Ni umri gani mtoto anapaswa kutembea?

mmmh happppo kwenye uzito duuuh wa kwangu miezi sita ana kg8.8 na sio bonge wala nini huyo msichana wa kazi usingemwambia akianza mchezo mchafu mtoto hatakua.. bali ungemwambia siku akifanya shughuli yake aoge kwanza ndio amshike mtoto tena umwambie kwa upole na taratibu.akuelewe...

Kweli kwenye huo uzito nao nafkiri pana tatizo, anakula na anashiba lakini? hebu muulize huyo Beki 5
 
dah! Pole sana ila kg 9 ni nyng mno na mwaka 1 na miez mitatu kasoro as wel ni ming pia! Hvyo kuna mawil either chakula anachokula mtoto hakina virutubisho vya kutosha na hasa madin ya calcium....au malezi ya mtoto kama ni mtoto wa kubebwa bebwa mda wote hi inachangia kwa kias kikubwa kupunguza kasi ya mtoto kutembea, jaribu kumuweka katk mazingra ya watoto waenzake wanao tembea!
Kila mtoto anakua kivyake,acha kulinganisha na wengine,hawana genetic material inayofanana,atatembea tu.
 
Watoto wanatofautiana hasa wale wa kwanza ni wazito kutembea na kuongea hii inatokana na kutokuwa na kampani ya watoto wengine . Usiwe na wasiwasi atatembea muda wake ukifika. Mimi mtoto wa kwanza hakutambaa na alitembea akiwa na mwaka na miezi mitano. Lakini wadogo zake wametembea mapema.
 
Usiwe na wasiwasi; so far hakuna cha kutisha. Watoto wanatofautiana sana. Na huyo wako kama unasema aliweza kusimamia vitu akiwa na miezi 10, ni dalili nzuri kuwa vioungo vipo ok. Most likely itakua ni woga tu. Inawezekana siku moja alijaribu akaanguka basi wapo watoto wengine, hasa wale wenye akili nyingi sana wale huwa hawataki kabisa risk za "kijingajinga" . Ni kama wanasema "kama naweza kutambaa, niharakishe kutembea nawahi wapi,...muda wenyewe wa shule bado,..."Jitahidi tu lishe; mkinge na maambukizi ya magonjwa kama malaria (my experience, motto akiugua homa kali katika stage hii, huwa anarudi nyuma sana katika maendeleo yake); na zaidi mwezeshe kupata company ya watoto wenzake wanaotembea (neighbours, relatives etc.) na mwombee kwa Mungu tu.Akianza kutembea uje utupe ushuhuda basi.
 
Asante sana gfsonwin kwa ushauri uliompatia jamaa hapo. Hata mimi mwanangu anafikisha sasa mwaka na wala haonyeshi mpango wa kutambaa achilia kutembea na ni wa kike...tumechanganyikiwa kiasi maana wenzake wenye umri sawa na wake sasa wanakaribia kutembea.
hebu mpeleke hospitalini ila angalia namna ya maisha yako. isije ikawa mtoto muda wote kafungiwa mgongoni na dada yake, hawekwi chini kucheza kama watoto wengine kisa unaogopa uchafu. au pia mtoto hana exposure kwa wenzie. lakini dietwise angalia kama ana anapata mlo wenye calcium vizuri.

mazoezi- mtoe nje kila jua linapochomoza kisha ukiwa na mafuta masaji miguu yake huku ukiwa unainyoosha ili kuiimarisha.

pia mnunulie kigari cha mbao cha matairi 3 kifunge jiwe ili kukitia uzito kisije kikamwangusha. jitahdi sana na mazoezi
 
Last edited by a moderator:
Hapa kuna mtoto katimiza mwaka mmoja jana.cha ajabu hajaanza kutembea.Anatambaa tu na kujivuta kwa kushikilia vitu na ukuta.Watu wengine wanadai km hadi sasa hajatembea basi hatatembea kamwe.
Kwani umri wa kutembea mtoto ni upi exactly,na nini husababisha wengine kuchelewa? Kwa anayechelewa kuna tiba yoyote?Na je kuna risk ya huyu mtoto kutotembea kabisa ie. Kuwa mlemavu?

Mwanangu wa kiume alitembea akiwa na mwaka na miezi 2. Usihofu sana. Cha msingi ni kuwa mkazanie mazoezi ya kutembea. Anunuliwe kile kigari cha kusukuma cha matairi 3, akimaliza tu chakula ameshiba anafanya zoezi la kutembea. Msisitize dada anayekusaidia kazi kumtembeza na kigari mara kwa mara.

Kama una baby walker ya kizungu asitumie sana hicho kigari cha miguu 3 cha mbao ndio kizuri zaidi kwa sasa.
 
Sasa wakwangu ana miezi nane ila ajaanza kutambaa akijaribu kutambaa anaanguka adi nimeisha ogopa.vip wangu ana tatizo lolote?
 
Asante sana gfsonwin kwa ushauri uliompatia jamaa hapo. Hata mimi mwanangu anafikisha sasa mwaka na wala haonyeshi mpango wa kutambaa achilia kutembea na ni wa kike...tumechanganyikiwa kiasi maana wenzake wenye umri sawa na wake sasa wanakaribia kutembea.

hata mimi mwanangu wa kwanza nimekonda nimebakia mifupa tu, hajatembea bado hadi watoto wa nyuma yake tayari
 
Usiwe na shaka ndugu hilo ni jambo la kawaida kabisa. Mwanangu wa kiume ameanza kutembea karibia mwaka na miezi 6 na hata kuongea alichelewa sana. Leo hii ana miaka 5 yupo gado ile mbaya. Tuliza pressure kama keshaanza kutembea kwa kushika ukuta basi ndo safari imeanza. Ukienda kuwauliza wazaramo watakutia pressure bure - watasema mtoto kabemendwa kumbe wala.
cheers!

nafarijika kwa kiasi fulani
 
Kweli kwenye huo uzito nao nafkiri pana tatizo, anakula na anashiba lakini? hebu muulize huyo Beki 5
Labda alizaliwa na kilo chache..mfano mtoto aliyezaliwa na Kilo 2 hawezi kuwa na sawa na mtoto aliyezaliwa na kilo 4.
 
Anayewahi Mara Nyingi ni ktk miezi tisa na anachelewa agharabu anafika hadi mwaka na miezi miwili. Sababu ni kwamba wato wengi huwa hawafanyiwi mazoezi ya viungo na mazoezi mengine mfano kukaa au kutembea. Unashauriwa asubuhi unakuwa unamfanyisha mazoezi na kumnyoosha nyoosha viungo vyake.

Tatizo la kutembea pia linasababishwa na wazazi kufanya mapenzi kabla mtoto hajakua vyakutosha (kumbemenda). Tatizo Hakuna ila ni aibu tu kuonekana kuwa hamumtendei mtoto haki yake na mara nyingi watoto hawa wana kuwa sio wachangamfu kama watoto wengine pia hata kiakiri.

N.B huu ni mtazamo wa kimazingira na hali halisi na sio wakitaalamu hivyo unaweza kukinzana na wakitaalamu.
Kwan ni muda gan unatakiwa kufanya mapenz baada ya kujifungua??
 
Back
Top Bottom