Ni wakati sasa wa JWTZ kutoka hadharani na kuwatoa hofu wananchi na kukemea viongozi wanaowasingizia

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
je si wakati muafaka kwa jeshi kujitokeza hadharani na kukanusha madai ya CCM na serikali kwamba wananjeshi wataingia mitaani kwa sababu ya serikali tatu.

Ni muda muafaka Mwamunyange kuwadhibitishia watanzania kwamba wao ni weledi na si kweli kwamba wanamawazo ya kupindua nchi eti kwa sababu ya serikali tatu.

Eti kutenganisha mambo ya Tanzania bara na ya muungano ili yawe wazi na yashughulikiwe peke peke eti jeshi litakosa mishahara?

C'mon, Mwamunyange jitokeze kuonya wanasiasa waache kulichezea jeshi; la sivyo tutaamini na nyie ni watu msiotaka mabadilikokatika nchi yetu!
 
Kaka wazo zuri sana hilo,hawa wasiasa wanalifanya kama vile JWTZ ni jeshi lilokuwa halina heshima,halijui nini linafanya..,hawa wanasiasa uchwara wanataka kulingiza Jeshi kwenye marumbano yao ya siasa.

Lakini kwa vile Mwamunyange ni rafiki yake mkuu wa nchi sifikirii kama anaweza kumwamrisha msemaji wa jeshi atoke hadharani kuwatoa hofu watanzania
 
Jeshi linaumizwa na wajinga ...linaingizwa kwenye siasa uchwara za CCM , wajitokeze waseme na watoe Onyo la sivyo watapelekewa uchafuzi wote
 
Captain John Komba akichangia Bungeni amedai Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawajatoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba

Sasa,kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote.

-Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim,Mzee Butiku na Mzee Warioba bado ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere.

-Huwezi kusema unamuenzi Mwalimu Nyerere kisha ukakubaliana na kauli za kifedhuli na vitisho vya kipuuzi kabisa vya Captain Komba .Bila aibu wabunge na mawaziri wanashangilia?

-Sasa natoa Rai kwa Viongozi na wafuasi wote wa UKAWA,tusikubaliane hata kidogo na Amri zinazotolewa na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano yetu.Kumbe kuzuia mikutano na Maandamano ni katika kutimiza malengo yao na kuminya haki za kiraia na kidemokrasia?

Katika mchakato huu wa kudai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili tulitakiwa kujadiliana kwa hoja na sio vitisho.

Captain Komba na CCM wenzake pamoja na Mawaziri waliokuwepo Bungeni leo watambue kuwa ndani ya Jeshi la Polisi kuna Askari wanaoguswa na harakati za kudai Tanganyika huru na Zanzibar Huru.

Ndani ya Jeshi la Wananchi watambue kuwa kuna Wanajeshi tena vijana wanaoguswa na hoja za kuidai Tanganyika huru na Zanzibar huru

-Nje ya jeshi na nje ya Bunge lipo jeshi kubwa la wananchi na hasa vijana wanaojiandaa kuidai Tanganyika Huru na Zanzibar huru

-Zama za kulazimisha Muungano wa serikali mbili kwa Vitisho zimekwishwa

-Captain Komba,wabunge na Mawaziri waliopo Bungeni leo wametuonyesha njia kwa rangi zao halisi.Tusirudi nyuma na tusiogope
 
je si wakati muafaka kwa jeshi kujitokeza hadharani na kukanusha madai ya CCM na serikali kwamba wananjeshi wataingia mitaani kwa sababu ya serikali tatu.

Ni muda muafaka Mwamunyange kuwadhibitishia watanzania kwamba wao ni weledi na si kweli kwamba wanamawazo ya kupindua nchi eti kwa sababu ya serikali tatu.

Eti kutenganisha mambo ya Tanzania bara na ya muungano ili yawe wazi na yashughulikiwe peke peke eti jeshi litakosa mishahara?

C'mon, Mwamunyange jitokeze kuonya wanasiasa waache kulichezea jeshi; la sivyo tutaamini na nyie ni watu msiotaka mabadilikokatika nchi yetu!

Nakuunga mkono kwa wazo lako hilo kwani muda si mrefu nimemsikia mchangiaji mmoja mnengua kiuno wa taarabu CCM anayejiita kapteni Komba katika mchango wake wenye majivuno, kejeli, vijembe na upungufu wa hoja mwisho akihitimiza kuwa kama wananchi wakiaamua serikali tatu "YEYE ATAINGIA MSITUNI", Cha ajabu wapumbafu wengine mle ndani wakamshangilia, hivi kweli kauli kama hiyo ni ya kushangiliwa?................................It is time for JWTZ to answer these rubbishes.
 
Ilipotolewa kauli kuwa nchi haitatawalika,tulisikia makaripio mengi tu. Sasa kama watu wanasema wataingia msituni kupigania s2 na hawakaripiwi, hapo inaashira nini kwa mustakabali wa Tanganyika yetu!
 
