GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 57,115
- 110,505
Kuna taifa moja Duniani (kwa sasa nimelisahau) wao wameshakubali idara yao nyeti na iliyokuwa ikisifika miaka ya nyuma sasa kununulika (hasa watendaji wake baadhi ila siyo wote), kupenda na kupokea hovyo rushwa kwa tamaa ya kuwa matajiri hali ambayo inaihatarisha hiyo nchi kiusalama kwa siku zijazo.
Na hofu yangu zaidi GENTAMYCINE kwa hiyo nchi (niliyoisahau jina lake kwa sasa) ni kwamba, kama tu idara yao nyeti imeanza kununulika nunulika (kwa baadhi wa watendaji wao) wenye dhamana kubwa na kiapo cha kulinda maslahi ya taifa hilo, kirusi hicho pia kinaweza kupenya hadi katika jeshi imara na kali linaloheshimika la nchi hiyo (niliyoisahau) hasa idara yake (yao) ya CMI. Hivyo taifa lao hilo likawa ni mali ya mataifa mengine na hata maadui zake wakuu.
Nitoe tu pongezi zangu binafsi kwa idara nyeti za Tanzania (TISS) na Burundi (SNR) kwa kutokuwa idara nyeti pekee barani Afrika zisizokuwa na mapungufu haya niliyoyaelezea kwa utuo (undani) kabisa hapa juu.
Baba Mungu iponye hiyo idara nyeti.