewe ndio chizi kabisa unayeshabikia katiba iliyopigiwa kura na marehemu..hv nyie mnaojiita wasomi usomi wenu unalisaidia nini taifa hili? Ikiwa mnashabikia katiba haramu kama hii? ukiendekeza njaa unaweza kuuza utu wako..hv mnafikiri kwa kichwa au M-A K-A..L.£-¤?Wewe unautajili gani wakati hata chai mpaka kwa mama yako halafu unajifanya unapesa,Nimesema mtu anayepinga katiba hii ni chizi.
Hii mbona ipo wazi sana hii ni katiba bora kabisa sote tunajua hivyo
hawa wasomi wa tz hawa...umaskini umewatafuna vibaya mno
Wakati baadhi ya watu wakiendelea kuamini kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samuel Sitta alichakachua kanuni ili apitishe Katiba, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia Kanuni hizo za kuendeshea Bunge hilo, Profesa Costa Ricky Mahalu amemtetea akisema Bunge halikukosea kurekebisha kanuni hizo.
Profesa Mahalu ambaye ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Bunge la Katiba liliendelea kubadili baadhi ya kanuni zilitungwa ili kufikia malengo ya kupata Katiba nzuri
Profesa Mahalu anawasihi watanzania na wanasiasa kutomhukumu Sitta kwa madai kuwa alikuwa akichakachua kanuni hizo kwa maslahi binafsi. Alisema kamati yake kuidhinisha kanuni zilizofaa kuendesha Bunge la Katiba, bado kulikuwa na fursa ya kuendelea kuzifanyia mabadiliko kanuni hizo kadiri ya mahitaji.
Sitta hana uwezo wa kufanya marekebisho kwa maslahi binafsi au ya chama, tatizo ni kuwa hili jambo limeingiliwa na siasa kidogo, mchakato mzima ulifanya kazi kama timu, anasema
Anasema marekebisho yeyote ya kanuni yanapoibuliwa na mjumbe, hupelekwa kwenye kamati ya uongozi, kisha kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na Spika Sitta huwauliza wajumbe iwapo wanaafiki au la.
Sitta huuliza tu iwapo marekebisho yanaafikiwa au la. Lakini masuala ya kisiasa yanamhukumu jambo ambalo si kweli, mimi nilikuwa mwenyekiti najua hakuna chochote. anasema
Profesa Mahalu anaendelea kueleza Marekebisho ni muhimu kwa kuwa sheria mbaya inakwamisha vitu, iwapo mambo hayaendi inavyotakiwa kutokana na baadhi ya kanuni, hatuna budi kuzifanyia marekebisho kwa sababu nia yetu ni kupata katiba bora, anasema Profesa Mahalu.
Anasema kuwa katika kipindi chote cha uendeshaji wa bunge hilo hakuna kanuni iliyoharibiwa na kama jambo hilo lingetokea basi angelipinga kwa nguvu zote.
Pamoja na hayo Profesa Mahalu anasema kuwa, Bunge hilo lilifanya kazi katika mfumo uliokubaliwa wa kanuni kuanzia uteuzi wa wajumbe hadi pale Rais alipokabidhiwa Katiba pendekezwa.
Uteuzi wa viongozi ulikuwa mzuri, sheria namba 83 ilitumika ipasavyo na kila kitu kilienda sawa, anasema
Mwanasheria huyo ambaye pia alikuwa katika kamati ya uandishi anasema, watanzania hawana budi kufurahia katiba hiyo pendekezwa kwa sababu imefanyiwa kazi na jopo la wasomi na wazalendo wa nchi hii.
Tulifanya kazi sana, hatuwezi kusema kuwa tutafanya vitu vyote kila mwananchi anavyovitaka lakini misingi muhimu tumeiweka katika katiba hiyo, kwa mfano, misingi ya uchumi, utamaduni na haki, anasema
Anasema katiba hiyo imemlenga Mtanzania wa kawaida ambaye hapo zamani alikosa haki zake za msingi na hakujua wapi pa kupeleka kilio hicho, lakini sasa Katiba inamtambua.
Anatolea mfano wa makundi ambayo yalisahaulika kaw muda mrefu kuwa ni pamoja na wakulima, wafugaji na wavuvi ambao hivi sasa Katiba inawatambua.
Asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima na wafugaji, katika Katiba hii haki zao zimeainishwa. Kila mmoja amepata haki ya kufuga, kuwinda, kumiliki ardhi na kulima. Hili halikuwepo hapo zamani kwani sasa hivi hata wachimbaji wadogo nao wamepewa umuhimu, anasema.
Profesa Mahalu anayataja mambo matatu makubwa ambayo yameainishwa na kuchambuliwa katika Katiba mpya kuwa ni ushirikishwaji wa Tanzania bara na Zanzibar. Anasema masuala ya Muungano katika Katiba hii yatasaidia kuondoa kero zilizopo na kuleta suluhu.
Jambo jingine kubwa ambalo Profesa Mahalu amesema Katiba imeyafanyia kazi ni ushirikishwaji wa vijana katika siasa kwa kiasi kikubwa hadi kutambuliwa kwa Baraza la Vijana la Taifa.
Unajua vijana ndiyo taifa la kesho, na ni asilimia kubwa ya Watanzania...hivyo katika Katiba tumeweka haki nyingi za vijana na ndiyo maana likaundwa Baraza la Vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 35 ambao watatakiwa kushiriki kikamilifu katika siasa, anasema.
Kingine ni ushirikishwaji wa wanawake kwa asilimia 50 jambo ambalo anasema kuwa litawanyanyua wanawake hao katika kushika nafasi za uongozi. Profesa Mahalu anasema kuwa wanawake sasa hawatanyanyasika katika masuala ya ardhi na watatambulika kisheria katika masuala ya mirathi.
Kilichobaki ni wanawake wenyewe kutambua haki zao na kuzidai kwa sababu tayari Katiba imeshaweka masuala hayo ndani yake. anasema
Sambamba na hilo masuala ya haki za makundi ya wafugaji, walemavu, wakulima na wachimbaji wadogo kuwekwa katika Katiba ni jambo ambalo anasema limeifanya Katiba hiyo imguse mwananchi katika kiwango cha chini kinachowakilisha jamii kubwa ya Watanzania.
Ni Katiba bora Afrika Mashariki
Profesa Mahalu anawanyooshea vidole wale wanaodai kuwa Katiba ilipitishwa kiujanja ujanja na kuwa hata uandishi wake haukuwa bora, akisema kuwa huo ni wongo.
Ni waongo wanaodai kuwa Katiba ilipitishwa kiujanja, nilikuwa pale, tulikuwa na wasomi waliobobea katika uandishi na sheria, hakuna mahali ambapo palipindishwa au kipengele kilichobadilishwa kiujanja. Hatukubadili chochote, anasema.
Anasema Katiba hiyo iliyopitishwa ni bora na yenye viwango ambavyo hata majirani zetu Kenya, Uganda na Rwanda, wanaitamani.
Tumeitengeneza katika viwago ili kila kitu kiende sawa, bila hivyo tusingeweza kufanya lolote. Tumefanya kazi kubwa kuunda Katiba pendekezwa na watanzania hawana budi kujivunia hilo, anasema.
Ukawa na Bunge la Katiba
Profesa Mahalu anaeleza kuwa kitendo cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia Bunge la Katiba ni kutumia uhuru wao kama wanasiasa.
Siwezi kuwahukumu au kuwalaumu Ukawa kwa chochote kwa sababu wana uhuru wa kushiriki kikamilifu katika Bunge hilo na pia wana uhuru wa kuliacha iwapo wanaona hawaridhishwi nalo, anasema.
Anasema kama Ukawa waliona mchakato wa Katiba haukuwaridhisha, wana uhuru wa kulisusia na hakuna atakayeweza kuwahukumu.
Chanzo: Mwananchi
hawa wasomi wa tz hawa...umaskini umewatafuna vibaya mno
nadhani utakuwa unapenda kukaa kwenye vijiwe vya kahawa au vingine vyote vinavyofanana na hivyo ambavyo vina sifa kuu ya watu kuzungumza pasi na kupeana nafasi hasa inapozuka hoja yenye mkinzano mkubwa ama wa kisiasa. Na huna muda wa kujishughulisha kujisomea vitabu na sitashangaa sana nikisikia kuwa umeambiwa kuwa rasimu ya Sita nad Chenge ni bora ila hujaisoma.Ingekuwa vizuri kwa wale wanaosema katiba ni mbovu wa-identify kifungi kipi ni kibovu kuliko kutoa blanket denial.