Ni ubabe au? Bodi ya Mikopo wanakata mpaka 500,000/ kwa mwezi, watumishi ni kilio

Hapa watu wanashindwa kuelewa ,hivi kulipa deni kwa 15% kunakufanya ulalamike? Hizi asilimia siyo riba eti useme tulikopeshwa kwa riba ya 8% nasasa riba 15%, bali hiz % ni mfumo wa kulipa mkopo na siyo riba , sasa kinachotufanya kulalamika ni nini? Tulipe tuache tamaa! Watu wanaenda benki wanakopa mipesa mingi kwa mshahara wao huohuo na mwezi unaofuata anaanza kurejesha ,lakin bodi iliyokupa kibri cha kusoma hadi mwisho na umepata kazi hutaki kuilipa ,hapa akili zinatumika kweli au UJINGA MTUPU? wengine isingekuwq Bodi ya mikopo Tz tusingesoma! Kwahiyo mimi hata wakisema wakate 30% ,wakate tu si pesa yao bwana! Na kadri wanavyokata kubwa ndivyo deni linawahi kuisha ,sasa shida iko wapi?
TUTUMIE AKILI NA TUWE WASTAATABU, UKILIPA KUNA WADOGO ZETU NAO WATAPATA MIKOPO PIA KWAHIYO TUSIJISAHAU KUWA KUNA WENGINE WANAHITAJI HUDUMA ULIYOWAHI KUNUFAIKA NAYO.
 
Kila unapopanda daraja bodi nao wanapandisha makato kulingana na daraja husika
Hiyo si shida, ishu ni % mkuu. Sasa mkataba tumeingia nao 8% ambayo salary ikikua nayo inaongezeka, sasa ghafla wanaongeza to 15% bila concert wala kupeleka mswaa bungeni kuiweka kisheria; afu salary haikui na kodi zimeongezeka. Si utu!
 
Kinachoongelewa siyo kupewa mkopo, nadhani hamjaelewa hoja aliyoleta mwenzetu, kinachoongelewa hapa ni kwamba makato ni makubwa kiasi kwamba mfanyakazi huyu anashindwa kumudu gharama za maisha, na kama akishindwa kumudu gharama za maisha unategemea atafanya kazi kwa ufanisi? Mfano mwanzoni serikali walikuwa wanakata asilimia 8% ya mshahara wa mtumishi, ghafla tu serikali ikaongeza makato hadi asilimia 15% wakati hakuna nyongeza yeyote katika mshahara kama ilivyo ada kwa mwaka wa fedha. Kama yeye magufuli hakuongeza mshahara kwa watumishi wa umma qnapata wapi ujasiri wa kuongeza makato kwa watumishi wa umma, hakika huu ni uonevu usiovumilika. Binafsi nashangaa vyama vya wafanyakazi vimekaa kimya katika jambo hili
Mbona inapokuja hoja ya serikali kukata pesa yake mnalalamika, wakati mtu umepata kazi miaka nyuma hata ile hamu ya kusema nilipe deni uko hauna, upo kimya tu, bado unaenda benki unakopa kwa kutumia mshahara na unaanza kulipa immediatelly ,sasa wa muhimu hapa ni serikali alikupa mkopo kasoma na kupata degree na hiyo degree ikakufanya uapate kazi na kazi ndo inakuingizia mshahara kwa maisha yako ,au wa muhimu ni benki anayekupokelea mshahara wako kutoka serikalini na kukata pesa yake kwanza uliyomkopa na kubakiza chako cha TAKE HOME AMBACHO BADO HAKIKUKIDHI?
ukitambua ni nani wa muhimu hapa hakika hatutalalamika.
 
Unadhani wangetuambia mkataba ni kurejesha 15% tungeingia? Tungekomaa wenyewe tu ishu ni kwenda kinyume na makubariano. ILA NILIVYOKUSOMA FASTA INAONYESHA ULIMALIZA CHUO MWAKA JUZI NA BADO UNATEMBEA NA BAHASHA

Teh teh teh

Tokea mwaka juz?sasa hiyo bahasha si ni bora tuh angekwenda nayo kufungia vitumbua?

Maana uhakiki naskia ni zoez endelevu hadi 2020.
 
We kweli viroba vimekuharibu, contract ya HESLB unaijua? Kunasehemu imeandikwa makato ni 15% . Au ndo wale wanafagilia kila maamuzi ya baba J ili wapate nafasi ya kuteuliwa? Umeenda chaka wewe maana hata ujumbe wa sina la chama hawatakupa.
Contract ya HESLB iko wazi, makato ni 8% ,lakin isome vizuri kuna mahala imeelza kuwa makato yanaweza kubadilika pale itavyoamliwa na mamlaka husika kwa kibali maalumu kutoka ngazi za juu!
Kwahiyo rejea kwenye hicho kipengele! Tatzo tunasoma mikataba jujuu ,haafu wenzetu wanapokuja kuanza kutumia vifungu vingine tunabaki kulalamika na kipengele tulichoishia kusoma sisi!
 
