Ni sawa wizara kutumia kodi ya wananchi kutumika kwenye mazishi ya Kanumba?

Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa

I second you mdau..watanzania tuna manung'uniko sana!!
 
Tuache kuwa EMOTIONAL DRIVEN kama wanawake, serikali IMEKOSEA. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called FILAMU kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (Sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa Kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya SHIGONGO yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa UWAZI na IJUMAA ndio magazeti bora hapa Tanzania? (Lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa Kanumba 15m, kesho (kwa mfano, Mwenyezi Mungu aepushie mbali) akafa Juma Kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe MUHUNI. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya UDAKU utaona jinsi yalivyopambwa na habari za Fulani na Fulani wamelala chumba kimoja Nairobi, Uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, Sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, ETI HAYO NI MAFANIKIO KWA TANZANIA, nyooo! Kwendeni zenu huko

Uko sawa mkuu! Sema hii serikali yetu inafanana na maigizo hayo hayo, na nikuambie watu waliohudhuria kwenye msiba inawezekana ni hilohilo kundi la wanaopotea maana wapoteao ni wengi kuliko waokokao! Wewe fikiri mtu hamjui Kanumba zaidi ya kwenye filamu lakini anaanguka na kuzirai sababu Kanumba kafa! Ajabu hii! Hata mtu mwenye akili timamu atakushangaa sana, Wasanii hawajawa kioo cha jamii hata kidogo, ametembea na mtoto miaka 17, anakufa Wema Sepetu anadai bado walikuwa wapenzi kwa siri sema tu walikuwa wanaibiana maana kila mtu alikuwa na mpenzi wake mwingine....
Huu ni uchafu na zaidi ya uchafu! Sikatai watu wamtetee maana hakuna mtu asiyekuwa na watu wa type yake, kuvaa suti siyo ustaarabu wala kuendesha VX V8 siyo ndiyo umekuwa mtu wa juu sana maana wengi wamezipata kwa njia za ajabu ajabu..
 
Kwa hiyo hata kubaka vibinti vidogo ni kuitangaza vema nchi yetu? Acheni hizo sio wivu ila ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Wamekufa wangapi waliofanya mazuri kwa nchi hii mbona hawajatendewa hivi? Au mnataka kutuambia kuwa ukiondoa baba wa Taifa anaefuata ni Kanumba?

Hakubaka ila ni wapenzi
 
Laiti watu tungekuwa tunaijiua siri ya kifo, haya yote yasingetokea, ninauhakika asilimia mia moja marehemu kanumba angeliumwa na kuomba hizo hela zimsaidie katika matibabu sidhani kama huyu kiongozi angemuelewa anachosema, lakini kwa kuwa leo ni mfu basi ndio sehemu ya wao kuvujisha hela za watu wanaoshinda kwa mlo mmoja kwa siku, nadhani hata kanumba leo hii akafufuka sidhani kama itampendeza ila kwa sababu uhai haujirudi basi, serikali inahitaji kuja na majibu ya kutosha kutueleza watanzania kama kuna fungu ambalo hutengwa kwa ajili ya misiba au dharura vinginevyo huu ni uvujaji wa fedha za umma
RIP KANUMBA
 
Mi binafsi sioni mchango wa bongo movie kwani haziuziki kimataifa. Ni movie za very low quality na childish stories..mama mkwe hampendi mkwe..wifi hamtaki bi arusi..girlfriend kakumbia umepata mwingine...ujinga ujinga kama huo tu nothing serious. Wapenzi wa movie hizi ni wale wale wa magazeti ya udaku tu yaliyojaa fumanizi tupu. Walete data za mapato ya fedha za kigeni kupitia movie za Kanumba na kodi serikali iliyopata then tuone. Huu msiba ulikuzwa nadhani kwa shinikizo toka juu na ulikaa kiushikaji zaidi. To me he was not a hero but just another guy anayebangaiza kupata mlo wake. Thanks
 
mkuu ndoleha niko kwenye mobile ningekutwanga na LIKE ya nguvu.
 
