Ni umri gani hutakiwi kuvuka kabla ya kupata mtoto wa kwanza?

Mhn! hayaaaaaaa!
nikiwafundisha vijana kuhusu familia na uchumi na jinsi ya kuondokana na umaskini huwa nawashauri kama ifuatavyo:-
  1. kama elimu yako ni darasa la saba mpaka kidato cha pili na unafanya kazi ngumu (unskilled labour) kama unaendesha bodaboda unashauriwa kuona au kuanza familia ukiwa na miaka 24 kama umechelewa sana kwasababu umri wa kuingiza kipato kwa boda boda cha uhakika hakizidi miaka 45 na vifuatavyo ni vigezo vya ukomo wa kazi yake
    • wateja wengi alio nao ni wanawake walio na umri wa miaka 16-40 na wengi wao ni wadangaji hivyo kuwa na mteja mmoja mwenye safari zaidi ya tatu inawezekana. Pia katika kundi hili kuna wake za watu wasio waaminifu hivyo wanapiga day waka kipindi cha asubuhi na jioni kabla ya saa 12 jioni.
    • kwa hiyo katika umri huo anaweza kuwa na wateja wengi wa single mama akiwabeba pamoja na kuwapeleka watoto wao shule
    • baada ya miaka 10 mtoto aliye na miaka 8 aliyekuwa anampeleka shule akiwa darasa la pili ana 18 wakati bodaboda anamiaka 34 wakati mteja wa 40 ana 50 sasa biashara itakuwa kama ifuatavyo:-
      • yule mtoto aliyefikisha miaka 18 hawezi kuwa mteja wake tena labda yeye ageuke kuwa mteja kwa kuwa amepevuka na ameanza safari binafsi na vijana wenzake hivyo hawa hawapo.
      • wazazi wao walio kuwa na 40 wana 50 hawasomeki tena wamebakisha safari za kwenda kwa felloship na vicoba huku wakiendesha vigenge vidogo karibu na nyumbani (kwa lugha nyingine shetani kazeeka kawa malaika mdogo) wengi wanaokoka katika umri huu.
      • kipindi hicho atakuwa amebakiza miaka 11 na wateja wake hawaongezeki ila kupungua vinginevyo ashauriwe afanye shughuli zingine.
    • hivyo akioa akiwa na miaka 24 anaweza kupata mtoto(if other factor remain constant) akiwa na miaka 25 huku akiwa amebakiza miaka 20 inayoweza kumtosha kulea mtoto kwa miaka 7 na kumsomesha kwa miaka 7 sekondari miaka 6 na mtoto akienda chuo baba akiwa na 47 kwa mwaka wa kwanza.
    • hapo kidogo mtoto anaweza kuepukana na umaskini wa familia yake.
  2. kwa wale wenye shule inategemea japo kiukweli MWENYEZI MUNGU mpango wake kwa kila mtu. hivyo vijana msitoe mimba na wala msiwatoreshe watoto wa watu mimba kila japo lina fursa yake.
  3. kwa leo niishie hapo japo naweza kueleza zaidi kwanini iko hivyo
 
Mnatutesa kisaikolojia tuliochelewa kupata watoto, sio poa hata kidogo yani.
Relax maisha haya unafikiri yana formula mkuu ..basi tu ......ukianza kuwazawaza haya mambo ni kujipa pressure tu....relax ishi maisha yako
 
Brod darling haya mwambie Mungu nisamehe.

Aliyesema kuwa ukijifananisha na waliokuzidi vitu fulani hutoona jinsi ulivyobarikiwa au kui-appreciate baraka yako hakukosea. Hivi umeshawaza wanavyojisikia wale ambao hadi wanakufa uzeeni kwao hawakubarikiwa kupata watoto? Wale ambao walizaa mapema lakini leo hii wamezika watoto wote? Umewawazia wanaostruggle na infertility issues na hadi leo hawajabarikiwa kupata watoto?. Wangapi ambao wamevunja ndoa zao kisa kukosa watoto? Wangapi ambao wamekufa wakijifungua au wababa wamekufa wakawaacha wake zao wakiwa wajawazito? Regardless uliwapataje, na kwa wakati gani, em mshukuru Mungu. Huo unyonge wa nini, kuna raha kama kuitwa baba? Acha hizo brod darling, na wasalimie watoto wangu. Darling you are blessed
Mnatutesa kisaikolojia tuliochelewa kupata watoto, sio poa hata kidogo yani.
 
Miaka 26-28 kwangu watoto wanapishana miak miwili 2*4=8, 8+(26...28)=34,35,36. Kufikia hapo nabakiza malezi.
 
Brod darling haya mwambie Mungu nisamehe.