...WANAFANYA VIZURI. NYIE WAKATI MNAKOPA MLIKUWA MWAJUA HAMNA KULIPA. WACHA FAMILIA ZILALE NJAA NDIO WAJUE KUWA WAZAZI WAO SIO WAAMINIFU. KWANZA INGEKUWA MIE NINGETIA JELA TUU
hizi ni side effects za dawa gani??
 
Mm nilikuwa nakatwa laki 6 na 37 elfu, nashukuru nimemaliza kabla ya hiyo 15% yao. Huu uonevu sana.
 
Siku zote masikini hutamani na kufurahia umasikini wake uendelee na Kwa wengine. Yaani wanafurahia kuona anaepiga hatua fulani anaanguka kwa namna yoyote,. UPUMBAVU MKUBWA SANA
mlipokuwa mnachungulia kwenye accnt zenu na kukuta zimenonamnafurahia eh,huu sasa ni wakati wa kulipa myavumiloe makato ili na wadogo zenu nao wanaufaike na hiyo mikopo,maana wwngine mlikuwa mnalewea na mabibi tu.
 
Kinachoongelewa siyo kupewa mkopo, nadhani hamjaelewa hoja aliyoleta mwenzetu, kinachoongelewa hapa ni kwamba makato ni makubwa kiasi kwamba mfanyakazi huyu anashindwa kumudu gharama za maisha, na kama akishindwa kumudu gharama za maisha unategemea atafanya kazi kwa ufanisi? Mfano mwanzoni serikali walikuwa wanakata asilimia 8% ya mshahara wa mtumishi, ghafla tu serikali ikaongeza makato hadi asilimia 15% wakati hakuna nyongeza yeyote katika mshahara kama ilivyo ada kwa mwaka wa fedha. Kama yeye magufuli hakuongeza mshahara kwa watumishi wa umma qnapata wapi ujasiri wa kuongeza makato kwa watumishi wa umma, hakika huu ni uonevu usiovumilika. Binafsi nashangaa vyama vya wafanyakazi vimekaa kimya katika jambo hili
serikali imeongeza makato ili mmalize mkopo mapema nyie mwalalama tu
 
Kama serikali isipoingilia kati nadhani huko mbele kuna fukuto kubwa sana!!

Hata kama ni ubabe huu umezidi

Ni wakati wa kupambana na hawa kupe

Watumishi hawa wataishije na familia zao?

Serikali inapenda pesa kuliko watu wake?
Serikali inayoongozwa na mtu aliyemteua Mac Conder unategemea itafanya maamuzi ya busara? Ngojeni kwanza Chato ikishakuwa jiji mtakumbukwa. Yaani umesimamisha nyongeza ya mshahara unaleta punguzo la mshahara!! Then mfalme anataka apigiwe vigelegele na kusifiwa kama nabii Suleiman popote apitapo na asikosolewe.
 
Kumbe ile asilimia 15 ndio imeanza kukatwa hivi sasa. Nasikia tu vilio kutoka kwa watu huku maofisini waliopata mshahara.
 
PATHETIC IT MYT BE BUT I TELL U THIS, U WILL PAY THAT 15% WETHER U LIKE IT OR NOT NOW USE UR BRAINS AND CHOOSE LOVE OR LEAVE TZ. SIMPLE. ELIMU TULISHAKUPA.
Why should i pay? Sijasomeshwa na serikali mimi, punguza stress maisha ndio haya haya
 
Kama serikali isipoingilia kati nadhani huko mbele kuna fukuto kubwa sana!!

Hata kama ni ubabe huu umezidi

Ni wakati wa kupambana na hawa kupe

Watumishi hawa wataishije na familia zao?

Serikali inapenda pesa kuliko watu wake?
Duuuh yaan 15 percent ya mshahara tu laki tano mbona huyo mtu anapokea mipesa mingi hivyo, huyo hawezi kufa njaa aisee huyo mshahara wake ni zaidi ya 3.5 milion, akibaki na 2million zinatosha sana kwa matumizi ya mwezi aisee sasa njaa atakufaje aisee
 
Daah jaman kweli hii awamu ni ya kupambana na watumishi wa umma 2020 tukutane hii ni vita baina ya serikali vs watumishi wa umma
Najua kwa sasa serikali ni washindi ila tutakutana mungu ni wetu sote

Tusiwaamini wanasiasa labda wakati wa kutaja majina yao tu

Hakuna ongezeko la mshahara hii tobo ya mwisho 2016/2017 inaanza

Zile push up zilimaanisha mengi sana JK WE MISS YOU
Mkuu na wewe ulidanganyika na zile push up ukauza uhuru wa maoni?
 
Back
Top Bottom