Kitendo kilichofanyika ni cha busara,kubali ukatae Kanumba amewasaidia kwa njia moja ama nyingine vijana wengi kujiajiri kwa sababu ya kazi zake na pia amelitangaza soko la nchi yetu(la filamu) kwa kiasi kikubwa.usiwe mtu wa kupinga tu mambo ndugu yangu kama kusoma huwezi hata picha huoni,hawezi kuwa kama wewe kiukweli vinhinevyo uniambie ni nin ulishafanya kwa nchi yako chenye manufaa kimataifa

Raia wa kawaida kama wewe? Ni watu wangapi wanakufahamu wewe? Mchango wako ktk jamii ni upi?

Kanumba? Aaah' acha aende kijana wetu,ameifanyia makubwa sana nchi yetu!

Kama huwezi kuthamini mchango wa Kanumba katika nchi hii,basi hujui maana ya kutoa mchango wa Taifa Lako. Katika umri mdogo Kanumba ametoa mchango mkubwa kukuza ajira, ku-intertain, kueleimisha jamii, na kuitangaza vyema nchi yetu. Kumbuka waliko itoa Bongo Movies, kutoka maaigizo hadi kufikia kuwa Industry inayowaweka watu kibao mjini. Sisemi kuwa Industry imekomaa, lakini ilipofika inatia moyo. Mchango wa Kanumba ni mkubwa kuliko mchango wa wanasiasa wengi tu, ambao wanaiba fedha zetu na mwisho wa siku wanazikwa mazishi ya kitaifa. After all hizo unazoita fedha za walipa kodi si pamoja na Kanumba na Familia yake? Halafu watu kama ninyi ndo unaweza kukuta hata hiyo kodi hamlipi na hamna mchango wowote kwa Taifa hili. Hovyo sana wewe.

Nimejaribu kuquote wachache tu niliowapitia na kuona ni jinsi gani Taifa letu lilivyofilisika kimawazo!! Yaani mchango wa Kanumba ni mchango mkubwa kwa Taifa?? This is a joke of the century!!! Hizo movie zake ndiyo mchango mkubwa kwa Taifa........... wapi?? Zinaonekana wapi?? Duniani, Africa au EA?? Can't believe what I'm hearing here!!! Hivi kapata awards ngapi kwa hizo cinema zake?? Abroad watu walilizilalamikia kwa quality mbovu mpaka zimeondolewa M-net halafu mnataka kutudanganya hapa.
Hatukatai watu kuhudhunia na kuona huruma kwa kifo chake..........Hata mimi namuhurumia kwa jinsi alivyokufa mapema............ lakini hili la kutaka kumfanya HERO wa Taifa nitalipinga mpaka mwisho. Tanzania hatuna vipaumbele ndiyo maana watu kama akina Kanumba wanaonekana ni Heroes wakati akina Mahundi (IGP) na Kyaro (General) ambao mpaka walipigana Kagera wanasahaulika. Nafikiri TZ tungekuwa na Heroes acre CCM wangemzika Kanumba huko!!
 
kusema kweli naunga mkono. wanaopinga matumizi fedha za umma kwa masishi ya mtu ambae kimsing hakustahili na hiyo idhi ya kuzitua waziri kaitoa wapi? tufike mahali viongozi waheshimu kodi zetu. milioni 15 alizotoa nchimbi na milioni 10 za jk. zingeweza kununu vifaa vya maabala kwa watoto wetu. kweli tunajenga taifa la wajinga maana asilimia 80 ya vijana wanapata 0. na hao ndio washabiki wakubwa wa hizo zinazoitwa bongo move na magazeti ya udaku. hii nikwasababu hawajui kigireza hivyo hawawezi kulinganisha sinima za watu wengine na hizo takataka. kusema ukweli hizo sinema zimeachwa mbali na hata tamsilia kama lami vida shade of sine na nyinginezo. watu hawan utalaamu wowote na hata hsule na upeo wao ni mdogo sana leo ndio wanonekana mashujaa hadi raisi wa nchi anaacha shughuli za umma kwenda kwenye msiba. kweli tyanzania tumekwasha. labda salma anampenda hizo taka. maana nayeye kingireza hata cha kuombea maji hjui.
 