Aliyesema kuwa ukijifananisha na waliokuzidi vitu fulani hutoona jinsi ulivyobarikiwa au kui-appreciate baraka yako hakukosea. Hivi umeshawaza wanavyojisikia wale ambao hadi wanakufa uzeeni kwao hawakubarikiwa kupata watoto? Wale ambao walizaa mapema lakini leo hii wamezika watoto wote? Umewawazia wanaostruggle na infertility issues na hadi leo hawajabarikiwa kupata watoto?. Wangapi ambao wamevunja ndoa zao kisa kukosa watoto? Wangapi ambao wamekufa wakijifungua au wababa wamekufa wakawaacha wake zao wakiwa wajawazito? Regardless uliwapataje, na kwa wakati gani, em mshukuru Mungu. Huo unyonge wa nini, kuna raha kama kuitwa baba? Acha hizo brod darling, na wasalimie watoto wangu. Darling you are blessed
Nimesoma X2, asante sis darling...
 
Mtoto wangu wakwanza nilimpata nikiwa 20yrs NI wa kike....kwasasa yupo chuo ,2nd year!!!utafikiri n mdogo WANGU...sema TU sijaoa mama YAKE...NAJUA MUDA SI MREFU NITAANZA KUPATA RAHA YA KUITWA BABU...KUZAA MAPEMA RAHA
Hongera sana
 
Hili la mtoto lishaanza kunitoa nje ya reli

Nina miaka 28 sasa na ni mtoto wa kwanza,tupo wa4,wa3 wa kiume mmoja wa mwisho ni wa kike

Juzi Tu hapa sikukuu ya pasaka rafiki yangu niliyesoma nae kuanzia la 1 Hadi form 4 kaenda home kijijini Kula sikukuu na familia yake

Jamaa ana mke na watoto wawili,jumatatu akaniaga naenda home kwenu kumsalimia mamaako,nikamwambia fresh mpe hi mama.
Jana juma5 akarudi DSM akanipigia simu jioni tuonane nikamjibu poa nikirudi job nitakucheki

Saa moja usiku nikamkuta home kwake akaanza kunisimulia yaliyojili kijijini,na leo nakutana na huu Uzi

Akasema,ndugu yangu nimepata malalamiko sn kutoka Kwa mamaako ananiuliza mbona rafiki yako simwelewi,watoto karibia wote mliocheza nae mmeoa na mna watoto,Mimi najisikia vibaya sn mpaka Leo sina hata mjukuu,sasa ukienda kamuulize kulikoni
Leo umekuja na familia Hadi nasikia Raha lakini mwenzio akipata likizo anakuja yeye Tu hata sijaskia mama nakuja kitambulisho mchumba na haonyeshi hizo dalili za kufanya hivyo

Niliposikia haya maneno nilikuwa wa baridi sn,kumbe kuhusu kutokuwa na mtoto jamii inaweza kukutazama tofauti sn,pia mzazi anajisikia vibaya pia anapoona mwanae unachelewa kumletea mjukuu

Niliwaza sn maana sioni dalili ya kuoa wala kuwa na familia maana akiki yangu ipo bize kukimbizana na ndoto

Yaani sioni dalili ya kumletea bi mkubwa mjukuu labda demu anitegeshee nimpe mimba

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Same story to me. Tena mimi ilinitokea wakati ambapo jamaa yetu mmoja ambae tunatoka kijiji kimoja alifariki; so tukakusanyana washkaji kibao kwenda bush kumsindikiza mwenzetu. Shughuli ya mazishi ikamalizika, na kama kawaida watu wanafurahi kuwaona vijana wao... ikatokea tukawa tumeongozana na mama mzazi. Akaja mzee wa kwanza, akatusalimia then akauliza,"Vipi, kijana wako ameoa?" Mama akajibu huku anacheka,"Akuuuu!!! Muulizeni mwenyewe - si huyu hapa!" Nikabaki najichekesha chekesha tu. Akaja jirani yetu akasimulia kuhusu binti yake ambae tulisoma nae na saivi ana watoto watatu, wawili wanaishi pale kwa bibi yao; and strangely she was so happy kwamba binti yake amemwachia wajukuu wawili awalee. The fact is, unamuona mama wa watu kachoka, maisha yanamnyorosa - kiasi ambacho si sawa kuachiwa wajukuu awalee!! Kimoyo moyo I was like ...WTF!! Mwisho wa stori yake akaniuliza,"Sasa wewe kijana wetu unakwama wapi? Hatuoni unamletea mamaako hata kajukuu kamoja!". Haikuishia hapo, almost wazee 10 walikuja na stori hizo hizo.

Binafsi hainisumbui though kuna wakati najaribu kuvaa viatu vya mama na naelewa; Yeye amekua katika zama ambazo kuzaa ilikuwa ni kama jadi, kwamba ukifika umri fulani ni lazima uzae whether upo kwenye ndoa au la. Zama ambazo wakati mwingine wazazi wakiona hawakuelewielewi basi wanakulengeshea kabinti ili kujua kama wamekuza dume au nyuki wa mashineni. Hainisumbui kwasababu kwanza naamini katika kujiandaa kimaisha kabla ya kuzaa. Siamini zile za "Kila mtoto anakuja na sahani yake/ baraka zake." Kwasababu, wale waliotufundisha hizi imani wao wanaishi kwa akili, hawaishi kwa imani. Naamini mimi nimekua kwa kuungaunga kwasababu kwa kiasi fulani wazazi hawakujipanga kabla ya kuamua kuzaa. Malezi yana gharama (Na sizungumzii za kifedha tu.)

