mojax
Member
- Aug 18, 2015
- 13
- 23
ELIMU BIASHARA
NI UWEZO WAKO
Kufanya maamuzi mara nyingi huwa inategemea na nini kipo kichwani kwako na nini unafahamu kuhusu hicho kitu cha kufanyia maamuzi. Uwezo wa kutambua jambo na uwezo wa kutafakari na kulifanyia maamuzi hutofautiana baina ya mtu na mtu na ndio maana tunatofautiana hata level za maendeleo. Kwa kawaida uwezo huwa unapimwa na mafanikio, ukiwa unapanda cheo ofisini watu watajua una uwezo mkubwa wa kufanya kazi hivyo unastahili nafasi ya juu ofisini.
Swala huwa sio Fursa, swala huwa ni Uwezo wako wa kuona na kuitambua fursa, na kujua ni namna gani ya kuitumia ili kufikia mafanikio. Kwa mfano, Mtwara kinafunguliwa kiwanda cha Dangote, kila mtu anasema kutakua na fursa nyingi, na mimi nakubali, swala ni fursa ipi unaiona? Unaiona fursa ya ajira? Unaiona fursa ya kupata Tender ya kuwa agent wa kusupply cement zao? Unaiona fursa ya kufungua restaurant karibu na kiwanda uuzie wafanyakazi chakula? Unaiona fursa ya kujenga apartment wafanyakazi waje wapange? Unaiona fursa ya kununua kiwanja now ili baadae kikipanda bei ukiuze? Unaiona fursa ya kuandaa kozi ya environment and safety management kwa wafanyakazi wa viwandani? Unaiona Fursa gani?
Fursa zipo nyingi sana, swala ni una uwezo wa kuzifanya? Una uwezo wa Kuthubutu kuikamatia fursa moja ukaitimiza. Una uwezo wa kumshawishi mtu mkaingia joint venture mkafanya au utasema huna mtaji? Una uwezo wa kumshawishi mtu akakupa Mtaji uende ukaifanye? Je, una uwezo wa Kuifanya? Tusilalamike hakuna fursa bali tujifungue uelewa wetu na upana katika kuzifanya na kuzikamilisha Fursa zilizopo.
JIKUNG'UTE, JIPANGE, ANZA.
By Man Dea
#ElimuBiashara #ManDeaIdeas