Tuache kuwa EMOTIONAL DRIVEN kama wanawake, serikali IMEKOSEA. Kanumba was just an individual na alichofanya si jambo linalokubalika na kila mtu.
1. The so called FILAMU kwa sasa imekuwa ndio kitovu cha uhuni na uasherati mkubwa kama huu uliopelekea kifo chake (Sipongezi, zinaharibu akili zenu)
2. Huyu anayesema msiba wa Kanumba umewagusa wengi, hicho si kigezo. Magazeti ya SHIGONGO yanasomwa na karibu wanawake wooote waliofeli form 4 na wasio na mwelekeo, je hicho ni kigezo kuwa UWAZI na IJUMAA ndio magazeti bora hapa Tanzania? (Lipime wewe mwenyewe kama una akili timamu)
3. Allocation ya fedha za serikali ina taratibu zake. Ikiwa leo kafa Kanumba 15m, kesho (kwa mfano, Mwenyezi Mungu aepushie mbali) akafa Juma Kaseja, serikali isipotoa 15m tutawaelewa?

Nionavyo mimi: Kuwa msanii hakumlazimishi mtu awe MUHUNI. Ukisoma headlines za magazetu yenu haya ya UDAKU utaona jinsi yalivyopambwa na habari za Fulani na Fulani wamelala chumba kimoja Nairobi, Uwoya kafumaniwa na mume wa mtu, Sijui nani kabakwa, yaani ni full upuuzi. Ikiwa haya ndio mnayoyaita maendeleo leo hii tukiwa wabovu kiuchumi kama nchi, basi tuna safari ndefu.

Wasanii wafanye sanaa na sio uhuni. Umaarufu kunuka huo mnaojivunia kwa kuwa nje ya nyumba za baba zenu saa 8 usiku ndio matokeo yake haya. Mtoto wa miaka 18 ana mabwana 6 hadi anawaua wengine kwa presha halafu mniambie mimi nikiwa na akili zangu timamu bila pombe, ETI HAYO NI MAFANIKIO KWA TANZANIA, nyooo! Kwendeni zenu huko
Ahsante sana, umeutakatisha moyo wangu. Rest in peace former CDF Generali Mwita Kyaro na IGP Harun Mahundi.
 
Mimi sishangai kwa sababu watu kama huyu mleta mada Never miss katika jamii yoyote hile
 
Nimejaribu kuquote wachache tu niliowapitia na kuona ni jinsi gani Taifa letu lilivyofilisika kimawazo!! Yaani mchango wa Kanumba ni mchango mkubwa kwa Taifa?? This is a joke of the century!!! Hizo movie zake ndiyo mchango mkubwa kwa Taifa........... wapi?? Zinaonekana wapi?? Duniani, Africa au EA?? Can't believe what I'm hearing here!!! Hivi kapata awards ngapi kwa hizo cinema zake?? Abroad watu walilizilalamikia kwa quality mbovu mpaka zimeondolewa M-net halafu mnataka kutudanganya hapa.
Hatukatai watu kuhudhunia na kuona huruma kwa kifo chake..........Hata mimi namuhurumia kwa jinsi alivyokufa mapema............ lakini hili la kutaka kumfanya HERO wa Taifa nitalipinga mpaka mwisho. Tanzania hatuna vipaumbele ndiyo maana watu kama akina Kanumba wanaonekana ni Heroes wakati akina Mahundi (IGP) na Kyaro (General) ambao mpaka walipigana Kagera wanasahaulika. Nafikiri TZ tungekuwa na Heroes acre CCM wangemzika Kanumba huko!!
Bila shaka kuna karata ya siasa ili kugain sympathy ya Kanumba's followers ambao majority ni udaku type. Kutokana na mfumo wa elimu wengi wamejikuta wamekwama katika kundi hili. Wanasiasa wakajionesha wako positive kwa jamii through Kanumba. Hivi ni tafiti gani zinazoonesha kanumba ameliingizia taifa fedha za kigeni kiasi kadhaa, au kodi kiasi kadhaa au amesaidia ajira kwa vijana kadhaa. Kama alivyotangulia mdau mmoja Kanumba was nothing but normal mbangaizaji through entertainment industry. Ingawa nakiri Kanumba kama angetumiwa vizuri na Serikali pamoja na sanaa ya film kwa ujumla wake wangeweza kuingiza mapato kwa fedha za kigeni kwa kuteka soko la Afrika mashariki na kati na ushahidi ni pale akina UWOYA walipofanya ziara CONGO DRC na kufunga mitaa. Kwa hiyo utaona demand ilivyo kubwa. Technically ni kwamba kiswahili kimecover eneo kubwa so hizi filam wakaazi wengi wanazielewa kwa hiyo jamaa wangefanikiwa kuongeza kifarans ktk tafsiri basi mauzo yangekuwa juu zaidi
 