Nakuunga mkono kwa wazo lako hilo kwani muda si mrefu nimemsikia mchangiaji mmoja mnengua kiuno wa taarabu CCM anayejiita kapteni Komba katika mchango wake wenye majivuno, kejeli, vijembe na upungufu wa hoja mwisho akihitimiza kuwa kama wananchi wakiaamua serikali tatu "YEYE ATAINGIA MSITUNI", Cha ajabu wapumbafu wengine mle ndani wakamshangilia, hivi kweli kauli kama hiyo ni ya kushangiliwa?................................It is time for JWTZ to answer these rubbishes.
Hii kauli haiwezi kukanushwa na JWTZ,ilitolewa na amiri jeshi mkuu,na inavyoonekana ndiyo msimamo wa kamati kuu ya ccm make siku ile mhe alikuwa anatoa msimamo wa chama,wengine mtakuwa mnawasakama bure!!
Kombe angekuwa anajua msitu nadhani asingeimba taarabu,mwanaume wa bara kuimba taarabu ujue hata akili yake siyo!!
 
Captain John Komba akichangia Bungeni amedai Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawajatoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba

Sasa,kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote.

-Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim,Mzee Butiku na Mzee Warioba bado ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere.

-Huwezi kusema unamuenzi Mwalimu Nyerere kisha ukakubaliana na kauli za kifedhuli na vitisho vya kipuuzi kabisa vya Captain Komba .Bila aibu wabunge na mawaziri wanashangilia?

-Sasa natoa Rai kwa Viongozi na wafuasi wote wa UKAWA,tusikubaliane hata kidogo na Amri zinazotolewa na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano yetu.Kumbe kuzuia mikutano na Maandamano ni katika kutimiza malengo yao na kuminya haki za kiraia na kidemokrasia?

Katika mchakato huu wa kudai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili tulitakiwa kujadiliana kwa hoja na sio vitisho.

Captain Komba na CCM wenzake pamoja na Mawaziri waliokuwepo Bungeni leo watambue kuwa ndani ya Jeshi la Polisi kuna Askari wanaoguswa na harakati za kudai Tanganyika huru na Zanzibar Huru.

Ndani ya Jeshi la Wananchi watambue kuwa kuna Wanajeshi tena vijana wanaoguswa na hoja za kuidai Tanganyika huru na Zanzibar huru

-Nje ya jeshi na nje ya Bunge lipo jeshi kubwa la wananchi na hasa vijana wanaojiandaa kuidai Tanganyika Huru na Zanzibar huru

-Zama za kulazimisha Muungano wa serikali mbili kwa Vitisho zimekwishwa

-Captain Komba,wabunge na Mawaziri waliopo Bungeni leo wametuonyesha njia kwa rangi zao halisi.Tusirudi nyuma na tusiogope

Nyie kauli zenu huwa hamzioni enheee? mpaka kieleweke, nchi haitatawalika. Acha unafiki wewe. Ni bora ungewaacha wengine wakosoe lakini sio wewe uliyejaa uzandiki, ufitinishi, uchochezi, uongo uliopindukia, dharau, kejeli na ubinafsi.
 
kwani komba ujeshi ulukuwa kubana pua, alienda yule kupigana na amini....?
 
Nakuunga mkono kwa wazo lako hilo kwani muda si mrefu nimemsikia mchangiaji mmoja mnengua kiuno wa taarabu CCM anayejiita kapteni Komba katika mchango wake wenye majivuno, kejeli, vijembe na upungufu wa hoja mwisho akihitimiza kuwa kama wananchi wakiaamua serikali tatu "YEYE ATAINGIA MSITUNI", Cha ajabu wapumbafu wengine mle ndani wakamshangilia, hivi kweli kauli kama hiyo ni ya kushangiliwa?................................It is time for JWTZ to answer these rubbishes.

Mkuu.huyu jamaa hana jeuri ya kukimbilia msituni kama anavyodai na hata kiuhakika mtaani nako hana pa kukimbilia maake huko msituni kunakalika iwapo tu wewe unadhamira ya kweli ya kudai hicho unachokitaka lakini kwa huyu opportunisty siyo.
Hata huo ukapteni jeshini aliupata kwa kuimba kwaya na kucheza ngoma . kwasasa hawawezi hata kuruka matuta mawili ya viazi sembuse kuingia Msituni... asisubiri aingie sasa atambue kabisa kwamba wao wakiingia Msituni kutetea serikali Mbili wananchi tutaingia Mtaani kutetea serikali Tatu na pale watakapo amua kurudi mtaani kutoka msituni walikoingia watakuta nchi imekwisha kukombolewa.