Naumia sana ninapoona watoto wa mitaani. Mtu anaweza akasema,"Ni Mungu amepanga, amechukua wazazi wake - so eventually lazima wawepo." Well, guess what - kama wazazi wao wangekuwa wamejipanga, wale watoto wangeweza ku-survive hata bila uwepo wa wazazi. Bahati mbaya sana watu ambao tunaunga unga maisha ndo tunakimbilia kufyatua watoto bila kujua watasomaje, watakula nini, watavaa nini, afya zao itakuwaje - na what if ukifa ghafla, wataishije? Na kwasababu hatupendi kufikiri, ukitoa hiyo hoja watakwambia,"Acha kujichuria! Ukiwa mwoga hivyo utaishije!"

Nilimwambia mama, sitaki nizae halafu wanangu waishi kwa kuunga unga kama nilivyoishi mimi. I know the experience ya kuunga unga, I have been there and I have done that; sitaki niuendeleze huo mnyororo. As long as ninaishi na nina akili timamu, sijali maoni ya watu ya kunipangia jinsi ya kuishi, sijali desturi zikoje kuhusu masuala ya umri na kuzaa, my life - my choices - my decisions and I have decided, sizai mpaka niwe tayari kwa malezi. Period!
 
Mdogo angu usijipe presha kabisa. Kila mtu ana timeframe yake, kila mtu ana njia zake; ingawa inawezekana tukawa tunaenda destination moja. Kwenye maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa, kila mtu ana wakati wake na ana bahati yake.

Rafiki yako kapata familia mapema, good for him; lakini sio sababu ya wewe kuwa pressurized. Hujapata familia au hujaamua kuwa na familia bado, good for you too.

Unajua mtu kutoamua kuwa na mtoto kwa wakati fulani; ni one of the most selfless decision, ingawa kibongobongo mtu akisema hajaamua kuwa na mtoto anaonekana wa ajabu sanaaa. Wengi wetu tunajisikia tu raha kuwa na watoto; tunapata fulfillment kwa watoto wetu. Lakini ni wachache au sio wote ambao tunawaza wellfare ya hawa watoto kabla hatujawaleta; wengi wetu watoto wetu hawapati fulfillment kwetu; ni vile tu ndiyo wameshazaliwa na sisi. Kuleta mtoto kunahitaji utayari wako binafsi na mwenzi wako, lakini pia mazingira sahihi sahihi ya kiafya, kihisia, kiuchumi na kiroho ya kumuwezesha mtoto kuishi kwa ustawi.

Usijisikie vibaya kwamba wenzako wanakwambia mimi nilizaa mtoto ujanani sijui niliwahi; ukweli ni kwamba sio kila mtoto anafurahia kuzaliwa huko ujanani. Sis tunaona raha, lakini watoto wetu hawaipata hiyo raha. Kuna wengine walizaa mapema lakini hao watoto hawakumbuki hata mara ya mwisho waliwaona lini, wengine wanalea watoto kwenye simu, wengine raha ya kuzaa ujanani basi wakafyatua watoto kadhaa kila mtu na mama yake; leo hakuna mtoto hata mmoja ambaye amemlea mwenyewe. Wengine wana watoto ambao hata kuwaclaim mbele za watu wameshindwa, wanasubiri wakifa ndiyo hao watoto waletwe, wengine baby momma's drama hadi inabidi na watoto wenyewe wawasamehe kwa muda waishi kwa amani huko walipo. Na majority ya hawa watoto wa ujanani ni watoto wa nje ya ndoa, sasa sijui kama na wewe unatamani uje uzae watoto wakalelewe kwengine, wewe uoe kwingine au ndiyo uishi naye zije na story za mama wa kambo/baba wa kambo. So mtu asikwambie tu ni raha kupata mtoto mapema; lakini akwambie ni raha kama wote mpo tayari kumleta huyo kiumbe, na mmemuwekea mazingira sahihi ya yeye kuja. Kabla hujamleta mtoto kwa sababu ni raha, make sure una uhakika wa kumpa familia (baba na mama mzazi, sio single dad au single mom), na mahitaji mengine ya kiroho, kihisia, na kiakili.

Hushindani na mtu, so ishi maisha yako; wakati wako ukifika na Mungu akakujaalia watoto basi itakuwa njema zaidi. Kwa kweli kupata mtoto ni raha, ila ili iwe raha pia kwa mtoto wako; basi hakikisha mnawaleta watoto kwa utaratibu na mazingira sahihi. So relax kabisa

Back
Top Bottom