Ni upofu tu

Mar 6, 2010
74
0
Ni Upofu!



Badala ya kutumia kichwa wanatumia moyo na matokeo yake ni upofu uliokithiri!
Hivi hujashangaa wachumba wanavyoingia kwa mbwembwe kwenye ndoa na Wakati mwingine haraka haraka na baada ya kuoana wanakumbana na kasheshe za kuwa watu wawili tofauti kabisa na kuanza kujishangaa hata imekuwaje.
Pia hujawahi kumuona rafiki yako anavyomsamehe mchumba wake (au hao mnawaita girl/boy friend) kwa tabia zake haribifu na zisizovumilika na zinazojirudia ambazo mtu anaziona na kila mmoja anashangaa inakuwaje anaendelea na urafiki kama vile haoni au kichaa fulani.
Au hujakutana na majuto ya mwanandoa mmoja akilalama kwamba
“Kama ningejua kile nakijua sasa kuhusu huyu mwanaume kwa kweli nisingekubali kuoana naye”
Au
“Sijua kama nilikuwa simfahamu kiasi hiki kwani sasa amekuwa mtu mwingine kabisa”
Hiyo mishangao ni ya watu au wanandoa ambao Wakati wa uchumba na partners wao walijiona ni watu wanaopendwa na kuwafahamu hao watu wao vizuri kuliko mtu yeyote duniani na sasa wapo kwenye Wakati mgumu kujiuliza kitu gani kiliwapata hadi wakashindwa kufahamu siri kubwa ambazo baada ya kuoana sasa zipo wazi.
Ukichunguza kwa makini utagundua kwamba hawa watu walikosa ufahamu (knowledge) ambayo ni muhimu kutumia ili kujua good marriage material ana sifa zipi au anapatikana vipi.
Ukweli ni kwamba ukitaka kumpata mchumba kuna njia mbili tu (approach) ambazo unaweza kutumia nazo ni kutumia moyo (heart) na kutumia akili (head)
Kutumia akili ni pale Binti au kaka anayetaka kuoa huamua kutumia akili na kufikiria kwa kuangalia kuangalia kufanana kwa familia ya partner anayemtaka na yeye (background), nafasi yake katika jamii, tabia yake, dini, utamaduni, jadi za familia.
Na kujtumia moyo ni kuweka msisitizo katika mapenzi (love), kuvutia, chemistry, muda wa pamoja, sex, ukaribu wa kimapenzi na romance.
Ukweli ni kwamba ili uwe na uwezo wa kumfahamu mtu ni lazima akili iwe timamu na ifanye maamuzi yake kwa kushirikiana na moyo na si moyo kuzama kwenye feelings za mapenzi ili kushirikiana na akili
Ukimpenda mtu na kuzama kwenye penzi lake maana yake umewasha moyo (una switch on feelings na emotions kwenye moyo ) kiasi kwamba moyo unaidhibiti na kuikalia, zuia, komesha, zimisha akili kufanya kazi yake (switch off) na matokeo yake akili haiwezi kufanya analysis ya informations zozote kuhusu huyo mchumba kama anafaa au hafai.
Ukianza kwa akili basi inakuwa rahisi kumfahamu mwenzi wako vizuri kwani akili ikiwa switched on moyo unakuwa na uwezo wa kusikiliza kile akili imeona kama anafaa au hafai na hapa ndipo kwenye tofauti kubwa ya ndoa na kutumia kichwa na kutumia moyo.
Ndiyo maana kutumia moyo kupata mchumba huweza kuwafanya wahusika kuwa kichwa maji, hata kama mtu unayemchumbia ana matatizo na jamii nzima inafahamu ana matatizo, kama mhusika amezama kwenye mapenzi na huyo mtu basi anakuwa kipofu hasikii la mtu.
Hapo ndo utasikia sentensi kama
“Ni kweli si mwaminifu ila ameniahidi tukioana atakuwa mwaminifu”
“Ni kweli ana matatizo ila mimi nimempenda sana”
“Ndiyo ana dini tofauti ila ameniahidi tukioana atahamia dini yangu”
“Ndiyo nasikia ni mhuni ila wanamuonea wivu tu”
Hizi zote ni red flags ukiingia kwenye ndoa na mtu wa aina hiyo jiandae na kupamba na hurricane category 5, hali itakuwa mbaya sana na pole sana kwani akili ipo suppressed na moyo hivyo haifanyi kazi bali mapenzi na si mbali utauona ukweli hasa baada ya kuoana.
“It is easy to get fooled when you are in love
 
Back
Top Bottom