Hawa jamaa wa ccm wanapenda sana mambo maovu na ndo yaliyo wajaza mioyo yao kilasiku wao waiamba vifo,mapinduzi,wizi,kungoa kucha ,kuteka nyara ,kuwa na silaha za kutosha ,kuacha unyonge na kujibu mapigo ilimradi tu wajaribu kurusha roho za wananchi.

Wananch tunahitaji Katiba Mpya iliyozingatia Mahitaji yetu .Kimsingi Bunge lililoko hapo Dodoma ukiondoa wabunge wa Jamhuri ya Muungano ambao kimsingi hawakuchaguliwa na wananchi kwa kazi hiyo hawa wakilishi wananchi hao ni wawakilishi wa Kikwete aliowachagua na si wananchi .Halina uhalali wa kubeza maoni ya Tume.Hata ongea yao tu inathibitisha kwamba wanamsifu ALIYE WATEUA.
 
Nyie kauli zenu huwa hamzioni enheee? mpaka kieleweke, nchi haitatawalika. Acha unafiki wewe. Ni bora ungewaacha wengine wakosoe lakini sio wewe uliyejaa uzandiki, ufitinishi, uchochezi, uongo uliopindukia, dharau, kejeli na ubinafsi.
ACT vipi msimamo wenu - mbili au tatu?
 
Huo msitu anaodai Komba ni msitu upi? Yeye ni mwimbaji na mshereheshaji vita gani aliyopigana? Aeleze Vita ipi aliyopigana. Watu wamepewa vyeo vya kupendelewa unamdanganya nani?
 
Captain John Komba akichangia Bungeni amedai Serikali Tatu zikipitishwa ataingia msituni kudai Serikali mbili.Wabunge wa CCM ambao miongoni mwao kuna viongozi wa Dini,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wanasheria,Waziri mkuu na Mawaziri akiwepo waziri wa Ulinzi ambaye anaongoza wizara inayosimamia Majeshi na vikosi vyote pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani hawajatoa kauli yoyote ya kukemea kauli hiyo na wamekubaliana na msimamo huo wa Captain Komba

Sasa,kama ni halali kuingia Msituni kudai serikali mbili basi ni halali kuidai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili kupitia msituni au kwa gharama yoyote.

-Kumshambulia Dr.Salim Ahmed Salim,Mzee Butiku na Mzee Warioba bado ni kumdhalilisha Mwl.Nyerere.Huwezi kumtukana Dr.Salim Ahmed Salim na Mzee Butiku (Viongozi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere) halafu uwe unamuenzi na kumuheshimu Mwalimu Nyerere.

-Huwezi kusema unamuenzi Mwalimu Nyerere kisha ukakubaliana na kauli za kifedhuli na vitisho vya kipuuzi kabisa vya Captain Komba .Bila aibu wabunge na mawaziri wanashangilia?

-Sasa natoa Rai kwa Viongozi na wafuasi wote wa UKAWA,tusikubaliane hata kidogo na Amri zinazotolewa na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano yetu.Kumbe kuzuia mikutano na Maandamano ni katika kutimiza malengo yao na kuminya haki za kiraia na kidemokrasia?

Katika mchakato huu wa kudai Tanganyika na Zanzibar yenye mamlaka kamili tulitakiwa kujadiliana kwa hoja na sio vitisho.

Captain Komba na CCM wenzake pamoja na Mawaziri waliokuwepo Bungeni leo watambue kuwa ndani ya Jeshi la Polisi kuna Askari wanaoguswa na harakati za kudai Tanganyika huru na Zanzibar Huru.

Ndani ya Jeshi la Wananchi watambue kuwa kuna Wanajeshi tena vijana wanaoguswa na hoja za kuidai Tanganyika huru na Zanzibar huru

-Nje ya jeshi na nje ya Bunge lipo jeshi kubwa la wananchi na hasa vijana wanaojiandaa kuidai Tanganyika Huru na Zanzibar huru

-Zama za kulazimisha Muungano wa serikali mbili kwa Vitisho zimekwishwa

-Captain Komba,wabunge na Mawaziri waliopo Bungeni leo wametuonyesha njia kwa rangi zao halisi.Tusirudi nyuma na tusiogope

Serikali mbili ni kama maji Ben, usipo yaoga utakunywa, usipokunywa utayafulia, usipo yafulia utatawazia etc
 
Hivi jeshi huwa ni mali ya wananchi ama chama tawala? naona maluweluwe kuona ccm wanaongea kwa niaba ya jeshi nijualo mimi ni la wanachi. Au kuna nini hapo katiokati?
 
Nyie kauli zenu huwa hamzioni enheee? mpaka kieleweke, nchi haitatawalika. Acha unafiki wewe. Ni bora ungewaacha wengine wakosoe lakini sio wewe uliyejaa uzandiki, ufitinishi, uchochezi, uongo uliopindukia, dharau, kejeli na ubinafsi.

Acha hasira
 
Back
Top Bottom