Ni ubinafsi au ni chaka la maokoto lililokosa msimamizi?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kodi za Mtanzania hazijawahi kuheshimiwa na hii kwa kuwa kitabu alichokiita mama kinatoa Mwanya huo. Ukiangalia katiba ya JMT ibara ya 137.-(1) Rais atatoa maagizo kwa watu wanaohusika kuandaa na kuwasilisha kwenye Bunge katika kila mwaka wa fedha wa Serikali makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mwaka ujao wa fedha.

(2) Baada ya Bunge kuidhinisha makadirio ya matumizi (mbali na matumizi yaliyotozwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali kwa mujibu wa Katiba hii au sheria nyingine yoyote) Muswada utakaojulikana kama Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha utaletwa Bungeni kwa ajili ya madhumuni ya kuidhinishasuala kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali la fedha zinazohitajika ili kukidhi matumizi ya shughuli mbalimbali za Serikali inayohusika na makadirio hayo.

Hii inachochea matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali na kujikuta anayebeba mzigo mzito wa matumizi haya ni mwananchi.

Kwa Mwanya kama huo anatokea mke wa aliyekuwa Rais kwa influence ya ubunge wake bila kujali maokoto yake bado anataka wenza wao viongozi wastaafu walipwe stahiki kama wanavyolipwa waume zao. Maanake ni kujenga himaya ya kisiasa yenye ukwasi wa kutosha kujisimika katika maamuzi ya siasa za Taifa hili.

Hii Ina sababishwa na ubovu wa CCM usiozingatia Hali halisi ya maisha ya Mtanzania mbali na changamoto kubwa za kijamii mathalani elimu na miundo mbinu yake.

Na hapo dhana ya Shamba la bibi inapopata nguvu. Tumeamua kuwekeza kwenye kikundi kidogo cha wenye meno Kali na kuwaacha wananchi wakikaanga mbuyu.
 
Back
Top Bottom