Ulitaka ukale mchele tu eti eeh. wamezulumiwa sana kazi zao acha walipe mdogo mdogo.
 
Haaaaata, hiyo si sawa Serikali iache vitukooo! Kodi ya wananchi inapasa itumike kwenye mambo yaliyo na maslahi kwa umma. Ingawa Kanumba alikua ni msanii maarufu na aliyetoa mchango "mkubwa" kwa taifa, hiyo peke yake haiwezi kuhalalisha matumizi makubwa ya pesa ya walipa kodi kwenye mazishi yake. Kwa hakika wananchi wengi wanatoa mchango chanya kwa taifa kila mmoja kwa kiwango chake. Kama tutataka kugharimia mazishi ya mtu kwa sababu ya mchango wake kwa jamii, basi ili serikali itende haki basi itapaswa kutenga fedha nyingi nyingi sana ili kugharamia mazishi ya wananchi waliotoa mchango chanya kwa taifa wakati wa uhai wao kila mmoja kwa kadiri ya mchango wake. Hili halitawezekana hata kidogo.
 
mkuu serikali ya USA didnt contribute any cash towards the Michael Jackson funeral arrangements....this shows our govt is irresponsible
 
Whether it was right or wrong lakini serikali inabidi kuwa makini kwenye haya mambo maana inaweza kutengeneza precedent mbaya. Kesho anaweza akafariki msanii mwingine maarufu halafu serikali isichangie chochote. Kwa haki kabisa watu watataka kujua mbona serikali ilichangia kwa yule lakini siyo huyu.

Thanx mkuu..............na swali linabaki kuwa ni fungu gani la budget lilimegwa na lengo kusudiwa litakidhiwa vipi????

YA mheshimiwa Cheyo kuhusu pesa ya umma nadhani tumeyasikia tayari............and yet tupo fofofo eti katengeneza ajira kwa vijana......kwa mikataba ipi?? anachangia kwenye mfuko upi na nammba za hao waajiriwa ni zipi????

Kafanya aloyafanya well and good....public money should be well spent for the intended allocation
 
Yapi hayo makubwa embu tueleze,au kuwafanya akina Lulu na akina anti Ezekiel wafahamike hapa bongo?nahuko vijijini ambako ndiko kuna asilimia kubwa ya watu ,kipi wamenufaika na hizo filamu.Cha muhimu ni kumuombea jamaa apumzike mahala pema tu hayo mambo ya filamu ,filamu nyingi maudhui yake ni mabovu na za hovyo(sio filamu za marehemu tu bali zoooote),huwezi kuangalia sebuleni na watoto.Mimi nimeziona kwenye mabasi na hujaribu kutoziangalia,tukubali tu kila mtu na wakati wake na umaarufu wake,lakini la kusema kafanya makubwa kwa nchi hii haliniingii kichwani

Mkuu umenikumbusha(hapo kwenye red) kweli kama unapenda na kuta kuwalea vizuri watoto wako waweke mbali na bongo movie,na kibaya zaidi filamu zetu nyingi kama sio zote hazina zuio la umri(age restriction) hivyo basi ukinunua unaanza kuwa mara mbili mbili je niangalizie sebuleni au?. Nakumbuka juzi juzi nilikuwa na safiri na shabiby toka MBEYA waliweka hizo filamu yaani nilijuta kusafiri bora hood haina video.
 
Back
Top Bottom